Yuko wapi memba akili kubwa Barafu?

Yuko wapi memba akili kubwa Barafu?

passion_amo1

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2023
Posts
1,828
Reaction score
3,922
Wakuu Heshima mbele.

Kwa kweli miaka ya nyuma kidogo kabla ya kupoteza akaunti yangu ya Jamii forums. Nilikuwa napenda sana kumsoma jamaa mmoja anaitwa barafu.

Kwa waliokuwepo jamii forums miaka ya nyuma nadhani wengi mtamfahamu mwana jamii forums barafu akianza kuchambua kuhusu mambo ya serikali, akijenga hoja zenye mashiko Kwa kweli nilikuwa nikivutiwa sana na jinsi anavyofahamu mambo mengi sana

barafu alikuwa akianza kuelezea kuhusu serikali, alikuwa anatumia lugha safi isiyo na kejeli,matusi, dhihaka na kashfa katika kuwasilisha kile alichokuwa anakitaka.
Yupo wapi mwana jamii forums barafu??

Baadhi ya nyuzi zake 👇





Kwa kweli barafu alikuwa ni tunu hapa jamii forums siku hizi haonekani kabisa.

Nani wa kumrithi barafu hapa sasa Jf katika Upande wa kuelezea vitu vya serikali na kujenga hoja kwa wakati huu?

Nimebaki ninamsoma Kiranga DR Mambo Jambo Mama Amon na Maghayo kama kifungashio cha ziada.
 
Back
Top Bottom