Yu wapi Cheusimangala?

Yu wapi Cheusimangala?

Genekai wanitega, mataani waniacha,
Heri ningekuwa mboga, jokofuni singechacha,
Sasa najaa woga, wa fani hii kukacha
Vipi nitakutungia, nawe humo tenzini?

Shairi lake mdau, linayo tele manjonjo,
Pamoja nazo nahau, zavikoleza vionjo,
Hata pasipo limau, hutasahau muojo,
Vipi nitakutungia, nawe humo tenzini?

Kwa kuwa umenirai, nami sifanyi hiyana,
ili usijekinai, japo ni-bado kuchina,
lete hata mayai, tele tupate jichana,
Vipi nitakutungia, nawe humo tenzini?

Najua bado wataka, vingi vina shairini,
Hata vigeuzwe taka, pia vichorwe katuni,
Daima utavitaka, tele vimo moyoni
Vipi nitakutungia, nawe humo tenzini?

Kumbe mkali wa vina namna hiyo bibie? Hongera zako.
 
I am speechless,

Kashaijabutege (umeshamkamata baba?) na Judith nyie ni wakali.. Siku moja mtukumbuke na sisi wababu!

Ila tuache utane, Cheusi ameadimika sana kama Kakakuona!

Mkimwona Cheusi mwambie akaripoti kwa Babu DC haraka sana ili amfikishie mzigo Kashaijabutege!
 
:A S-heart-2:Ninamsaka Cheusi, Cheusi wangu Mangala,
Mtoto kama mdosi, asopenda masihala,
Naona kama kaasi, sioni zake makala,
Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.

:A S-heart-2:First Ladi nahisi, umemficha mahala,
Ninazo pia tetesi, kwa Preta analala,
Rose mtingisha nyusi, yu wapi wangu Mangala?
Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.

:A S-heart-2:Kila mlo ukakasi, sipati hamu ya kula,
Cheusi njoo upesi, niepe huu msala,
MadamT mkwasi, ni yupi kwangu mbadala?
Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.

:A S-heart-2:Nakuuliza Demsi, ijibu hii makala,
Ninagona kama fisi, usiku nianapolala,
Chapachapa mikamasi, nalowesha matambala,
Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.

:A S-heart-2:Mangala wangu Cheusi, nijuze pako pahala,
Nachekwa kandamnasi, mapenzi yanifanya ****,
Nitajitwanga risasi, nipumzike kwa Mola,
Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.

:A S-heart-2:Kaditama yangu pasi, kwako Cheusimangala,
Una utamu wa tasi, laini kama salala,
Sukari kama fenesi, sehemu gani walala?
Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.

teh teh we imba mashairi tu,wakati wenzio tunakula vitu vitamu nachuro hapa live.cheusi ninaye mimi hapa ilala msijisumbue kumtafuta:kev:
 
Genekai wanitega, mataani waniacha,
Heri ningekuwa mboga, jokofuni singechacha,
Sasa najaa woga, wa fani hii kukacha
Vipi nitakutungia, nawe humo tenzini?

Shairi lake mdau, linayo tele manjonjo,
Pamoja nazo nahau, zavikoleza vionjo,
Hata pasipo limau, hutasahau muojo,
Vipi nitakutungia, nawe humo tenzini?

Kwa kuwa umenirai, nami sifanyi hiyana,
ili usijekinai, japo ni-bado kuchina,
lete hata mayai, tele tupate jichana,
Vipi nitakutungia, nawe humo tenzini?

Najua bado wataka, vingi vina shairini,
Hata vigeuzwe taka, pia vichorwe katuni,
Daima utavitaka, tele vimo moyoni
Vipi nitakutungia, nawe humo tenzini?

Kumbe mkali wa vina namna hiyo bibie? Hongera zako.
 
Niko hoi kwa hizi tungo! Kumbe Miss J nawewe HAWAVUMI LAKINI WAMO! SENKI YUU!
 
kwa kweli nina kila sbb ya kumshukuru Mungu kwa kuniongezea watu wenye mapenzi nami,coz nilidhani kama niko humu chimbo na Uporoto01 wangu ni nani mwingine atakayenimiss?kumbe I was wrong,kumbe wengi mnanimiss kama ninavyowamiss,tena ni juzi tu nilikua namuandalia Uporoto01 biriani nikaliunguza sbb nilikua namuwaza sana 'kaka' Kashaijabutege,kumbe na yeye huku alikua ananimiss.
JAMANI NAFURAHI SAAANA KUONA WAPO WACHACHE WANAOPFURAHIA UWEPO WANGU HAPA,nawapenda sana nyote mlio na mapenzi mema kwangu.
Asante sana Kashaijabutege,nimukutengenezea nafasi special ktk mtima wangu.(Uporoto01 ntakufafanulia hapa tukiinga chumbani sina maana mbaya).
Mungu akubariki sana.
 
Nimefurahi umewajibu na Kashaijabutege kuna nafasi ya kuwa 'penpal' wa Cheusi lkn mambo ya kumtungia mashairi MARUFUKU! utahatarisha siha ya penzi letu ukizingatia mimi sijui kutunga,nadhani umenielewa.Na babe nashukuru kwa kunirudisha kwenye signature it means a lot to me,thanks.
 
baby don worry kabisa,hata nikikutoa kwenye signature lkn moyoni daima utabakia.

ila ujifunze umalenga kidogo basi siku moja moja unitungie tenzi.
 
hihihi...pole sana ndugu Kashaijabutege....ukweli ni kwamba Cheusi na Uporoto01 walikuja kunitembelea hapa Yaeda wiki iliyopita na walinieleza wanaelekea Mang'ola....sasa anachosema hapo juu huyu Uporoto01 ni mapya....labda atueleze zaidi yu wapi huyu kimwana

preta bora wee useme,huyu Uporoto01 kauli zake sometimes zinanitatiza,sijui anamuogopa nani hadi hataki kusema yuko na mm.
anyway acha nimsamehe tu coz kumnunia siwezi.
 
kweli umeishampenda, bila kujali weusi,
sasa watoa tenda, asakwe kama muasi,
huku wadondoka denda, kama mpanda farasi,
cheusimangala aja, kaa mkao wa kula

heri uketi kitako, ajapo iishe hamu,
sio urande makoko, asijekukuta homu,
kisha useme mnoko, eti kakupa pumu,
cheusimangala aja, kaa mkao wa kula

nasikia yuko mahali, hanemuni ndo shughuli,
tena hataki maswali, ya jaji wala wakili,
hawezi hata kuswali, yuko bize kama kuli
cheusimangala aja, kaa mkao wa kula

ngoja nitakurudia, kukujuza yalomsibu,
ikiwa ataridhia, kumchombeza kibabu,
majuto nitamtia, jamvini aje atubu
cheusimangala aja, kaa mkao wa kula

Kwa jibu hili siwezi, heri maisha yakome,
Nijuzeni huyo mwizi, nikamtwannge na sime,
Cheusi si mdowezi, mie ndio yake ngome,
Wengine magumegume, mie ndie la azizi.
 
jamani ngoja niseme ukweli, huyu Miss Judi kwa kweli ni kiumbe wa ajabu sana, yaani amekamilika karibu kila idara. ngoja nitamPM nimuulize vizuri siri yake, lo!
 
kwa kweli nina kila sbb ya kumshukuru Mungu kwa kuniongezea watu wenye mapenzi nami,coz nilidhani kama niko humu chimbo na Uporoto01 wangu ni nani mwingine atakayenimiss?kumbe I was wrong,kumbe wengi mnanimiss kama ninavyowamiss,tena ni juzi tu nilikua namuandalia Uporoto01 biriani nikaliunguza sbb nilikua namuwaza sana 'kaka' Kashaijabutege,kumbe na yeye huku alikua ananimiss.
JAMANI NAFURAHI SAAANA KUONA WAPO WACHACHE WANAOPFURAHIA UWEPO WANGU HAPA,nawapenda sana nyote mlio na mapenzi mema kwangu.
Asante sana Kashaijabutege,nimukutengenezea nafasi special ktk mtima wangu.(Uporoto01 ntakufafanulia hapa tukiinga chumbani sina maana mbaya).
Mungu akubariki sana.

Achana na Uporoto, atakutia msala,
Rejea kwangu mtoto, kwanini hivyo Mangala?
Nimekusanya kipato, nikakufiche mahala,
Uporoto ni kachala, Cash'ja ni kizito.
 
Achana na Uporoto, atakutia msala,
Rejea kwangu mtoto, kwanini hivyo Mangala?
Nimekusanya kipato, nikakufiche mahala,
Uporoto ni kachala, Cash'ja ni kizito.

Hivi, kashaijabutege,
kumbe shairi linaweza kukusaidia ukango'a mzigo eeeh?
kazi kwake Uporoto01!!!!!!
 
kwa kweli nina kila sbb ya kumshukuru Mungu kwa kuniongezea watu wenye mapenzi nami,coz nilidhani kama niko humu chimbo na Uporoto01 wangu ni nani mwingine atakayenimiss?kumbe I was wrong,kumbe wengi mnanimiss kama ninavyowamiss,tena ni juzi tu nilikua namuandalia Uporoto01 biriani nikaliunguza sbb nilikua namuwaza sana 'kaka' Kashaijabutege,kumbe na yeye huku alikua ananimiss.
JAMANI NAFURAHI SAAANA KUONA WAPO WACHACHE WANAOPFURAHIA UWEPO WANGU HAPA,nawapenda sana nyote mlio na mapenzi mema kwangu.
Asante sana Kashaijabutege,nimukutengenezea nafasi special ktk mtima wangu.(Uporoto01 ntakufafanulia hapa tukiinga chumbani sina maana mbaya).
Mungu akubariki sana.

Na wewe bidada,
uliadimika sana ati,
si unajua tunamis vingi kutoka kwako,
 
Kwa jibu hili siwezi, heri maisha yakome,
Nijuzeni huyo mwizi, nikamtwannge na sime,
Cheusi si mdowezi, mie ndio yake ngome,
Wengine magumegume, mie ndie la azizi.

Achana na Uporoto, atakutia msala,
Rejea kwangu mtoto, kwanini hivyo Mangala?
Nimekusanya kipato, nikakufiche mahala,
Uporoto ni kachala, Cash'ja ni kizito.

kashai siyo kaisha, butege siyo matege?
uporotoye maisha, mtoto yake amege
cheusi wako kaisha, pale kapata kidege,
wenzio wasema pisha, fanya hima usitege

kiumbe yako huruma, dunia kwako katili,
japo mapenzi yavuma, cheusi hachi ukali,
uporoto ndo auma, japo u-radhi kwa mali
wenzio wasema pisha, fanya hima usitege
 
Baada ya kuwa frustrated na Tangold, meremeta, IPTL, DOWANS, tume zisizotoa taarifa hadharani, serikali inayoshughulikia Richmondul miaka 5, Kupanda bei ya umeme, watoto kukalia viroba, wazazi kujifungulia juu ya matenga n.k basi tunapopata mambo kama haya ya malenga wetu, daa nimejisikia burdani kidogo. Ahsanteni wote washairi maana tunapata kitu cha kutabasam angalau. Zaidi ya hayo CheusiMangala amejitokeza yu bukheri wa afya, ahsante na Cheu! Tumeku mr oops! miss.
 
Back
Top Bottom