Ukweli, Chadema hawakuwa tayari kwa ajili ya kinyang'anyiro cha urais. Wanafahamu vizuri kabisa kwamba Slaa alikuwa anatetea kiti chake cha Karatu na Mbowe baada ya kugaragazwa ile 2005 na Kikwete akaona njia pekee kutomvaa mwaka huu kwani kipigo kingekuwa kikubwa zaidi. Akajipima akaona ubunge ndiyo size yake kugombea. Sasa Slaa kugombea urais ni kwamba amelazimishwa lakini pia baada ya yeye nae kuwawekea masharti magumu Chadema kuwa baada ya Oct 31 waendelee kumpatia stahili zake alizokuwa akizipata kama mbunge. Slaa aliamua kuwapa kisogo wana karatu kwa ajili ya mkataba huo akijua wazi hawezi kushinda urais na vilevile lolote lingeweza kumtokea Karatu kama angeamua kugombea ubunge.
Nini kilichotokea?
Chadema kwa vile haikuwa na mgombea, basi ilibidi wakurupuke na kuanza kukamatia yeyote ambaye alikuwa karibu, walijaribu kichinichini kuwashawishi baadhi ya big name ndani ya CCM hasa wale ambao wanawaponda kwa kuwatuhumu sana, lakini wakapigwa chini. Baada ya kukurupuka huko kwa Slaa, wakagundua kuwa hawana mgombea mwenza, wakataka kuwa-fool CUF kwamba waunganishe nguvu na Hamad Rashid awe mgombea mwenza. Lakini wakasahau kuwa tayari walishavunja makubaliano na CUF katika chaguzi mbalimbali ambazo CUF waliomba kusimamisha mgombea mmoja wa upinzani. Kana kwamba haitoshi Chadema ilionesha dharau kubwa kwa CUF kwamba wao wana uwezo wa kwenda kwenye uchaguzi peke yao matokeo yake jimbo la Busanda na Mbeya Vijijini wakayakosa CCM ikaendelea kuyashikilia.
Baada ya mambo kuwa magumu na kutokukubalika zaidi Zanzibar, Chadema ilichofanya ni kutafuta 'bora mgombea mwenza' ili itimize masharti ya NEC lakini wakijua kabisa wanachofanya ni kuwahadaa wa Zanzibar kwani hawana mpango wowote na Muungano. Kwahiyo basi mgombea mwenza yule yupo kama figure tu kwa ajili ya kutimiza masharti ya NEC na wana uhakika kuwa kuwapo kwake sitatizo kwani hawawezi kuupata urais na yeye kuwa makamu wa rais.
Falsafa iliyopo hapo ni kwamba tayari chadema walikwisha shindwa uchaguzi kabla hata mchakato haujaanza na ukitaka kuthibitisha hivyo fuatilia kampeni zao hakuna lolote wanaloelezea zaidi ya hadaa na mambo ya kufikirika tu.
Hopeful this time mgombea mwenza huyu 'hawatamjumbe' ili kusogeza uchaguzi mbele. Maana 2005 walipoona wanazidiwa duh...!!!