Kitendo cha Rais wa Uganda kulazimisha kutawala milele kwa gharama yoyote , kinafedhehesha sana Jumuiya ya Africa Mashariki na kudhalilisha mno wananchi wa Uganda .
Ikumbukwe kwamba jambo hili la aibu linafanyika baada ya njama za Museveni za kumrithisha urais wa nchi mtoto wake wa kiume kugonga mwamba , jambo hili baya litasababisha machafuko nchini Uganda na kusababisha mzigo wa Wakimbizi kwa nchi za jumuiya .
Ni wakati sasa kwa jumuia za kimataifa kuingilia kati ili kuepusha mauaji ya kimbari .