Tegelezeni
JF-Expert Member
- Dec 31, 2009
- 268
- 124
Yampita majuma kadhaa huyu mzee wetu Mjasiriamali Reginald Mengi simuoni wala sijamsikia kwenye vyombo vya habari kama kawaida yake. Nimeshangaa sijamuona hata kwenye msiba wa mtangazaji maarufu wa BBC Marehemu John Ngahyoma ambaye aliwahi kufanya kazi kwenye kituo chake cha luninga cha ITV, na hata kwenye msiba wa Halima Mchuka pia sikumuona, nikajiuliza kulikoni?
Huyu mzee amekuwa msitari wa mbele kujitokeza kwenye shughuli mbalimbali za kijamii hususan misiba ya watu maarufu ikiwemo ya waandishi wa habari. kuna mdau kanijulisha kwamba na yeye ni mmoja wa wananchi waliokumbwa na mafuriko yaliyolikumba jiji la Dar hivi karibuni, yaweza kuwa ni sababu ya kuadimika kwake?