Fisherscom
JF-Expert Member
- Mar 13, 2008
- 1,763
- 766
Genekai wanitega, mataani waniacha,
Heri ningekuwa mboga, jokofuni singechacha,
Sasa najaa woga, wa fani hii kukacha
Vipi nitakutungia, nawe humo tenzini?
Shairi lake mdau, linayo tele manjonjo,
Pamoja nazo nahau, zavikoleza vionjo,
Hata pasipo limau, hutasahau muojo,
Vipi nitakutungia, nawe humo tenzini?
Kwa kuwa umenirai, nami sifanyi hiyana,
ili usijekinai, japo ni-bado kuchina,
lete hata mayai, tele tupate jichana,
Vipi nitakutungia, nawe humo tenzini?
Najua bado wataka, vingi vina shairini,
Hata vigeuzwe taka, pia vichorwe katuni,
Daima utavitaka, tele vimo moyoni
Vipi nitakutungia, nawe humo tenzini?
Kumbe mkali wa vina namna hiyo bibie? Hongera zako.