Yuko wapi Kibakuli mdogo wake Nyama yao

Yuko wapi Kibakuli mdogo wake Nyama yao

Habarini Wadau,

Leo katika moja ya igizo la hapa nchini nimefanikiwa kumwona Nyamayao, msanii mahiri aliyeanza uigizaji akiwa binti mdogo kabisa ila kwasasa amekuwa mwanamke hasaa.

Baada ya kumwona nikamkumbuka dogo mmoja alikuwa akiigiza naye aliitwa Kibakuli. Mara nyingi waliigiza kama watoto wa Mhogo mchungu na igizo lilirushwa na ITV.

Huyu dogo kapotelea wapi? Bado anaigiza?
Kibakuli siku hizi kawa Camera Man.

Muvi nyingi tu za kibongo anahusika kwenye jopo la waandaaji yeye akiwa upande wa camera man.
 
Sema picha yake google haipo ila namfahamu jamaa. Kabonge kafupi cheupe na ana matatizo ya macho. Na taarifa za msiba alizirusha zamaradi clouds tv kupitia take one.

Huyo ni mlopelo ndo aliyefariki. Kibakulu yupo hai
 
Mropelo n huyu na kishadanja
20210511_110726.jpg
 
Back
Top Bottom