#COVID19 YouTube yafuta Video Milioni 1 zinazopotosha kuhusu COVID-19

#COVID19 YouTube yafuta Video Milioni 1 zinazopotosha kuhusu COVID-19

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mtandao wa Youtube Jumatano umesema umeondoa kwenye mtandao wake zaidi ya video millioni moja za habari hatari za kupotosha kuhusu virusi vya corona, tangu kutokea kwa hilo mwaka iliyopita.

Taarifa ya mtandao huo unaomilikiwa na kampuni ya Google, inajiri wakati mitandao ya kijamii ikishutumiwa vikali na viongozi wa kisiasa kutokana na kushindwa kudhibiti usambazaji wa habari potofu kuhusu virusi vya corona pamoja na mada nyingine.

Youtube imesema katika taarifa kwenye blogi yake kwamba inategemea maelezo ya wataalamu wa afya, ikiwemo kituo cha kudhibiti magonjwa hapa Marekani (CDC) na shirika la afya duniani (WHO), lakini imekuta wakati mwingine kwamba, si rahisi kutambua habari potofu, wakati ukweli mpya unaibuka.

“Sera zetu zinaangazia kuondoa video za aina yoyote ambazo zinaweza kusababisha madhara mabaya kwa ulimwengu,” afisa mkuu anaehusika na bidhaa, Neal Mohan ameandika.

Chanzo: VOA Swahili
 
Huyu bahati nzuri alifutika yeye badala ya video yake!🤡🤡🤡
 
Gwajima video zake bado zipo, wamemshindwa jasusi la mawinguni !
 
Wameona hazina madhara maana kwanza kanisa lake ni la ufufuo wa mazombie
 
Je hiyo ndio demokrasia wanayotuhubiria huku ilihali wao wenyewe hawataki mawazo mbadala
 
Wameathiri channel yangu hawa Views zimepungua kisa COVID
 
Back
Top Bottom