Young D ni maskini sana kwa sababu hizi

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Msanii Young Dar es salaam mbali na kipaji kikubwa cha muziki alichonacho lakini suala la kutokujielewa ni kizuizi kikubwa cha maendeleo yake.

Wajanja wengi wanatumia mgongo wa young D kupiga pesa huku yeye mwenyewe akibaki kapuku miaka nenda rudi.

Kinachofanyika ni hivi, wajanja wanachofanya wanampigisha pamba kali pamoja na kumgharamikia mambo yote ya starehe lakini nyuma ya pazia pesa wanazotumia kumgharamikia ni zile zile zake kwa kupitia muziki wake na show anazozifanya bila ya yeye mwenyewe kujua.

Imefika pahala siku hizi young D si ajabu akakuomba umuungie hata mia mbili ya sigara jinsi maisha yalivyompiga.

Mbali na Young D wasanii wengi wanapitia kasumba hii ya kunyonywa mfano kundi kama Yamoto band enzi hizo walikuwa wanaingiza pesa chafu kwenye show lakini wao binafsi wanaambulia kupewa laki moja moja na kupigishwa pamba pamoja kugharamikiwa starehe zozote wanazohitaji huku kiasi kikubwa cha pesa kikibaki mfukoni kwa mkubwa fella.

Madogo walikaa kimya mwisho wa siku wakaamua kuhoji maslahi yao lakini Fela alivyomjanja akawaambia pesa zao anawajengea nyumba ,lakini mbaya zaidi nyumba yenyewe ilijengwa moja tu na wote wakatupwa humo kitu ambacho hakikuwa makubaliano yao.

Ifike pahala wasanii waamke bila hivyo wajanja wachache watazidi kuneemeka kwa migongo yao huku wao wenyewe wakibaki kuwa masikini.

Walijaribu kumuingia Diamond Platnumz kwa ujanja huo lakini ndio hivyo Diamond mjanja sana haibiwi kirahisi rahisi bila hivyo na yeye angekuwa ameshapotea zamani sana.
 
Ngoja nicheke tu[emoji2] [emoji2][emoji13]
 
Wanapewa mishahara %fulani wale jama hawana uwezo wakumuibia diamond
UNASEMA DIAMOND NINI HUONI TALE MENDEZ MKUBWA WALIVYOMNG'ANG'ANIA... LAZMA APIGWE TU NA YEYE IKIFIKE KUPEPESUKA HAO AKINA TALE HUTAWAONA TENA ULIZA TIPTOP IMEKUFIA WAPI
 
Kwanini mtu unakua huna business plan nzuri?
Sababu za wasanii kudhulumiwa pesa zao ni mameneja wao sasa kwanini isitumike namna ya kuwa handle manager kwamba kile kinachoingia kiwe wazi? Nadhani transparent ni ishu kati ya meneja na msanii. Vitu kama idadi ya tiketi na mapato vinapaswa view open kwa msanii na manager.
Kwa maana hiyo ni bora mtu kujisimamia mwenyewe au na familia yako kwa watu mnaoaminia. Huko marekani na ulaya wao mbona wanatoboa kupitia mameneja wao?
Bongo tunapaswa kuondoa hili tatizo mapema.
 

Nimekuingiza studio, nimekulipia kurekodi, nimekulipia promo, nakutafutia shows, nakulipia bills zako kipindi ambapo nimekutoa chini kabisa ukiwa huna hili wala lile unaanzaje kuacha kuniskiliza nnachokwambia na kunipinga...?.

Unataka kupotea kwenye ramani ili urudi kama zamani wakati pesa unaitamani ila sanaa haina thamani lakini bado unaitamani.

Lazma upigwe tu mpaka unapokuja kushtuka. It's too late.
 
Mfumo mbovu sana huo wa msanii.
Mtu sharti ujue kiwanja Fulani umejaza watu kadhaa, VIP na kawaida pesa inagawanywa kiutaratibu.
Maskini ndio maana daily wanalia njaa bado sijajua bongo movie hali ikoje.
 
Mfumo mbovu sana huo wa msanii.
Mtu sharti ujue kiwanja Fulani umejaza watu kadhaa, VIP na kawaida pesa inagawanywa kiutaratibu.
Maskini ndio maana daily wanalia njaa bado sijajua bongo movie hali ikoje.

Bongo movie sjawahi kuona kama Bongo kuna movie.

Walewale tu mkuu.
 

barua hii imfikie mwakyembe
 
nimesoma huu uzi nikaishia kucheka hiiiiiiiiiiiiiiii
 
Bongo movie sjawahi kuona kama Bongo kuna movie.

Walewale tu mkuu.
Sidhani kama kuna jipya Zaidi ya kuigiza mapenzi concept ile ile.
Mimi najiuliza kwani hao wasanii wasitafute riwaya au vitabu vya matukio mbalimbali watengenezee muve kama ulaya na amerika wanavyofanya?
Kuna watu wana mikasa mikubwa sana maishani wanaweza kuwatafuta wakatengeneza bongee la picha.
Atleas naona waandika stori lakini hamna mafunzo kwani nyingi ni mapenzi na mambo ya giza.
Why wasiandike kitu constructive kuhusu maisha out of mapenzi na uchawi?
Nahis wana akili ndogo sana.
Picha zinazogharimu pesa nyingi ni za action lakini hizi nyingine tukiwauliza hawawezi jitetea.
 

Kwa sababu hata wanaoangalia hizo maigizo akili zao ni ndogo na ndio mana hata watengenezaji akili zao zinakuwa ni ndogo zaidi.

Wabongo wanapenda ujinga ujinga tu na mambo ya kipuuzi ndio mana wanadumisha ujinga na upuuzi wao kila kukicha mkuu.

Kwa hiyo wataendelea kupata mapato duni kila siku kutokana na ubora na kiwango duni cha kazi zao ambazo hata nchi jirani nyingi hazitambuliki.
 
Bongo movie niliachana nayo 2013 hamna jipya mkuu Zaidi ya drama zile zile.
Watu wanataka new idea na mafunzo pia.
Wenzetu wamejikita kutoa thamthiliya zinazoelimisha jamii.
 
Bongo movie niliachana nayo 2013 hamna jipya mkuu Zaidi ya drama zile zile.
Watu wanataka new idea na mafunzo pia.
Wenzetu wamejikita kutoa thamthiliya zinazoelimisha jamii.


Real Talk mkuu.
 
Du hayo mambo bado yapo? Nilijua yaliishia kwenye enzi za gangwe mobb
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…