Yondo Sister yupo hai? Naombeni historia yake

Kumfananisha Le Legend Diblo Dibala na Bwana Mdogo Dally Kimoko ( Dalikike au Gitare Ezanga Likwanza ) ni Sawa na Kufananisha Scania na Vitz! Gitaa la Dally Linasisimua ila Gitaa la Diblo Linatekenya na Kuburudisha Mpaka Ndege wa Mtini Hurukaruka. Ila Kwa Sasa Hao Wote Wamepotezwa Vibaya Sana na Vichwa Hivi Vitatu Vya Congo DRC Ambapo wa Kwanza ni Kijana Machachari wa Kundi Zima La Wenge Musica BCBG Chini Yake De la Patria Papa Chere JB Mpiana ( Bon Chic Bon Genre ) ikimaanisha Wazuri wa Sura na Wanaojua Kuvaa Aitwae Schevchenko Patou Solo huku Wa Pili Akiwa ni Kijana Mwingine wa Kundi Zima La Wenge Musica MM Chini Yake Le Roi De la Foree Werrason Ngiama Makanda ( Maison Mere ) ikimaanisha Nyumba Ya Mama Aitwae Flam Mwenie Kapaya na Wa Mwisho ni Kijana wa Kundi Zima La Quarter Latin Chini Yake Le Grand Mopao Le Maximone Large Degaire Koffi Olomide Aitwae Felly Tysone De ba Forme WAKATI Congo Brazaville Kuna Vichwa Viwili tu Kimoja Kinaitwa Cain Madoka Huyu Ukitaka Uijue Habari Yake Sikiliza Albam Ya Aurlus Mabele iitwayo Generation Wachiwa na Mpaka Album za Sasa Zote za Mabele Solo Kapiga huyo Dogo na Mtaalam Wa Mwisho ambaye hata Akina Diblo na Dally Wamemnyooshea Mikono ni Ibambi Ikombi Wengi Mnamjua Kama Roga Roga La Liberateur wa Kundi Zima La Extra Musica BPBL ( Bon Pied Bon Look ) ikimaanisha Wenye Mvuto wa Kimuonekano na Ukitaka Upate Habari Nzima Ya Roga Roga Sikiliza Album Hizi: Losambo, Etat Major, Shalai, Trosep Trop na Latest Album Yao iitwayo KINDOKI Ikimaanisha UCHAWI! Kwa Sasa Extra Musica Zimegawanyika ambapo Sasa Kuna Extra Musica Zangul iliyo Chini Ya Roga Roga na Ambaye ndiyo Le Orchestre President na Extra Musica International iliyo Chini Ya Fredy Nelson na Yule Repa Wao Kiboko Aitwae Mazikou Gislain ( Killa Mbongo ). Kila la Kheri!
 

Ya, hawa wote ni wazuri, ila ni wa kizazi hiki cha miaka ya tisini mwishoni kuja miaka hii ya elfu2. Wale hasa niliowataja ni generation ya nusu ya pili ya miaka ya tisini kurudi nyuma. Utakubaliana na mimi kuwa wakati ule Soukouss Stars inatamba Wenge hawa walikuwepo na vibao vyao vya mwanzo, vilikuwa vizuri, ila walizidiwa nguvu. Wakongwe walipofifia ndo wakaja Wenge BCBG( na kidogo Wenge el Paris) kabla ya kuja WengeMaison Mere, Extra Musica, G7 na wengine ambao inatajwa ni generation ya nne ya Congolese Music. Ile ya wakat ule ilikuwa ni generation ya 3, ingawa mtu kama Koffi amegusa kizaz cha 3 na 4 kwa kiwango kikubwa
 

Mkuu koooote umepatia ila kusema Diblo ni zaidi ya Kimoko sikubaliani na wewe! Angalia kimoko amefanya colabo na wanamuziki wangapi compared to Diblo.
Tukija ktk kizazi kipya there is no doubt Patou Solo anatisha, Framme Kapaya alivyokua WMM alikua moto wa kuotea mbali but kwa sasa hamna kitu,
NB: usiwasahau Kimbagu Solo, Japornaid, nao wanajitahidi
 

Kiukweli Dally Kimoko ni mkali dhidi ya Diblo Dibala
 

poa nimekusoma mkuu vp amezaliwa lin kaka?
 
umetisha Madame B ,daah cjui hata nisemeje...ila njoo hapa private watu wasi some...nikuulize viswali vichache tuu.
1. Kile kiuno(loketo) chake bado kipo vizuri hata kwa shepu tuu..naaaa la mwisho ni huyo mtoto wake amechukua nini hasa kutoka kwa mama yake? nijibu hapa private .
 
Santeeeee.Na
Nalog off
 
Yondo Sister hajafa.
Bado yuko hai na mtoto wake yule mmoja na pekee wa kike tunakaa nae huku Kinondoni Manyanya.
Jumapili iliyopita alikuja kumtembelea mwanae, ila amezeeka zeeka.

Mh! Kumbe unaishi manyanya! Ila mtoto wa Yondo haishi hapo. Ni wewe na wenzako ndo mnaishi hapo.
 

Isabelle hata mimi naikubali kinoma.
 
Kiukweli Dally Kimoko ni mkali dhidi ya Diblo Dibala
CHAZA......

Uzuri wa Diblo unadhihirika kwenye nyimbo nyingi.....Naomba nikuwekee hizi mbili hapa chini Tobina, Matchatcha Laisser Passer(ambao kuna sehemu gita linapigwa utafikiri limemwagiwa maji) na Extra Ball.......Kisha nikuombe uweke nyimbo ambazo unadhani Dally Kimoko amemshinda Diblo Dibala......




Mimi naona kwa kizazi chao hakuna anayemfikia Diblo Dibala mkuu wangu....Diblo yupo juu halafu wanamfuatia akina Dally Kimoko, Lokassa Ya Mbongo, Nene Tchakou, Allain Makaba 'Prince' , na Roga Roga (wa Congo Brazaville)......

Ni sawa na useme Gode Lofombo alikuwa ni zaidi ya Ngouma Lokiti katika kulikung'uta gitaa zito la bass.....
 
Last edited by a moderator:
Kwan DIBLO na DALLY KIMOKO nan zaid?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…