You must be kidding me! - 21.9Millions USD?

You must be kidding me! - 21.9Millions USD?

MwanaKijiji your assesment is politicaly and Economicaly wrong. Ki Uchumi , Kiwanja chaMpira cha Dola Milioni 50 Kinafaida kiuchumi kuliko milioni 170 tulizokopeshwa na IMF na zikaishia kwenye mikono ya mafisadi.WAkati tunazidi kupata hasara ya kuservice Intrest ya pesa zilizoibiwa na mafisadi kiwanja kitakuwa kinaongeza tija ya michezo Tanzania.

Pili Fedha zote ulizozitaja hazina Economic Value kwenye nchi yetu kwasababu zimefichwa nje ya nchi na mafisadi hivyo Basi hakuna faida yoyote tunayoipata.

Politicaly China policy to Africa is the right one, Wanajua viongozi wetu ni mafisadi kwahiyo wakitoa pesa wanaleta watalaamu wao na wanhakikisha mradi uliokuwa proposed umetekelezwa ,I bet u kama China ingekuwa imeipat hiyo milioni 50 ya Ujenzi wa kiwanja cha mpira serikali mpaka sasa usingeona kiwanja,

Pili hizo milioni 20 walizotoa kwa ajili ya kujenga hospitali ninauhakika zitajenga hospitali kwababu watasimami na kuahakikisha zinafanya kazi.

Tatu, Ukilinganisha mkutano wa kibiashara wa wachina na watanzania uliofanyika mwaka jana ngurudoto na mkutano ulifanyw kuwa wa biashara wa sullivan summit, ninakuhakikishia watanzania walifaidika na ujio wa wachina kuliko sullivan summit

Mwisho ninachojaribu kukuambia ni kwamba, ,Msaada ukitolewa Tanzania haijalishi kiasi ila kinachojalisha ni usimamizi wa utimizaji wa lengo la msaada huo

Therefore my valuation tells me that the chines aid has more Value than ur mentioned stolen moneies
 
Okay, is that rocket science? Do you have to be Albert Einstein to come up with even a few?

You don't have to be a super genius to come up with a few things. Lakini kuna uwezekano mwingine matatizo yetu yamo coded kwenye DNA zetu.
 
MwanaKijiji your assesment is politicaly and Economicaly wrong.
I like this one.. very bold claim!
Ki Uchumi , Kiwanja chaMpira cha Dola Milioni 50 Kinafaida kiuchumi kuliko milioni 170 tulizokopeshwa na IMF na zikaishia kwenye mikono ya mafisadi.
Kiwanja cha dola milioni 50 kina faida zaidi "kiuchumi"? Hapa ungejaribu kuonesha kuwa kiwanja hicho kinagharama ya kiasi gani kukiendeleza na kukisimamia, halafu linganisha na mapato yanayoweza kupatikana na matumizi ya uwanja hao.

Kwa vile hela iliyotumika karibu nusu ni ya mkopo basi gharama yake kwetu yaweza isiwe kubwa sana.

Hata hivyo, kusema kuwa kina faida zaidi kuliko fedha za dola milioni 170 zilizoibwa na mafisadi ni kutokuelewa ile opportunity cost. Gharama kubwa ya sisi siyo fedha kuibwa bali kile ambacho hakikuwezekana kufanywa kutokana na wizi huo.

Nitakupa mfano; kama kumtibu mgonjwa wa moyo kwa kumfanyia upasuaji ni dola elfu 20,000 na sisi tukazembea na kumuacha mtu aibe dola elfu 20 na kuzifanyia apendavyo. Mgonjwa wetu akafa kwa kukosa matibabu kwa sababu hatuna fedha; wakati huo huo hata hivyo, tumepata dola elfu 40 za kujenga kliniki kiasi ambacho pia kitachomolewa vya kutosha kuishia kwenye ulaji. Gharama, kwa mtu mwingine atasema kuwa kliniki ina thamani kubwa. In the future yawezekana lakini sasa hivi, gharama kubwa iko kwa kukosekana elfu 20,000 kwani mgonjwa amekufa!

Ipo gharama kubwa zaidi ya ufisadi na gharama hiyo huwezi kuioffset kwa kutujengea uwanja wa mpira ambao malipo yake kuleta faida itakuchukua miongo mingi tu.
WAkati tunazidi kupata hasara ya kuservice Intrest ya pesa zilizoibiwa na mafisadi kiwanja kitakuwa kinaongeza tija ya michezo Tanzania.
Kwa mechi gani? Hapa ungenipa mfano kuwa uwanja ule umeweza kuingiza kiasi gani kwa wakati mmoja na mechi ngapi kama hizo zinatakiwa kufanyika hapo na kuhakikisha kiasi hicho kinapatikana? Hapa tunaweza kupata kitu cha kulinganishia.
Pili Fedha zote ulizozitaja hazina Economic Value kwenye nchi yetu kwasababu zimefichwa nje ya nchi na mafisadi hivyo Basi hakuna faida yoyote tunayoipata.
economic value yake siyo kwa kile fedha hizo zimefanya bali kile ambacho zimeshindwa kufanya!!
Politicaly China policy to Africa is the right one, Wanajua viongozi wetu ni mafisadi kwahiyo wakitoa pesa wanaleta watalaamu wao na wanhakikisha mradi uliokuwa proposed umetekelezwa ,I bet u kama China ingekuwa imeipat hiyo milioni 50 ya Ujenzi wa kiwanja cha mpira serikali mpaka sasa usingeona kiwanja,
utaona kuwa sina tatizo hasa na policies za china bali sera yetu ya kuomba omba pasipo ulazima wa kuomba. Kwa upande wa China tatizo langu ni kuwa wao hawajali nini kinafanyika ndani ya hiyo nchi. As long as wanachotaka kinafanyika basi wao hawajali kama tutachinjana n.k (tumeyaona Sudan haya!)
Pili hizo milioni 20 walizotoa kwa ajili ya kujenga hospitali ninauhakika zitajenga hospitali kwababu watasimami na kuahakikisha zinafanya kazi.
Hivi unadhani tatizo liko kwenye kujenga hospitali? what happens after wamejenga hospitali?
Tatu, Ukilinganisha mkutano wa kibiashara wa wachina na watanzania uliofanyika mwaka jana ngurudoto na mkutano ulifanyw kuwa wa biashara wa sullivan summit, ninakuhakikishia watanzania walifaidika na ujio wa wachina kuliko sullivan summit
umechelewa mimi niliupinga huo wa Ngurdoto na kuonesha kuwa ulikuwa ni wizi wa mchana kweupe.

Mwisho ninachojaribu kukuambia ni kwamba, ,Msaada ukitolewa Tanzania haijalishi kiasi ila kinachojalisha ni usimamizi wa utimizaji wa lengo la msaada huo
Hapo ndipo tunapotofautiana, misaada mingine ni misaadaa ya kijinga. Kama kuna kitu unaweza kufanya wewe mwenyewe kwanini uombe msaada! Kama unazo milioni 21 (kwenye Kagoda kwa mfano) kwanini uombe milioni 21 kutoka kwa Wachina kana kwamba hauna kitu?

Therefore my valuation tells me that the chines aid has more Value than ur mentioned stolen moneies
Hayo mawazo ya kwako ndiyo yanawafanya mafisadi kuendelea kutafuna na kumung'unya wakijua kuwa wachina watakuja na misaada yao! Ni mawazo ya kupingwa.
 
Hamna kitu mbaya kama kuzubaa kimawazo Watz wenzangu!

Kuwa omba omba yaani ..kupitisha bakuli eti naomba unisaidie...naoamba mimi unifikirie...kwa nchi yenye raslimali watu ni aibu..na tunajidhalilisha!

Hakuna atakayetuheshimu duniani kwa vile sisi tunapenda Umatonya!!!!!
 
Hamna kitu mbaya kama kuzubaa kimawazo Watz wenzangu!

Kuwa omba omba yaani ..kupitisha bakuli eti naomba unisaidie...naomamba mimi unifikirie...kwa nchi yenye raslimali watu ni aibu..na tunajidhalilisha!

Hakuna atakayetuheshimu duniani kwa vile sisi tunapenda Umatonya!!!!!

Pengine sio kwamba tunapenda umatonya....bali hatuna jinsi ingine. Hatuko wabunifu...hatuko wavumbuzi....hatuko waigaji wazuri....yaani tupo tupo tu. Sasa tufanyeje ili na sisi tuonje ladha ya maendeleo kama sio kuomba na kupokea misaada isiyotusaidia?

Afadhali hata Wachina maana wao kwa kuiga hawana mpinzani.
 
Hoja hapa ni kwamba kwa nini tunaendelea kukumbatia misaada? Sababu mojawapo ni kwamba hatujajitawala bado..na wanaotutawala hawataki kutuachia tujitawale manake tukijitawala utawala wao utakuwa mashakani! Ni mapambano haya ya kifikra tunayosema hapa kila siku ..hadi tutakapobadilika kifikra kwanza ndipo tutakapoweza kuona 'uovu' uliojificha ndani ya hizo dola milioni 20 za msaada!
 
Nyani,
Siyo kweli kuwa HATUKO WABUNIFU. Ona walivyobuni na kuzitoa za EPA, Meremeta, Mwananchi Gold (wamemuacha Mzee Warioba hoi) nk. Tuna uunifu mkubwa sana wa KULA MTAJI. Ila kuendeleza mtaji hiyo kitu kwa Watanzania IS NOT REACHABLE.
 
Haihitaji mtu kuwa na kipaji cha kipekee kuiba hela za uma. Kwa hiyo mimi siuoni wizi wao kuwa ni ubunifu wa aina yeyote ile.
 
Hoja hapa ni kwamba kwa nini tunaendelea kukumbatia misaada? Sababu mojawapo ni kwamba hatujajitawala bado..na wanaotutawala hawataki kutuachia tujitawale manake tukijitawala utawala wao utakuwa mashakani! Ni mapambano haya ya kifikra tunayosema hapa kila siku ..hadi tutakapobadilika kifikra kwanza ndipo tutakapoweza kuona 'uovu' uliojificha ndani ya hizo dola milioni 20 za msaada!

Unaona sasa....mimi fikra kama hizi ndio nazipiga vita kabisa. Eti wanaotutawala hawataki kutuachia tujitawale....puh-lease....
 
Waafrika matatizo yetu ni makubwa mno kuliko tunavyofikiria.

Mimi mtizamo wangu ni tofauti, hakika simlaumu Hu Jintao hata kidogo. Hata ungelikuwa wewe kwenye nafasi yake..usingefanya tofauti. HU yuko anatafuta masoko ya bidhaa za nchi yake. Kifupi yuko anawatafutia ajira watu wake. Kitu ambacho kiongozi yeyote mwenye upeo wa kuelewa..anafanya.

Ufumbuzi wa matatizo ya nchi zetu za kiafrika utatoka Africa na kwa waafrika wenyewe. Na katika hili, siyo viongozi akina Kikwete wala CCM watakao leta mabadiliko..mabadiliko yatakuja endapo sisi wananchi kwa kauli moja tutasema: Tumechoka kunyanyaswa, tumechoka kuitwa wajinga na kuamua kudai uwajibikaji kwa wale tunaowapa dhamana. MABADILIKO YA KWELI YATAKUJA ENDAPO WANAOIBA PESA ZA KODI ZETU TUTAWARUSHIA MAWE BAADA YA KUWAPOKEA KWA VIGELEGELE, WANAOTUMIA MADARAKA KUJINEEMESHA TUTAWALAZIMISHA WAACHIE NGAZI NA KUWADAI WALICHOTUIBIA.

Hakuna serikali sehemu yoyote duniani ambayo ina watumikia wananchi wake WILLINGLY. Hata huko ughaibuni (Western Europe na US)..wananchi wako makini sana, serikali ikileta longo longo wanaitimua! Ni Africa pekee utakuta kiongozi anashika mateka wananchi na kulaumu wengine (Mugabe), ni Africa pekee..kiongozi anaiba...anapokelewa kwa shangwe na wananchi wake..na anayejaribu kuhoji zaidi anaambiwa..ana wivu au ana visa na muhusika au kabila lake. Its only Africa raisi anashutumiwa kwa wizi..baada ya kupelekwa mahakamani..tunasema hapana..mwache apumzike..... Ni Afrika pekee Serikali ikijenga barabara..wananchi wanaona wametendewa favour! wakati inatimiza wajibu wake....and on and on...

Nasema hivi: Hata leo tumpe kura Chadema, CUF just name them...watafanya madudu yale yale ya CCM. Unless and until sisi WANANCHI tuchukue jukumu na kutambua kwamba nchi yetu ni yetu sote na kama wananchi tuna wajibu wa kuitumikia na kuifaidi..NA VIONGOZI TUNAWAAJIRI SISI KWA KUWACHAGUA, SO WE CAN FIRE THEM IF NEED BE, tutaendelea kukandamizwa milele na akina Kikwete, watoto wao na wajukuu wao. I can guarantee you, CCM ingejua ina deal na wananchi waelewa..isingekuwa inatufanyia madudu inayotufanyia..lakini for now, they know..they can do whatever they want..without consequences. WANANCHI TUMELALA!

CCM kutuletea maendeleo ni ndoto! They arent interested. Ni mpaka wewe mwananchi uliyelala njaa, ambaye mtoto wako ameshindwa kwenda shule kwa kukosa nafasi, ambaye mke wako kashindwa kujifungua salama hospitali kwa kukosa daktari...et al..uanze kuuliza maswali magumu, uanze kutumia haki yako ya kupiga kura kwa uangalifu bila kudanganywa na maslahi ya chakula na mbege....! uanze kujiona kama mdau wa anchi yako... Ni wakati huo..safari ya kuelekea kwenye ukombozi wa kweli wa Mtanzania/mwaafrika itakopoanza. Ukiendelea kusingizia njaa kwamba ndo inakufanya upige kura bila kufikiria..uamuzi ni wako...lakini you can be sure: Utakuwa na hiyo njaa mpaka unaingia kaburini! kupewa kilo mbili za mchele kwa kura yako..ujue kabisa..unawaumiza hata vizazi vijavyo.

For now, lets relax and accept the reality. Tunaweza kulalamika, lakini bila kuamka na kutenda..hatuendi popote. EPA na mengineyo yatazidi kuibuka..na tutazidi kusahau, umasikini utazidi kuongezeka, akina Makamba watazidi kuzaliwa, akina Kikwete watazidi kuwepo, watoto wa kina Kingunge et al watazidi kupeta......matawi ya CCM, yatazidi kuongezeka huko London na Malaysia (kifupi opportunists watazidi ku-proliferate).....and on and on..... And life goes on. At the end of the day vicious of poverty for common mwananchi...

Now whether we can do it, sisi wananchi...tunarudi kwenye hypothesis ya Nyani......
 
Waafrika matatizo yetu ni makubwa mno kuliko tunavyofikiria.
Now whether we can do it, sisi wananchi...tunarudi kwenye hypothesis ya Nyani......

Heheheheeee....mimi bado na-maintain hiyo hypothesis kuwa ni ya kweli.....
 
Nyani,
Siyo kweli kuwa HATUKO WABUNIFU. Ona walivyobuni na kuzitoa za EPA, Meremeta, Mwananchi Gold (wamemuacha Mzee Warioba hoi) nk. Tuna uunifu mkubwa sana wa KULA MTAJI. Ila kuendeleza mtaji hiyo kitu kwa Watanzania IS NOT REACHABLE.

Huo sio ubunifu. Mfano wako ni sawa mtu kufanya mapenzi na mzazi wake. Ukichukua kuwa mzazi ni mtaji na mtoto ni faida.
 
Hoja hapa ni kwamba kwa nini tunaendelea kukumbatia misaada? Sababu mojawapo ni kwamba hatujajitawala bado..na wanaotutawala hawataki kutuachia tujitawale manake tukijitawala utawala wao utakuwa mashakani! Ni mapambano haya ya kifikra tunayosema hapa kila siku ..hadi tutakapobadilika kifikra kwanza ndipo tutakapoweza kuona 'uovu' uliojificha ndani ya hizo dola milioni 20 za msaada!

Kujitawala ni hisia tu. waChina walitawaliwa, tena vibaya sana. Waingereza, wafaransa walikuwa wanawatalawa waChina kama soko la madawa la kulevya. Kwanini wao waliweza kubadilika na sisi bado tunaboronga.
 
Masanja!

Waweja kulumba Njomba!!!!

taabu yako unaongea mno ukweli..wengi hawatapenda kukusikia!
 
Mwanakijiji,
What u missing is the acknowledgement of what work and what doesnt work ! Nilichojaribu kukuelezea ni kwamba misaada ya wachina hata kama ni kidogo but they fuilfill the objectives for what they proposed for, compared to other projects which their money end up in hands of few.

And talking of opportunity cost it doesnt matter for Tanzania because as u said urself knowing usd 170 miliion zimeibiwa itatusaidia nini wakulima kama hazitatufikia kwa lengo la kuboresha kilimo anyway but what matter is To move ahead by doing things that can be done even though the input will be small but something will be gained because something has been done .

Pia Kama itakuwa ni attitude ya Donors kuparticipate kwenye programme zote kama wanavyofanya wachina it will be the best ideas kwasbabu project zitafanyika kama inavyotakiwa.

Mwisho +1 is greater than 1 million negative always remember that
 
Sijui kama unafahamu kuhusu TAZARA na URAFIKI Textiles.. !!

And talking of opportunity cost it doesnt matter for Tanzania because as u said urself knowing usd 170 miliion zimeibiwa itatusaidia nini wakulima kama hazitatufikia kwa lengo la kuboresha kilimo anyway but what matter is To move ahead by doing things that can be done even though the input will be small but something will be gained because something has been done .

so should we try to recover our 40 billion Tsh from Kagoda or should we keep begging for such amount like 21 Billion kutoka kwa Wachina? Maana kwa mtindo wako ni kuwa as long as watu kama wachina wanakuja na misaada kidogo tusiwe na wasiwasi wa sisi kutumia fedha nyingi zaidi kifisadi.

Pia Kama itakuwa ni attitude ya Donors kuparticipate kwenye programme zote kama wanavyofanya wachina it will be the best ideas kwasbabu project zitafanyika kama inavyotakiwa.

Bado unafikiria kuwa donors ndio watatuokoa kwa sababu wana roho nzuri. Hata hizo fedha za Wachina zitaliwa vile vile (labda kwa kiasi kidogo). Si kampuni mojawapo ya Kichina na yenyewe imepigwa marufuku na IMF hivi karibuni sababu ya corruption?

Mwisho +1 is greater than 1 million negative always remember that

But +2x is always greater than +1 in any mathematical graph! as long as that x is not 0 or a negative integer!
 
Kujitawala ni hisia tu. waChina walitawaliwa, tena vibaya sana. Waingereza, wafaransa walikuwa wanawatalawa waChina kama soko la madawa la kulevya. Kwanini wao waliweza kubadilika na sisi bado tunaboronga.

Ewaa, Zakumi hapo tunasema tupo ukurasa mmoja, ndicho ninachomaanisha hapa...ni lini tutapata hizo hisia, ni suala la muda, nayo ni mapambano, ambayo inabidi tuyashinde ili tuweze kuepuka hilo, ila ni kwamba wakati tunapambana tujue na tutie akilini kuwa yule tunayepambana naye naye anapambana kumaintain status quo!
 
Unaona sasa....mimi fikra kama hizi ndio nazipiga vita kabisa. Eti wanaotutawala hawataki kutuachia tujitawale....puh-lease....

eh NN, sihitaji kukuelezea usome kwa kuangalia muktadha na sio sentensi moja...and by the way that is clear enough,,,,,kama unavosema 'miafrika ndivyo tulivyo' tunatakiwa tupambane kuondokana na hali hiyo

Kinyume na hivyo utakuwa bado unafikiria miafrika ndivyo tulivyo kwa sababu ya prescriptions ambazo zimeshakuwa imposed kwenye uelewa wako...unafikiria tu kuwa 'to be is to be like and to be like is to be like....wazungu? ama wachina?

tafakari
 
Back
Top Bottom