YouTube inalipa ila sio hapa Bongo

YouTube inalipa ila sio hapa Bongo

De Opera

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2013
Posts
780
Reaction score
1,664
Wakuu mambo vipi?

Ni muda mwingine tumekutana tukiwa salama kabisa, ila poleni sana kwa wale mnaopitia changamoto kinamna yoyote ile na ninawaombea muweze kurudi katika utimamu.

Wakuu, uzi huu leo naupitisha katika sindano ya YouTube.

Mimi nimekuwa YouTube Creator it's about 10yrs now, and I know YouTube as well. Nimeshachukua pesa za Youtube mara nyingi sana, that time nilikuwa nachukua pesa kupitia 'Western Union' kabla YouTube hawajaitoa na kubakisha 'Wire transfer'.

Siku hizi vijana wengi wameajiriwa na YouTube. You make money depends on what you're doing.

Kwa hapa Bongo neno linaloshika sana na linalomshawishi mtu naye aweze kuwa YouTube Creator, ni "Youtube inalipa".

Binafsi mimi huwa sipendi kulitumia neno hili kwa sababu najua challenges zilizo kwenye YouTube.

Kibongo bongo hapa ukisikia mtu anakuambia anapiga hela YouTube hapo usikubali moja kwa moja.
Kuna watu wanaficha aibu. Unakuta miezi 6 ndio anapata $100, halafu anasema eti anapiga hela. Seriously, hii haisound poa.

Kiukweli, ili upige hela za YouTube lazima utengeneze unique contents halafu ziwe kwenye moja ya lugha zilizotajwa kwenye Adsense na sio kiswahili. Kingine ukitaka YouTube chaneli yako iwe na matangazo yenye CPC (Cost per click) kubwa, lazima contents zako ziwe zinazungumzia mambo ya pesa.

Mfano: Buy, Sell, Credit, Money, nakadhalika. Hizi zinakuwa na CPC kubwa kuanzia $10 kuendelea. Hapo utakuta unapiga $20 kwa siku. Lakini kama contents zako ni za kiswahili, sahau hilo, kwa sababu 'Kiswahili' ni miongoni mwa lugha ambazo hazijatajwa kutumika kwenye Adsense.

Mara nyingi kwa wastani chaneli yenye contents za kiswahili 'cpc' yake huchezea kwenye $0.01 au $0. Ikipanda sana ni $0.03 inategemea upepo wa contents za siku hiyo.

Mfano, una video moja kwenye chaneli yako imepata Views 30,000 watu 100 wakabonyeza matangazo, hapo utakuwa umeingiza $1 au $1.5.
Youtube hawalipi kwa views, wanalipa kwa watu waliobonyeza matangazo na sio kila video inaweza kuwekewa matangazo. Unaweza ukaona video ya mtu ina Views Milioni 3 lakini asiwe amefaidika chochote.

Lakini tukihamia upande wa pili wa lugha na aina ya contents kama nilivowaeleza hapo juu, hapa unaweza piga pesa ndefu kwa sababu cpc kwa wastani inachezea kwenye $2 per click.

Mfano una video ina views 30,000 na watu waliobonyeza matangazo ni 100, chukua hiyo $2 zidisha kwa hao watu 100, ambapo ni sawa na $200. Hii ni pesa ndefu! Kama ukiwa na unique contents za kutosha kwenye chaneli yako, hapo maisha ni mtelezo tu.

Narudia teena 'Youtube inalipa hila sio hapa Bongo'. Na ukikuta mtu anakuambia anapiga hela Youtube na yupo hapa bongo na contents zake ni za kiswahili tena ni za kusimulia, mwambie akuoneshe Adsense ama YouTube Dashboard asikudanganye kirahisi. Bora hata za muziki zinalipa kidogo.

Na hii ni kwa hata wale ambao Tovuti au Blog zao ziko monetized na Adsense. Wembe ni ule ule! Tena kule kwenye site, ukiwa unapost kwa kiswahili, unaondolewa kabisa matangazo.

Ahsanteni wakuu; Kama utapendezwa na elimu zaidi, napatikana kupitia deoperacc kwenye mitandao ya kijamii. Huwa si mpenzi wa kupost sana kule ila unaweza uka -DM tu.
 
Nimekuelewa braza...

Hakuna kitu rahisi hapa duniani hasa kwenye kutafuta pesa....

Ndiyo maana ukiona mtu anakwambia njoo huku mtandaoni kuna pesa za kudaunilodi tu (mf. Forex) shtuka sana.

Nitakuja kukuuliza kitu kuhusu blogging....
 
Jana nilikuwa napita pita huko mtandaoni. Nikashangaa kusoma kuwa shakira, anachukua kama dola milionin4 YouTube kila mwezi. Na kwa ngoma yake hii kiasi hicho kitaongezeka kwa muda fulani. Nikasema hiii
 
Nimekuelewa braza...

Hakuna kitu rahisi hapa duniani hasa kwenye kutafuta pesa....

Ndiyo maana ukiona mtu anakwambia njoo huku mtandaoni kuna pesa za kudaunilodi tu (mf. Forex) shtuka sana.

Nitakuja kukuuliza kitu kuhusu blogging.

Pesa mtandaoni ipo mkuu lakini watu wengi wanaopiga pesa ya ukweli hawajitangazi. Wanaojitangaza ni wale ambao wanaziotea mara moja halafu wanaendelea kula njaa. Ila pesa mtandaoni ipo sana na si ya kudownload ni ya kufanyia kazi.

Shida ni kwamba watu wamekalili kwamba pesa sijui mtandaoni ni blogging, forex, youtube. Kuna vitu vingi sana vya kufanya. Kenyans and nigerians wako vzuri kwa hili hadi wananipa hasira.
 
Wakuu mambo vipi? Ni muda mwingine tumekutana tukiwa salama kabisa, ila poleni sana kwa wale mnaopitia changamoto kinamna yoyote ile na ninawaombea muweze kurudi katika utimamu...
Sasa Mkuu kati ya You Tube na Blog which is best kwa hapa Bongo? Hapo umeeleza upande wa You Tube, vipi kuhusu Blog, ni vitu gani mtu anapaswa kuvizingatia ili apige Pesa kupitia Blog?
 
Unaweza jazia malezo kidogo hapa.
-
Kwenye Muziki unaweza kupiga hela kwa sababu, YouTube huwa wameweka kipaumbele kwa wasanii. Kuna robots huwa zinadetect mapigo, yaani sounds kuanzia db(decibels) kadhaa. Hiyo itajulikana kama huo ni wimbo.

Kiufupi YouTube hawatoi kipaumbele kwa contents za kuzungumza kama Voice over, coz unaweza ukawa unamzungumzia mtu vibaya.

Na kama ni wimbo, baasi vocal na beat inabidi zisipishane sana db.
 
Hizo njia zingine ni zipi kama hutojali mkuu? Hao Nigerians na Kenyans wanafanyeje?
Kuna blogging, kuna Ai data collection, kuna interpretation - hii unaweza chagua kufanya consecutive ndiyo rahisi kidogo.

Kuna voice over, mkuu almost kila kitu unachoweza kufanya remotely kina soko.

Wanaijeria na wakenya wanapga pesa na wahindi.

Hapa kati kuna ukusanyaji data za languages mbalimbali dunia nzima ikiwemo hizo local kama.lichaga kihehe kigogo, wahindi na wakenya wanapatana na hayo makampuni halafu wanakuja watafta watu mtandaoni wanalipa nusu ya ela waliopatana.

Juzi juzi tu kuna kademu ka kikenya kameondoka na zaidi ya dollar $80000 kwa lugha za tanzania kakaishia kukipa si zaidia ya dollar 50,000 nyingine faida kwake.
 
Kuna blogging, kuna Ai data collection, kuna interpretation - hii unaweza chagua kufanya consecutive ndiyo rahisi kidogo.
Kuna voice over, mkuu almost kila kitu unachoweza kufanya remotely kina soko....
Sema sisi huku kila kitu huwa tunachukulia poa.
 
Back
Top Bottom