Yu wapi Tido Mhando?

Nimeipenda. Aaaah:laugh:


Mkuu umenena hapo. Huku tunaishi kwa ujanja ujanja na wizi wizi, na tunachukia wataalamu wanapotofautiana na wishes zetu. Natamani TUNISIA ihamie hapa, tuwachape JK na wezi wenzake hadi wakimbilie Costa Rica.😛lane:
 
Kweli kuna watu hawaoni mbali, unafikiri tunisia ikihamia hapa JK na hao unaosema watadhurika? watatoroshwa na kusaidiwa waliokula kiapo kwao. Mimi sitaumia maana nina vihela mbuzi nitaondoka zangu nchi za jirani ila bibi yangu, shangazi zangu, baba na mama wadogo pale kijijini ndio watakaoumia na ndio ninaowaonea huruma maana wao ni innocent. Wakienda costa rica kwa taarifa yako maana wana pesa watapokelewa kama wafalme maana watawekeza huko kwa masharti nafuu bila 10% ohooooo. Niambie tunisia waliokamatwa ni kina nani kama siyo ndugu wa rais wanaoishi katika mazingira magumu? Inamaana Tido akifa na TBC ingekufa? Amefanya yake makuu na naamini atakua ameiacha katika mazingira yaliyotukuka hata kama ni watu kupenyeza madudu lazima watafanya hivyo kupitia yeye kwa hasira zake la sivyo itakaa vyema kwa muda mrefu. Kuna haja ya TIDO kuajiriwa na media binafsi ili tuone umahiri wake kwani lazima awe serikalini?? Kuna nini huko serikalini wakati media house binafsi wanalipa mshahara mnono zaidi??
 

Kipindi hicho alikuwa analinda kibarua chake
 
Utangazaji wa kibongo hauwezi ila sijui itakuwaje manake bbc nao wanataka kulay off wafanyakazi!
 
Tido alikuwa ameshastaafu BBC so hawezi kurudi.Kwa sasa yuko zake London na familia yake.Kwa kweli wataalam wetu chini ya CCM wanadhalilishwa sana na hata walioko nje kwa hali hii hawawezi kurudi kulisaidia taifa
 
Ameondoka akiwa bado anahitajika, hiyo imetulia kuliko angeondoka na kashfa. Kwa peak alikoifikisha, panahitajika jembe la nguvu!
 
Chama kwanza kisha takataka zingine zinafuata baadae.
Kama hulindi wala kuboresha maslahi ya chama hata kama wewe ni malaika ziraili watakutupa nje tu....
Cheza na yooote bali usicheze na maslahi ya ccm
Sijutii Tido kuondoka maana alishiriki kujenga unafiki ktk utangazaji pale tbc lakini aliijengea sehemu ya heshima tbc. Kinacholeta tashwishwi ni namna alivyoondoka. ametimuliwa kama pepo....
 
Wanajamvi anaefahamu aweke wazi hapa, Tido yupo wapi sasa baada ya kutemeshwa mzigo TBC. zipo tetesi anataka kurudi BBC, kweli???

Huyu Tido angekuwa fisadi angepeta pale TBC1! Pole sana Tido, umeponzwa na uzuri wako kama vile chui naye huponzwa na uzuri wa ngozi yake hata anauawa na wawindaji ili kuipata ile ngozi!
 

Walau umekuwa mkweli kuwa uwezi kujutia kuondoka kwa Tido sababu watu wengi mmezoea ubabaishaji! SHAME
 
pole sana tido, ccm wamekulamba dume..utakuwa mgeni wa nani sasa jamani, bora ungekuwa upande wa wapinzani pengine tungesema utakuwa mgeni wa wapinzani...lol.
 
TIDO wakati akiaga wasikilizaji wake pale BBC kwenye kipindi cha Wiki Hii alisema kwamba mkataba wake na BBC ungekwisha by 2014 lakini anajisikia faraja kurudi nyumbani kwa ajili ya kuitumikia nchi yake,kwani ni heshima kuombwa na rais,nami nilifurahi sana lakini kilichotokea sikuamini na ndipo nilipoamini kuwa AFRIKA INAUA VIPAJI VYAKE YENYEWE:twitch:
 
at least kaondoka na dignity yake in place
 
thanks man.....ndio maana nataka kukimbia nchi.....watz mlioko uko msirudi....
Ingawa kila mtu ana haki ya kuamua wapi aishi, bado ninawashauri watz walioko nje kurudi nyumbani kusaidia kuing'oa CCM maddarakani kabla ya 2015.
 
u have said everything
Yaliyomkuta Tido ni mwanzo wa wataalam wa nchi hii kukataa kurudi tena Tanzania kufanya kazi maana huku bado watu wako ki-ccm ccm na sio kwa maslahi ya taifa
 
Viongozi wetu (sisi-M) wanapenda watu wanao-dance to their tunes, a slight mistake U r out! thank God wasipoku-kolimba.
 

Hii ya kusema Tanzania ina wenyewe ndiyo kauli inayotufanya tuwaachie wajinga wachache waendelee kutawala nchi hii na kufanya maamuzi yanayomuathiri kila mmoja. Tujizatiti kudai nchi yetu na kuwaonyesha kuwa tuna uchungu na nchi hii. Kumbuka ule msemo nchi inajengwa na wenye moyo (na kwa Tanzania) inaliwa na wachache wenye meno...
 

Wenyewe hawajijui pamoja na kuwa wengi (zaidi ya 40 million), wamewaachia mafisadi na vibaraka wao wakitamba!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…