Yoweri Museveni anatia aibu EAC

Yoweri Museveni anatia aibu EAC

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Kitendo cha Rais wa Uganda kulazimisha kutawala milele kwa gharama yoyote , kinafedhehesha sana Jumuiya ya Africa Mashariki na kudhalilisha mno wananchi wa Uganda .

Ikumbukwe kwamba jambo hili la aibu linafanyika baada ya njama za Museveni za kumrithisha urais wa nchi mtoto wake wa kiume kugonga mwamba , jambo hili baya litasababisha machafuko nchini Uganda na kusababisha mzigo wa Wakimbizi kwa nchi za jumuiya .

Ni wakati sasa kwa jumuia za kimataifa kuingilia kati ili kuepusha mauaji ya kimbari .
 
Afrika inakera sana,uroho wa madaraka inaitesa Afrika kwakweli
Kitendo anachofanya Museveni ni dharau kubwa sana kwa wananchi wa Uganda , ni dharau kwa dunia nzima na ni kufuru kubwa sana kwa Mwenyezi Mungu .
 
Subirini tu Muda si mrefu watawa milele ninyi. Ni suala la muda tu.
 
Africa na hasa EAC ni mbaya, mbovu na hakuna wa kumnyooshea mwenziye mkono. Angalia eti mpatanishi wa waRundi ni Mkapa!!! Huyu Mkapa asiyeamini ktk democracy nyumbani kwake awe mpatanishi wa waRundi!!??

Mseveni, Kagame, Nkurunzinza, Maghufuli na Uhuru nani wa kumyooshea mwenzie mikono?! WOTE WANAKERA KWELI
 
Tangu nimeona wabunge wa upinzani wakibebwa kama jeneza kutolewa bungeni na kutupiwa kama mizigo ktk gari na askari maalumu toka ikulu, sina hamu na Museveni.
 
Hivi hawa watawala wanaotaka kufia madarakani hawaonagi aibu.. Yani ni wewe tu ndio unafaa kuwa rais?
 
Wao hawana makosa kuna walio nyuma yao ambao kamwe hawaitakii mema Africa, sio rahisi kuliona hili kwa mtu mwny upeo wa kawaida, inahitaji jicho la tatu!
 
Back
Top Bottom