You are available for 105%. Ntahamasikaje kukuoa?

You are available for 105%. Ntahamasikaje kukuoa?

tupe tupe vidonge mkuu na kale katabia mtu anafikia hatua ya kutosa gari la ofisini anamsubiri mupenzi ampitie ili amuone kipenzi tu .....mh.....! nako kanakinaisha
 
Tuheshimu hizi semi za wahenga... mfano; "if you can get a free milk", why keep a dairy cow?"...

Hii inawahusu sana wadada (probably na wanaume)

Jaribuni kuwa na mvuto, walau wanaume zenu wajisikie kuwamisi...

Unakuta mdada ni girlfriend tu, au mchumba basi...

kila siku yuko kwa mwanaume, kama mwanaume anakaa mwenyewe basi kila siku mdada anaenda kufanya usafi, kufua, kupasi, kupika nk, nk.
Kila siku mdada yuko pale, available for sex kwa staili na manjonjo yote...
Kila wikiendi mdada anashinda kwa mwanaume...
Akipigiwa simu hata saa sita za usiku, yupo radhi atoroke kwao, aende kwa mwanaume...
nk.nk...

Hata kama unampendaje mwanaume wako, jaribu kuonyesha kuwa unajiheshimu kama msichana ambaye hajaolewa, na mwanaume akitaka vyote, basi akuoe. Sisemi kwamba muwanyime sex, bali sio mnawapa hadi wanakinai... Sisemi kwamba msiende kwao, bali nendeni kwa ratiba, mkionyesha kuwa mna mambo mengine ya binafsi ya kufanya...

Unakuta mwanaume anakukinai kabla hajakuoa, unadhani atahamasika na nini kukuoa?
Mwanaume anataka mke mwenye maamuzi binafsi, sio anayefuata tu upepo wake...
Mwanaume anavutiwa kuoa mwanamke mbunifu, anayejituma... kama uko shule akikuita sometimes umwambie no, nina assignment au najisomea nk... Kama uko tu kwenu akikutaka kwake sometimes umwambie no, unawafundusha wadogo zako, au unajifunza kitu fulani, au unapika, au unaplan kuanzisha biashara yako...

Inatakiwa ucreate hali fulani ya mwanaume kukumiss, na kuona umuhimu wa kukuoa ili afaidi 100% ya kuishi na wewe...

Try to be available only for 30% ya mahitaji ya mwanaume kwako...

Halafu mwisho wa yote, wanalazimishia na kubeba mimba kabisa ili wapate tiketi ya kuolewa haraka haraka, jamani, hebu jitunzeni na kijilindia heshima zenu!!! :A S wink:
 
Angalizo usifikiri kujifanya unanata/au unakwenda kwa mpenzi wako kwa nafasi yako itaonyesha unaheshima/unajiheshimu!kuna baadhi ya wanaume kama alikuwa na kiu na wewe na unaleta za kwako anatafuta kitu cha kuondoa njaa yake,sasa uombee asivutiwe maana mwingine anapata kifaa cha ukweli na anahamia jumla.Let me tell u something guys kwa uzoefu wangu haya maswala nionavyo ni kuwa hayana formula,swala la kuolewa/kutoolewa kila mtu ni ki-vyake vyake.
 
Kwa kweli kukinahi nako tabu,wanawake wengne ving'ang'anizi anaona mwanaume hana mpango kabisa wa ndoa bdo yy anang'ang'ania kunijibebesha mimba matokeo yake anaachwa na mimba yake au mwanaume anahudumia kila kitu mpaka anampangia nyumba nzima na kila kikorokoro anamuwekea ndani bado anamwambia anaoa mwanamke mwingine ambaye ni chaguo lake....jamani wanawake msiwe km wajinga mnajishauri ujinga matokeo yake u suffer with the consequences of ur choice..
 
Sinunui hii idea hata punje moja.

kama sababu za kuoa mwanamme ni hizi tu, then hanifai, he is not a man enough for me.

Hivi mwanamke mnamchukuliaje? Chombo cha starehe tu? au chombo cha kurahisisha maisha ya mwanamme?

Kwa nini haya basi asiyafanye mwanamme? Kwa nini yeye asinchenge mie
Kwa nini unadhani mwanamme ndo anamkinai mwanamke na si mwanamke anamkinai mwanamme?

Na unadhani anayetaka ndoa ni mwanamke tu?

With ndoa au bila ndoa, i will be proudly myself, siwezi jibana kuishi eti kisa nim-impress mtu mwingine, khah!

Anyway, expectation za ndoa zinatofautiana kati na mtu na mtu.
 
1+1=11 !!!! endeleeni mi come here later! lol!
 
.....animal instincts, marking territory.....acha wabanane bana, si unajua "kunguru hafugiki?" kaba mpaka penati...
 
.....animal instincts, marking territory.....acha wabanane bana, si unajua "kunguru hafugiki?" kaba mpaka penati...

hahaaa... Hivi mbu ulishawahi kutamani siku moja walau wife apate kasafari ka siku tatu?...
 
hahaaa... Hivi mbu ulishawahi kutamani siku moja walau wife apate kasafari ka siku tatu?...

.....mara nyingi sana aisee, 😀 pheeeww....."uhuru" mtamu wa ku'recharge' battery aisee..
 
Short and clear.
MAPENZI HAYANA FORMULA.
Hakuna taratibu ambazo mwanammke anaweza akazipitia/akazizingatia ili ajijengee mazingira ya yeye kuonekana ni mzuri kwa kuolewa hatimaye akaolewa na pia hakuna vigezo ambavyo mwanaume anaweza akavitumia katika kumpata mke bora atakayemfurahia muda wote.
Mapenzi hasa katika ndoa ni kama effect ya kuondesha gari ukiwa umelewa.It is not a fact kama ukilewa na ukaendesha gari basi utapata ajali,ndivyo mapenz navyo yalivyo mtu unaweza ukamuona huyu kwa tabia hizi hatoolewa mwishowe akaolewa na akafurahia ndoa kuliko yule anayeonekana kwa tabia zile anafaa.
Kwa hiyo mtoa mada wacha vijana wafanye wanavyohisi ni sahihi kwa kuwa HAKUNA USAHIHI.
J is out.
 
Haya mambo hayana formular, la muhimu ni kumsoma mtu wako ujue anapendelea vitu gani ndo ufanye hivyo, wapo wanaume/wanawake wengine hawapendi kugandana na wapo wanaopenda mapenzi ya kugandana....so angalia uliko na ujue nini mwenzako anapenda ili kuepuka kuchoshana
 
wazee wetu walipoamua kuwa tusimegane mpaka ndoa zifungwe hawakuwa wajinga, walikuwa wanaona mbali, sasa huu utandawaz unatuponza, mi huwa nacheka unakutana na mtu anaishi na jamaa halafu anakwambia ni mchumba na mtoto tayar wanae,
 
Maneno kuntu hayo Tuko; ndoa gharama kama unaweza kupata yote bila gharama why not?

Na ukimganda mtu sana unafanya aamini kuwa bila yeye hakuna anayeweza kukutokea; ni nzuri kumweka mtu roho juu uone kama hatangazi ndoa kwa hofu ya kuwaiwa.

My husband proposed to me when I was surrounded by the most eligible bachelors, with interest in me of course. Lol.
Na alienda kwetu wakati mi niko safarini; nikajua tu ni wasiwasi wa kupigwa chini any time t, toka nilivyoanza kazi jamaa kawa hana amani kabisa. Lol.

Tuheshimu hizi semi za wahenga... mfano; "if you can get a free milk", why keep a dairy cow?"...

Hii inawahusu sana wadada (probably na wanaume)

Jaribuni kuwa na mvuto, walau wanaume zenu wajisikie kuwamisi...

Unakuta mdada ni girlfriend tu, au mchumba basi...

kila siku yuko kwa mwanaume, kama mwanaume anakaa mwenyewe basi kila siku mdada anaenda kufanya usafi, kufua, kupasi, kupika nk, nk.
Kila siku mdada yuko pale, available for sex kwa staili na manjonjo yote...
Kila wikiendi mdada anashinda kwa mwanaume...
Akipigiwa simu hata saa sita za usiku, yupo radhi atoroke kwao, aende kwa mwanaume...
nk.nk...

Hata kama unampendaje mwanaume wako, jaribu kuonyesha kuwa unajiheshimu kama msichana ambaye hajaolewa, na mwanaume akitaka vyote, basi akuoe. Sisemi kwamba muwanyime sex, bali sio mnawapa hadi wanakinai... Sisemi kwamba msiende kwao, bali nendeni kwa ratiba, mkionyesha kuwa mna mambo mengine ya binafsi ya kufanya...

Unakuta mwanaume anakukinai kabla hajakuoa, unadhani atahamasika na nini kukuoa?
Mwanaume anataka mke mwenye maamuzi binafsi, sio anayefuata tu upepo wake...
Mwanaume anavutiwa kuoa mwanamke mbunifu, anayejituma... kama uko shule akikuita sometimes umwambie no, nina assignment au najisomea nk... Kama uko tu kwenu akikutaka kwake sometimes umwambie no, unawafundusha wadogo zako, au unajifunza kitu fulani, au unapika, au unaplan kuanzisha biashara yako...

Inatakiwa ucreate hali fulani ya mwanaume kukumiss, na kuona umuhimu wa kukuoa ili afaidi 100% ya kuishi na wewe...

Try to be available only for 30% ya mahitaji ya mwanaume kwako...
 
Yawezekana mapenzi hayana formular, lakini kumbuka tahadhari inampa mtu akili (which can also be a formular in same touch)....ya kujua afanye nini. Na ndo maana huwaga tunajistukia.....hapa sikufanya hiki or hapa nimekosea au nimesababisha mwenyewe and so forth.

Thenafter.....I do concur with Tuko's explanation as a helpful guideline!
 
Hivi wanawake tu ndo wanaotakiwa kuwaimpress wanaume??kwani wanaume hawatakiwi kujijengea mazingira fulani ili na wapenzi wao wawamiss??hivi kwani wanawake hua hawawachoki wanaume??sielewi ati!
 
Back
Top Bottom