Yuko wapi Producer Allan Mapigo?

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,154
Reaction score
31,246

Leo nimesikiliza hii ngoma ya Makamua enzi zile za wakali kwanza. Ila hawa jamaa walikuwa wanajua bwana kweli wakati ukipita hata uwe wajua vipi basi muda ukiisha umeisha.

Ngoma kaitengeneza Allan Mapigo. Enzi zake ametengeneza ngoma nyingi za Banana Zorro, Hafsa Kazinja na hits kibao.

Alikuwa mkali sana wa Zouk ila siku hizi simsikii kabisa.
 
Mimi nahitaji kujua wapi hiki kipaji kilipokosea kikapotea, VUMILIA wa Tatizo umasikini producer Allan Mapigo na Utanikumbuka chini ya Mika Mwamba
 
Mimi nahitaji kujua wapi hiki kipaji kilipokosea kikapotea, VUMILIA wa Tatizo umasikini producer Allan Mapigo na Utanikumbuka chini ya Mika Mwamba
Vumi ni habari nyingine yule na dada naelewa sana ngoma zake has Duseh dushe
 
Itakuwa aliolewa, mademu wakiolewa tu muziki basi tena... hapa mifano mingi.
Basi atakuwa amefanya jambo la maana kuipa kipaumbele ndoa yake kuliko mziki lakini yule dada nyimbo zake nazipenda sana
 
Vumi ni habari nyingine yule na dada naelewa sana ngoma zake has Duseh dushe
Yule ni kipaji kikubwa ambacho hakipo kwenye midomo ya mashabiki na kibaya zaidi bongo huwa hatuthamini wasanii ukipita umepita
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…