YouTube inalipa ila sio hapa Bongo

Jana nilikuwa napita pita huko mtandaoni. Nikashangaa kusoma kuwa shakira, anachukua kama dola milionin4 YouTube kila mwezi. Na kwa ngoma yake hii kiasi hicho kitaongezeka kwa muda fulani. Nikasema hiii
Mimi siyo YouTuber ila ninachojua, kinachoweza kukulipa zaidi YouTube ni mchanganyiko wa vitu vitatu vikubwa:
- Audience yako ( Watazamaji wako wengi wanatokea nchi gani?
Nchi za Ulaya na US hata ukipata views chache utapata PESA kubwa.

Kibongobongo ili pesa iwe angalau lazima uwe na views za kutosha, kiti ambacho ni ngumu.

- Maudhui ya video zako. Hii inatokana na matangazo yatakayokuwa yanapita kwenye video zako, maana lazima Ads ziendane na Maudhui ya video. Kwa kawaida makampuni ya Finance, bima, crypto, travel huwa yanalipa pesa kubwa.

- Wingi wa views.

Binafsi, changamoto ninayoiona ni kupata views.
 
Yah views ni changamoto ndio maana wanamuziki wenye majina wanapata. Waliobaki wanabaki tengeneza title za ajabu na kuwahoji wasichana wanaojidhalilisha ili nao wapate views.
Sema hata blogging kuna inaowalipa kiasi sema kwa content za kiujanja ujanja. Mmojawapo ni yule jamaa anayesema alianza sijui blogging na shilingi ngapi. Yule kweli hizo $400 anapata ila kwa content za kiujanja ujanja zile za form 4 results unaenda hakuna matokeo hajatoka.
 
Kwa hapa Tanzania hata mabando ya simu ni ghali mno. Mpaka mtu afungue video ya YouTube basi lazima iwe ni content anayoipenda
 
Asante sana kwa elimu mkuu.

Sent from my 2201116TG using JamiiForums mobile app
 
Kuna la kujifunza hapa[emoji1755]
 
Wanamziki wanapataje pesa kupitia YouTube, nijuze tafadhali
Kaka, kuna njia nyingi za kupiga pesa kwenye YouTube, ila tu kinachotakiwa kwanza ujibrand watu wakufahamu wewe ni nani hata kwa asilimia 40.

Unaweza ukafungua YouTube channel ukaweka wimbo wako na ukaufanyia promotion kupitia Google Ads. Baadaye watu wataanza kukufuatilia wewe ni nani na unafanya nini. Chamsingi ni kutengeneza muziki mzuri hasa katika nyimbo zinazoweza kukupandisha zaidi ni nyimbo zenye 'mguso' nyimbo za hisia na nyimbo za club pia.

Ukishapata Subs 1000 na Watchtime ya masaa 4000 kiujumla ndani ya siku 365, unatuma maombi YouTube ili uweze kupewa matangazo, na kama muziki wako hauna copyright na haukiuki baasi hapo utapewa na utaanza kuingiza kipato. Kuna ugumu mara ya kwanza unavyoanza.
 
Acha kuwakatisha watu tamaa

Hakuna mtandao Kama YouTube katika malipo

Ukiwa na 400hrs
Na subscribe 1k unaanza kuchukua $200 at the first time

YouTube wanalipa vizuri Sana Tena sana
Kaka, hii mbona rahisi!? Inapatikana wapi kaka? 😀
 
Hapa kati kuna ukusanyaji data za languages mbalimbali dunia nzima ikiwemo hizo local
Nafaka inaonyesha una upeo mpana kuhusu kazi za kimtandao...hongera!

Ili kuwasaidia vijana wenzio hebu fungua darasa fupi ili wapate mwanga( basic) jinsi kufanya na taratibu zake.
Mf. ukusanyaji wa hizo data za lugha na utaratibu wake.

Ukifanya hivyo utakuwa umetoa mchango mkubwa sana kwa hiki kizazi na kuliweka jina lako kwenye kumbukumbu ya wengi.
 
Mimi Nina blogs 2 mpaka Sasa ila nataabika sana.

Kuna wakati nilikuwa natumia "click baiting techniques"

Natengeneza picha ya ngono halafu naweka "play button" katikati, mtu akibofya tu anaingia kwenye blog. Na nilikuwa natarget watu wa nje.

Ndio nikapata Kama Laki 8 kwa miezi 3. Ila baadaye Facebook ikaanza kuwa very aggressive ukishare picha Kama hizo, unakula block na spamming warning. Ikashindikana.
 
Watz , wanaamini katika kubaniana fursa Mimi nachofahamu hii Kazi ya YouTube inalipa Sana na nimepata pesa nzuri so waacheni vijana wajiajiri
Naam, ila mimi sijaonesha kuwabania kaka. Nadhani hujaielewa vizuri post yangu.
 
Naona facebook siku hizi wanablock sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…