Hata mimi nimeziponda sana safari za KQ kutoka JKIA Jomo Kenyatta International Airport kwenda Tanzania ukiwa unaunganisha safari ya kimataifa sema toka Charles de Gaulle Paris - Nairobi Kenya - kuelekea viwanja vitatu vya kimataifa vya Tanzania vya AAKIA ZnZ, JNIA DSM, KIA Kilimanjaro, huduma zao hazifai kabisa KQ kukuunganisha toka Nairobi. Watakuweka masaa kibao JKIA Nairobi bila sababu, nadhani ni vita vya kiuchumi ya makusudi kudhoofisha sekta ya utalli Tanzania.
Hawajifunzi kwa Ethiopian Airlines via Bole International airport Addis Ababa kuunganisha kuelekea viwanja vitatu tajwa vya kimataifa vikubwa vilivyopo Tanzania vinavyopokea flights nyingi za kimataifa, huduma za Ethiopian ni za kuigwa maana masaa ya kusubiri yakizidi utapelekwa hoteli Addis kwa gharama za ET Ethiopian airlines ukasubirie flight nyingine.