:A S-heart-2:Ninamsaka Cheusi, Cheusi wangu Mangala,
Mtoto kama mdosi, asopenda masihala,
Naona kama kaasi, sioni zake makala,
Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.
:A S-heart-2:First Ladi nahisi, umemficha mahala,
Ninazo pia tetesi, kwa Preta analala,
Rose mtingisha nyusi, yu wapi wangu Mangala?
Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.
:A S-heart-2:Kila mlo ukakasi, sipati hamu ya kula,
Cheusi njoo upesi, niepe huu msala,
MadamT mkwasi, ni yupi kwangu mbadala?
Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.
:A S-heart-2:Nakuuliza Demsi, ijibu hii makala,
Ninagona kama fisi, usiku nianapolala,
Chapachapa mikamasi, nalowesha matambala,
Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.
:A S-heart-2:Mangala wangu Cheusi, nijuze pako pahala,
Nachekwa kandamnasi, mapenzi yanifanya ****,
Nitajitwanga risasi, nipumzike kwa Mola,
Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.
:A S-heart-2:Kaditama yangu pasi, kwako Cheusimangala,
Una utamu wa tasi, laini kama salala,
Sukari kama fenesi, sehemu gani walala?
Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.