Sajenti
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 3,651
- 413
Huyu bwana alikuwa mmoja wa waandishi mahili wa habari za michezo katika gazeti la mfanyakazi miaka ya 80 mpaka 90. Nakumbuka mwaka 1985 kwenye kombe la challenge timu ya taifa ya Zimbabwe ilishiriki kama inavyoshirikia zambia mwaka huu kule Kenya na hatimaye kuchukua ubingwa, jamaa alikuwa anatoa ripoti zenye kiwango mtu unaweza ukadhani kama vile na wewe unashuhudia yale mashindano. Kwa kuzingatia mazingira ya wakati ule na hasa teknolojia ilivyokuwa duni kwa gazeti la mfanyakazi kila jumamosi toleo lake ka michezo lilikuwa bomba sana. Kuna mwana-JF anafahamu huyu bwana alipo? Nilitegemea kuendelea kusoma makala zake sasa kwa kuwa kumekuwa na utitiri wa magazeti.