Yuko wapi James Nhende??

Yuko wapi James Nhende??

Sajenti

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2008
Posts
3,651
Reaction score
413
Huyu bwana alikuwa mmoja wa waandishi mahili wa habari za michezo katika gazeti la mfanyakazi miaka ya 80 mpaka 90. Nakumbuka mwaka 1985 kwenye kombe la challenge timu ya taifa ya Zimbabwe ilishiriki kama inavyoshirikia zambia mwaka huu kule Kenya na hatimaye kuchukua ubingwa, jamaa alikuwa anatoa ripoti zenye kiwango mtu unaweza ukadhani kama vile na wewe unashuhudia yale mashindano. Kwa kuzingatia mazingira ya wakati ule na hasa teknolojia ilivyokuwa duni kwa gazeti la mfanyakazi kila jumamosi toleo lake ka michezo lilikuwa bomba sana. Kuna mwana-JF anafahamu huyu bwana alipo? Nilitegemea kuendelea kusoma makala zake sasa kwa kuwa kumekuwa na utitiri wa magazeti.
 
Hata mimi namkumbuka sana ila namimi sijui alipo.Ningefurahi kujua alipo maana namimi umenikumbusha mbali sana enzi zile za kina Eduard Chumila(marehemu),Malota Soma,Salum Kabunda,etc we acha bwana!
 
Huyu James Nhende yupo Mwanza, anapatikana sana maeneo ya Salma Cone, Sizzler restaurant , Mwanza Hotel. Ana gazeti lake binafsi hapo Mwanza sina uhakika na jina la Gazeti. Kiufupi yupo mjini mwanza ukimuulizia unampata.
 
Juzi juzi nilimwona jijini MWANZA akiwa amefunga mkono wake PLASTA
 
Ni kweli nami kadhalika namkumbuka katika gazeti la mfanya kazi lilikuwa likitoka kila wiki, vp gazeti analo miliki halifiki au halizambazwi Tz nzima? Mi namsalimia sana
 
Tunashukuru kujua kama bado yupo.Ila tutafurahi tukipata hilo gazeti lake.
 
Tunashukuru kujua kama bado yupo.Ila tutafurahi tukipata hilo gazeti lake.
Au gazeti la Mzawa?Maana mwanza kuna msanii Afrika na Mzawa. Msanii Afrika ni la watu wa Star TV (mh Mbunge), mzawa sina hakika
 
Back
Top Bottom