Yondo Sister yupo hai? Naombeni historia yake

Ghato mzima ila ameokoka anaimba injili!!
 
Ni extra ball au african ball?
 
Uko sawa mkuu kwa sababu wakati wimbo unaanza unamuona diblo mpini wake! Mie namkubali diblo
extra ball solo imepigwa na mchawi wa nyuzi Diblo Dibala Machacha .huu wimbo hata dally kimoko mwenyewe aliyoosha mikono kwa diblo
 

Diblo ni mchawi wa gitaa Africa hii.
 
Last edited by a moderator:
Diblo ni mchawi wa gitaa Africa hii.

Yaa, jamaa kachapa gitaa hatari. Diblo Diballa ni mkali tena sana. Ila kwa gitaa lenye ladha, Dally Kimoko ni hatari. Ladha yote tamu ya wimbo uitwao Madi-Yondo, Album nzima ya Soukouss Stars ile ladha ni yake. Si kwamba anakuwa peke yake, kwa mfano utakuta yupo na Lokassa Yambongo, tena na huyo Diblo wakati fulani walicharaza mpini.
 
Diblo ni mchawi wa gitaa Africa hii.

Kaka, hivi nani alipiga mpini wa nyimbo hizi: Evelyne-Aurlus Mabelle, Missete- Lucien. Leo pia tuwaguse Wenge BCBG. Kuna watu mi huwa wananikuna sana hasa album tatu za Wenge Musica BCBG chini ya Jean Badel Mpiana. Album hizo ni Titanic- Internet na Toujours Humble(TH) .Watu wenyewe wa kwanza ni Jules Kibens( le' professior), Alain Mpella( Afande), Aimelia Lyesse Demingongo, Chai Ngenge, Rio, Burkinafasso, Titina Alcapone ambae ni mpiga drums, lakini kwenye album ya Titanic alitunga wimbo uitwao Tour Eiffel(ule mnara maarufu wa pale jijin Paris). Nyimbo zifuatazo zina ladha tamu kuzikiliza kutoka kwa wenge bcbg! Nyimbo hizo ni: TH, Education, 48 Heures Gecoco,Walay Danico( hizi kutoka Album ya TH), Liberation, Tour Eiffel,Champion Kapangala, Omba( Album Titanic) na Internet, le' spo'ir de Chicago na love force za album ya Internet. Japo album za nyuma ambazo Wenge ilikuwa imetimia zilikuwa nazo ni nondo. Nyimbo kama pile ou face, no comment shenghen, Filandu, ndombolo, hi ho ha, kalayi boeing, masuwa, conse'il patcho, banalunda na feu'x d' la' mour utakubali jamaa walikuwa poa.
 
wabongo aisee, swali moja majibu kibaaaooo

Mtu kaulizia Yondo sister, kama kawaida wakware tunashusha data za akina diblo, sukus sijui na nini na nini

aisee:A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1:
 
wabongo aisee, swali moja majibu kibaaaooo

Mtu kaulizia Yondo sister, kama kawaida wakware tunashusha data za akina diblo, sukus sijui na nini na nini

aisee:A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1:

Ni kupitia forum unajazia nyama ili kuongeza wigo wa ufahamu, hivyo maelezo yakiwa ya ziada hayana athari zozote inakuwa bado siyo mbaya
 
wabongo aisee, swali moja majibu kibaaaooo

Mtu kaulizia Yondo sister, kama kawaida wakware tunashusha data za akina diblo, sukus sijui na nini na nini

aisee:A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1:
Kwani kuna ubaya gani? Au imekuuma?!
 

Champion Kapangala moto wa kuotea mbali,wakati huo Emelia anatisha, BCBG moto wa kuotea mbali
 
Champion Kapangala moto wa kuotea mbali,wakati huo Emelia anatisha, BCBG moto wa kuotea mbali

Pamoja mkuu. Mi ni mpenzi wa Wenge BCBG ya JB M'piana. Wenge Maison Merre mi siwakubali kiivyo, japo Werrason na Didier Masella , bila kumsahau Adolph Dominguez ndo hasa magwiji wa mwanzo kuanzisha Wenge, wakamwita JB M'piana nae kaifanya Wenge iwe juu. Ila ubinafsi wa JB M'piana wa kutunga yeye nyimbo karibia zote na kuimba yeye karibia nyimbo zote album ya Feu'x d' l'mou'r na mkwanja karibia wote kutia kapuni pekeyake kuliwakasirisha sana wenzake, na hivyo kuamua kujitenga. Werrason akaanzisha Wenge Maison Merre na kutunga album na wimbo: Force de Intervention Rapide( Jeshi la uvamiz linalokuja kwa kasi) na Wenge BCBG ikaja na Titanic kumaanisha meli ile iliyozama! Hapa utagundua walitumia Music kutupiana madongo
 

mkuu sio ubinafsi wa Jb mpiana, bali ilikuwa ni makubaliano kuwa kila mwanamuziki wa wenge bcbg atoe solo albam. ndipo jb akaanza kutoa project yake ya albam ya fex de lamour wimbo uliompa tuzo nyingi. albam hii maarufu kama ndombolo ya solo ikauza sana kuliko hata albam za wenge bcbg walizozitoa kama kundi, kwa kuwa alishirikisha baadhi ya wana wenge, wakataka waifanye albam ya kundi na wagawane mapato, jb akakataa, ndipo zilipoanza futina na zikiongozwa na werason ngiama makanda wa meison mere, akazushiwa jb ni mshirikia alienda hadi kwa mganga akanyweshwa damu ya mtu ili apendwe zaidi. na hii iliwauma baadhi ya wana bcbg hasa wale waliokuwa ndio waasisi wa bendi waliomkaribisha jb kisha kuja kuwa kinara zaidi yao. mwisho watu wakagawana mbao,meli ikazama, wengi ikamegika vipande, marie paul akaanzisha bendi ya wenge el paris, werason akaanzisha wenge meison mere,baadaye adolf domingize akaanzisha wenge tonyatonya,blaize bula nae akatoka kivyake.
ila kiukweli bendi zilizitakana na wenge bcbg ziliziweza kusimama mpaka sasa ni ya wenge ya werason na jb mpiana.
sasa kati ya wera na jb, wera son akabaki kuwa sio mtunzi mzuri wala muimbaji mzuri bali ni muandaaji wa show nzuri,kwa masebene tu na uchezaji wako vizuri kuliko wenge ya jp mpiana. kwa upande wa wenge ya jb, jb mpiana ameendelea kuonyesha kuwa yeye ni mtunzi na mwimbaji bora na imethihirika wazi kuwa yeye ndiye aliyekuwa anaibeba wenge bcbg 4x4 by far kabla haijavunjika kiumbaji na kimpangilio wa muziki.jamaa ni mpangiliaji mzuri saana wa muziki na mwinbaji mzuri. tafuta show ya jb live at kinkole ndio utajua jb ni nani
 

Da nimefurahi sana kaka! Naipenda ile live show ya Zenith1999, ilikuwa bomba sana. Wimbo wa Papito mbala version, ulirefushwa na kuwekewa manjonjo( nadhani ni show ya olympio) kwa ubunifu wa sauti JB ni mtambo na ndo maana alifanya kazi hadi kumnasa Jules Kibenga/ Kibens. Kwenye wimbo wa Moh'd Kanyasi aliimba vizuri ubeti wake akiwa amevalia suti nyeupe. Wengine ambao JB anapongezwa kwa umahiri wa kuwatumia watu ni Fi Care, na Genta. Fi Carey ana sauti ya base na alitunga wimbo uitwao l'e spoi'r de Chicago, ni wimbo mzuri sana kwenye album ya internet, unaweza kugoogle wimbo huo na kucheza kwa you tube. Jamaa aliyenyoa panki kama kiduku na kuvaa suti nyeusi ndo huyo Fi Carey. Genta anarap pamoja naTutu Calugi kwenye wimbo wa Internet, ni bonge hivi! Alain Mpela( Afande) nae anaimba na kwa kiasi kikubwa alihusika kuipaisha Wenge BCBG ya JB M'piana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…