We have varieties of resources but we dont have capital to utilize those resources. Poor plans and selfishness in some of our leaders has often been a core sources of our poverty!
Kwani hao viongozi wenye uchu ,mipango na matumizi mabaya ya madaraka wanotokea wapi? Mbinguni,America, China au wapi?SI ndio hao hao jamaa zetu,wanatokea kwenye familia zetu..
Au sisi tunasema kwakuwa hatupo kwenye Kona hyo?
Je!? Ungepewa madaraka ya uongozi ungeenda tofauti na walioongoza hapo awali?
Jibu Ni hapana,maana matatizo ya nchi za bara la Africa yanafanana
Labda kwa nchi za kiarabu zilizopo kaskazini mwa jangwa la Sahara..
Na sababu inayotutofautisha sisi na wao Ni MTINDO WA MAISHA..
Mitindo yetu ya maisha ndio imetufikisha hapa tulipo Leo,
Mitindo yetu ya maisha ndio inayozaa viongozi wabadhirifu wa Mali za Uma, ndio Inayozalisha ujinga ndani yetu,ndio inayozalisha tamaa ya kujilimbikizia Mali kiujanjajanja,mitindo yetu ya maisha ndio Inayotufanya tudharaulike, tuendelee kuwa wajinga na maskini...
Angalia jamii tunazoishi nazo km wahindi na hebu fuatilia mtindo wao wa maisha uje ulinganishe na wa kwetu,tafakari..
Nimewahi kusoma shule mojawapo inamilikiwa na wahindi,hvyo wanafunzi wa kihindi walikuwa wengi kuliko sisi weusi,
Kuna wahindi walikuwa vilaza tu darasani,ila wao wamefaulu maisha kuliko mm niliekuwa na faulu darasani,
Yote kwa sababu ya mfumo waliojitengenezea
Muhindi anaweza akawa babu,baba, mtoto wamezaliwa Tanzania,ila akaongea kihindi au kupika chakula Cha kihindi km yupo Bombay..
Tukitaka kuikomboa Africa, mabadiliko yaanzie kwenye ngazi ya familia kubadili mtindo wa maisha,lakini tusitegemee viongozi waje kuibadilisha Africa
Asanteni: