Youssoph Dabo Atangazwa Rasmi Kocha Mpya Azam FC

Youssoph Dabo Atangazwa Rasmi Kocha Mpya Azam FC

Kicha ameshindwa kabisa mapema. Kipa mbovu hana uzoefu unamuacha mpaka anawagharimu.
 
Nilikwambia mkuu.

Azam Wana mapungufu kwenye KOCHA na Manager

JEMEDARI ALIWANYOOSHA MNO
Hebu nieleweshe kwenye hoja ya udini ya Azam.
Wakati Azam FC unachukua ubingwa jemedari said ambae ni muislam ndio alikuwa manager.
Je hapo kulikuwa hakuna udini?
Na CEO wa timu alikuwa muislam pia
 
Nimepata fununu kuwa Azam sasa hivi wanamtaka Mgunda, kwa hiyo Dabo atayarishe passport yake iwapo Mgunda atawakubalia.
 
Taarifa rasmi toka Chamazi zinathibitisha Azam kushusha kocha mpya kutoka Senegal. Yossouph Dabo ni kocha kijana mwenye mafanikio makubwa ambayo yameipaisha Senegal kwenye ulimwengu wa soka . Kocha huyo amepewa kandarasi ya miaka mitatu.

FvDA5hcWcAEzw42

WASIFU WAKE.
Dabo amezaliwa kwenye mji wa Saggata,Senegal miaka 43 iliyopita.
Amecheza soka nchini mwake, kisha Tunisia na Ufaransa.

Yafuatayo ni baadhi ya mafanikio yake kama kocha. Mwaka 2016, akiwa na Tengueth alishinda ubingwa wa Kombe la Ligi.

Mwaka 2017 akiwa kocha wa Tengueth alifika fainali ya Kombe la Senegal (sawa na Kombe la Shirikisho la Azam hapa nchini)

Desemba, 2018 alitwaa ubingwa wa vijana chini ya miaka 20 kwa timu za taifa ukanda B wa Afrika Magharibi (Wafu B), mashindano yalipofanyika Togo.

Februari 2019 alichaguliwa kuwa kocha bora wa Afcon chini ya miaka 20 huko Niger alipoisaidia Senegal kufika fainali. Juni 2019 aliiongoza Senegal kufika robo fainali ya Kombe la Dunia chini ya miaka 20 nchini Poland.

Julai 2019 alikuwa sehemu ya benchi la ufundi la timu ya taifa ya Senegal iliyofika fainali ya Afcon kule Misri. Agosti 2019 akiwa kocha wa timu ya taifa ya Senegal chini ya miaka 23, aliiongoza kushika nafasi ya tatu na kushinda medali ya shaba kwenye michezo ya Afrika jijini Rabat, Morocco.

Desemba 2019 aliiongoza Senegal kushinda ubingwa wa kanda ya Wafu mashindano yaliyofanyika Guinea. Machi 2020 aliiongoza Senegal kushinda ubingwa vijana chini ya miaka 20 wa mashindano ya mataifa ya Kiarabu. Senegal ilishiriki kama wageni waalikwa mashindano yaliyofanyika Saudi Arabia.

Novemba 2020 akiwa kocha wa timu ya taifa ya Senegal chini ya miaka 20 walifika fainali kuwania ubingwa wa kanda A ya Afrika Magharibi. Msimu wa 2020/21 alishinda ubingwa wa ligi ya Senegal akiwa na Tengueth.
Huyu ana undugu na marehem Amin Dabo?

Kama katoka ukoo huo basi mtegemee kipaji hapo. Azam wamelamba dume.

Nawafahamu watu wa ukoo wa Dabo, wengi tu, niliishi nao majuu huko. Ni koo yenye vipaji sana.

Mmoja wao yupo Unguja anaitwa Adel Dabo:

1691664930056.png
 
Back
Top Bottom