Habari zenu wakuu,
Huyu mwanadada Jackie Marie alivuma Sana na nyimbo yake Tulia mpenzi lakini tangu hapo hajawahi kutoa nyimbo nyingine Tena. Ni miaka mingi imepita, nadhani hata kizazi Cha Sasa hivi hakimtambui. Natamani kujua social media anatumia jina gani angalau nimfatilie mhenga yule.
Tulia mpenzi inabaki kuwa my all time favorite Kuanzia mistari ya nyimbo Hadi video. Nikipita YouTube lazima niichungulie, Video yake hadi leo inanivutia.