Young entrepreneurs in tz

Mimi namfahamu kijana mmoja yeye ni mfanyabiashara mkubwa sana na kutoka kuajiriwa kama muuza duka la vifaa vya ujenzi hadi kuwa boss anayemiliki biashara kubwa za maduka ya ujenzi na nyumba za maana za biashara(ghorofa).Hata hivyo hab ari za watu wake wa karibu zinasema alitoa kafara kama sharti la kupata utajiri!swali;je huyu ana vigezo vya kuwepo kwenye project yenu?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 

Ingawa siamini sana katika ushirikina ila naskia upo,,labda wengine washauri pia
 
Nitumie details za hiyo event maana kwa maelezo yako tuna qualify lol 🙂

Check details
 

Sidhani kama atakuelewa, huyu naona anatafuta watu "wenye pesa" na si wajasiriamali wabunifu waliofanikiwa. Tuachane na mawazo hasi ya kuangalia tu kwamba anamiliki biashara ya bilioni ngapi wakati bado ni mchuuzi tu, Tanzania inahitaji vichwa vyenye kujikita kwenye uzalishaji zaidi, lakini ujanja ujanja na sanaa vilishazoeleka kuanzia kwa waandaaji wa seminar za ujasiriamali wanaandika project na kupiga pesa kisha wanaandaa seminar na kufundisha vitu vya nadharia sana wakati wao hakuna walichokifanya! Hapa bongo kila mtu anaangalia fursa ya kupiga pesa, hata huyu mama ukimuuliza incentive nyuma ya hiyo project na nani anafund utaskia stori nyiiingi! Vijana wapo wenye mawazo original wamejichimbia kwenye uzalishaji wako bize, nadhani utawapata mapapaa wanaopenda show off; nadhani anza na Shigongo, nenda ya yule mhaya ya Clouds, hao watawaita wenzao kibao wanafahamiana.
 
nadhani anza na Shigongo, nenda ya yule mhaya ya Clouds, hao watawaita wenzao kibao wanafahamiana.
CYBERTEQ comment yako ni nzuri isipokuwa name calling kama hii sio afya.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu umeongea ukweli tupu, Watanzania waache show wajikite kwenye uzalishaji, haya mambo ya sijui events hayatawatoa kamwe, ni kweli huwa siku zote nawaona hao wakina Shigongo na jamaa wa Clauds kwamba ndo Wajasiriamali walio fanikiwa, Bongo ni nchi ya wapenda sifa sana.
 
Jaribuni kutafuta kweli talented entreprenuer, kuna wakati niliona eti January Makamba kaalikwa akawahutubie wajasiriamali kwa kweli nilichoka.
 
Ingawa siamini sana katika ushirikina ila naskia upo,,labda wengine washauri pia

Achaneni na maneno ya vijiweni, ushirikina upo sawa lakini watu wanapiga kazi; huyo anayemsema kibaravumba huenda ni Mkinga, maana hao ndiyo walivyo, they are very serious with work na wanafanya kwa passion na determination, mwisho wa siku wakifanikiwa watu wanaanza kusema mchawi huyo!!...I have a friend of mine ambaye alipitia kulima kwa jembe la mkono (kibarua), kufyatua tofali, kuuza karanga, kuuza barafu, kuosha vyombo kwenye mgahawa, and now he is big, ana mafanikio makubwa mno!
 
Last edited by a moderator:
CYBERTEQ comment yako ni nzuri isipokuwa name calling kama hii sio afya.

Mkuu kwani ni siri, sijamsema kwa baya lolote, ni kweli jamaa wamefanikiwa lakini hawawezi kuwa mfano kwa mtu yeyote! We need professionals Mkuu, wenye kujua nini wanafanya, ambaye akipanda jukwaani watu nyoyo zinawagusa, si wajanja wajanja wa kutumia "fursa" then unawakusanya kwa sababu unawajua ni maarufu watakusanya watu, lakini mwisho wa siku what do we achieve?!!!
 

Sifa na shortcuts tu Mkuu, mafanikio kidogo display kibao!
 
I get you! Concern yangu ni kuwa anaweza take it personal!
What you said is really true!
 
naomba uniweke na mimi kwani nami ni mjasiriamali kijana je nitapata nafasi hiyo

 
Vip wafanyabiashara wa sembe vijana wanaruhusiwa ambao wamepata mafanikio makubwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…