Yu wapi Rais Samia? Baada ya matukio haya, ni vema aongee na Taifa

Mbowe anahusishwa na kutaka kuua viongozi wa serikali, baadhi ya bavicha humu wanadai mpira utarudishwa kati muda si mrefu, rais haonekani, tetesi kuwa jpm haikua natural death...
Mambo ni mengi kweli...atoke hadharani aonekane kwa kweli. Je anaumwa?
 
Gwajima na yeye katangaziw waumini wake wasichanjwe chanjo ya corona - anapingana waziwazi na serikali yake..

Nchi kwa sasa haiko sawa.
 
Watendaji wake wanamgomea wanamdharau check ishu ya tozo mwigulu ndo kwanza yupo kwenye kampeni ya kujipigia debe uraisi 2025 keshaanza drama tunduma za kukusanya watu kuzuia misafara.
 

Nimesikia mahali inasemwa hafiki 2025,naanza kuelewa.

Kuna harufu Kali ya uhasi,yafuatayo yanafikirisha;

....makamu wa Rais kumsimamisha DED bila kuzingatia mamlaka ya uteuzi,

....Mwigulu kuinuka kuonyesha kutotii maagizo ya Rais,

....Gwajima kupingana wazi na agizo la serikali kuhusu chanjo,

....uchelewaji wa uteuzi ktk nafasi za DEDs,

....ukimya wa Rais. Kuna jambo kubwa linaendelea la uasi ndani CCM na si muda mrefu bomu litalipuka,na uenda safari za Burundi ni kuandaa kimbilio baada ya bomu kufyatuka.
 
Tutaitwa wabaguzi ila ndio ukweli, hii nchi haiko tayari kuogozwa na wanawake. Wako emotional zaidi. Mama mwoga wa kufanya maamuzi magumu kisa anaogopa umiza watu sababu ya usofti wa uanawake hawataki lawama.


Ni kweli tutawaita wabaguzi.
Hata wanaume wapo ambao ni high emotional sana tu.
Mtu kuwa na subira katika maamuzi isitafasiliwe kama ni uoga wa kufanya maamuzi magumu .

Sasa hao wanaume ambao ni less emotional na wenye kuweza kufanya maamuzi magumu wametufikisha wapi tangu Uhuru?

Mbona mambo kama ni yaleyale tu ?

Jipya ni lipi ?

Imeandikwa : hekima itokayo juu ni safi, ina upole, amani, ina utayari wa kusikiliza mawazo ya watu .
Imejaa rehema na matunda mema.
Haina fitina, haina unafiki.

Someni Yakobo 3:17
 
Tutaitwa wabaguzi ila ndio ukweli, hii nchi haiko tayari kuogozwa na wanawake. Wako emotional zaidi. Mama mwoga wa kufanya maamuzi magumu kisa anaogopa umiza watu sababu ya usofti wa uanawake hawataki lawama.
Tayari ilishaonekana uongoz imemshinda
Huyu na washauri wake ndo hao
Kina ndugai na mwingilu

Kwakweli naona bora jk achukue Tu hii
Nchi Kwa mara nyingine
 
Napingana na wewe! Akae kimya ila aongee kupitia Wasaidizi wake
 
Mkuu tindo ,hakuna kitu kinachouma kama watu waliokuwa wakikuamini kupoteza imani yao kwako halafu na wewe ukajua wazi kuwa huaminiki tena. Aiseee inaumiza mno mno.
Kibinadamu, kuaminiwa na binadamu wenzako kunaleta furaha,faraja na amani ya kipekee.
Kibinadamu, kupotea kwa imani kwa binadamu waliyokuwa nayo awali juu yako,huleta mateso makubwa ajabu.
Hilo hupelekea watu kuanza kufanya matendo ya kulazimisha kurudisha imani tena.
 
Ni hivi majuzi tu alionekana akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair. Labda kuna majukumu mengi yanamtinga ikiwemo kuandaa mkeka wa Wakurugenzi wapya wa Halmashauri.

Aidha, tusisahau kumwombea kwa Mungu awe na afya njema na hekima itokayo juu, maana kazi ya urais si lelemama!

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
lakini kweli voo Raisi Samia tulikwisha mzoea haipiti wiki karusha vitu,ila naona ni mda, hivi ka na yeye akifa atarithi mwingine ?
 
Point of correction; Vifurushi vya muda wa maongezi/simu havikuwahi kurudi kwenye hali yake ya awali.
 
Ccm wanamvuruga sana huyu mama yote haya na mabadiliko yake baada ya siku 100 yalibadilishwa na kikao cha dharura au cha kikanuni cha ccm pale Dodoma baada ya hapo tu mama amebadilika kabisaaa sijui wamemfanya nn au wamemtisha nn
 
Alipost twitter kifo cha Mngwhira reaction ya watu ilikuwa kali sana hasa tozo na Mbowe
 
Na tuambiwe pia hao viongozi Mbowe alioshiriki kuwaua ni kina nani na alikuwa akishirikiana na kina nani katika kuwaua.
Na hao viongozi waliokusudiwa kuuawa na mbowe wajitokeze,na je walifungua jalada polisi.
Wananchi tujue unafiki wa mbowe kujificha kwenye chama huku Gaidi,watu wanashindwa kunywa maji vikaoni kisa Mbowe.
 
jeshi na polisi ni sukuma gang wamemwambia tulia tufute upinzani.
Jeshi letu la polisi na jeshi la wananchi wa Tanzania hawana ukabila wala hawako tayari kupanda mbegu ya ukabila nchini.

Tatizo la ukabila ni la baadhi ya wanasiasa
 
Yani napata tabu sana.
Hajaonekana mida sasa
Na haikuwa kawaida yake. Alikuwa ni mtu wa watu, mtu wa ziara nyingi, mwenye kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua kwa wakati pale inapowezekana
 
Lengo la kuuliza alipo ni kutokana na mambo ya ajabuajabu yanayoendelea kwenye nchi alafu yupo kimya ukizingatia tumezoea wiki haipiti bila kumsikia au akiwa kwenye ziara za ndani na nje ya nchi.

Kwanini wakati huu wa kauli mbovumbovu za wasaidizi wake ndipo awe kimya?
 
Style ya kuhutubia na kujibu jibu kila wakati ilikuwa ya mwendazake. Mama amerudi kwenye urais taasisi enzi za Marais kuonekana kwenye jambo zito.

Mbowe kukamatwa yupo Waziri wa mambo ya ndani na IGP. Tozo waziri yupo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…