Shing Yui
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 15,168
- 38,049
Ukweli ni kwamba, yanayoendelea kwenye hii nchi yanaumza.
Lakini kabla hatujatupa lawama kwa Amiri Jeshi mkuu lazima tujue kwanza alipo na tujue nini msimamo wake kwenye mambo yanayowafanya wananchi wake wanong'one chinichini kama makinda yasiyo na watoto.
Tangu tumepandishiwa miamala hatujamsikia ila tumemsikia waziri wake akitukejeli wananchi kwamba tuhamie Burundi.
Tangu kiongozi wa chama kikuu cha cha upinzani Mh. Mbowe alipokamatwa na kuhusishwa na ugaidi hatujasikia sauti ya rais wetu.
Kuna matamko mbalimbali ya viongozi wa uma kuhusu covid19 lakini hatujamsikia mama! Yuko wapi?
Je, tangu ameapishwa kuna wakati amewahi kupiga kimya namna hii ukizingatia kuna update ya matukio mbalimbali yanayohitaji kauli yake?
Kwenye miamala tuliambiwa amesikia kilio chetu lakini mpaka muda huu sio miamala imerudi kawaida wala sauti yake. Hii sio kawaida!
Mwanzoni vifurushi vilipanda bei akatokea fasta na ile kauli yake ilifanyiwa kazi ndani ya siku mbili vifurushi vikarudi kwenye bei ya awali.
Nikiwa raia wa Tanzania naomba rais aongee na taifa