Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 20,137
- 26,189
Msanii Young Dar es salaam mbali na kipaji kikubwa cha muziki alichonacho lakini suala la kutokujielewa ni kizuizi kikubwa cha maendeleo yake.
Wajanja wengi wanatumia mgongo wa young D kupiga pesa huku yeye mwenyewe akibaki kapuku miaka nenda rudi.
Kinachofanyika ni hivi, wajanja wanachofanya wanampigisha pamba kali pamoja na kumgharamikia mambo yote ya starehe lakini nyuma ya pazia pesa wanazotumia kumgharamikia ni zile zile zake kwa kupitia muziki wake na show anazozifanya bila ya yeye mwenyewe kujua.
Imefika pahala siku hizi young D si ajabu akakuomba umuungie hata mia mbili ya sigara jinsi maisha yalivyompiga.
Mbali na Young D wasanii wengi wanapitia kasumba hii ya kunyonywa mfano kundi kama Yamoto band enzi hizo walikuwa wanaingiza pesa chafu kwenye show lakini wao binafsi wanaambulia kupewa laki moja moja na kupigishwa pamba pamoja kugharamikiwa starehe zozote wanazohitaji huku kiasi kikubwa cha pesa kikibaki mfukoni kwa mkubwa fella.
Madogo walikaa kimya mwisho wa siku wakaamua kuhoji maslahi yao lakini Fela alivyomjanja akawaambia pesa zao anawajengea nyumba ,lakini mbaya zaidi nyumba yenyewe ilijengwa moja tu na wote wakatupwa humo kitu ambacho hakikuwa makubaliano yao.
Ifike pahala wasanii waamke bila hivyo wajanja wachache watazidi kuneemeka kwa migongo yao huku wao wenyewe wakibaki kuwa masikini.
Walijaribu kumuingia Diamond Platnumz kwa ujanja huo lakini ndio hivyo Diamond mjanja sana haibiwi kirahisi rahisi bila hivyo na yeye angekuwa ameshapotea zamani sana.