Yuko wapi wa kuvaa viatu vya Ruge?

Yuko wapi wa kuvaa viatu vya Ruge?

Kunufaika kwa kuwapa promo wasanii hadi awagonge?? Hapana aisee, Nahisi kina Ruby walimbania ndio maana akawapiga chini.

Ogopa sana aina hii ya watu mkuu.

Haiingii akilini wadhamini wamechanga mamia ya mamilioni kudhamini fiesta halafu msanii anapewa eld 40, rubbish kabisa
Alikuwa anamgonga barnabas au amini?
 
Huwezi kuona thamani ya kitu mpaka siku ukikose!

Wako wapi wasanii wale waliopiga kelele kuwa wanashindwa kung'ara kwakuwa marehemu Ruge alikuwa anawanyonya? Wengi nawaona wakiwa na hali mbaya kuliko hata kipindi cha kunyonywa na marehemu.

Leo sitajadili uwezo na vipawa vya Ruge kwenye tasnia nzima ya mziki wa kisasa lakini kuna siku historia itampa heshima anayostahili...Ninachotaka kusema hapa ni kwamba kama hujui basi katika kundi ambalo halina shukrani wala fadhila basi ni hili kundi la wasanii wa kibongo, wote wa mziki na maigizo kwa mukatadha wa mada hii

Hulka sugu ya hawa watu ni ile dhana ya kupenda kitonga kwenye kila kitu.. Utamtoa jalalani uswekeni akiwa ni kapuku asiye na mbele wala nyuma utatumia gharama kubwa kumbrand na kumng'arisha... Akishang'aa na kuonekana mtu kati ya watu, thamani yako inakomea hapo

Atasahau kila kitu
Atasahau namna ulivyomfadhili
Sehemu ya kulala
Mavazi na mapambo
Chakula na vinywa
Usafiri
Gharama za studio
Matumizi ya kila siku nknk
Ole wako...nasema ole wako akishakuwa maarufu uje umkumbushe ulikomtoa ama ujaribu kumshauri kitu.. Utajuta kumfahamu

Sakata la Harmonise na lundo la tuhuma kwa Diamond limenikumbusha mengi lakini pia limefunua na kufumua mengi...Hakuna ubishi Harmonize ni msanii mzuri mwenye kipaji cha utunzi na uimbaji na ni mpambanaji asiyekata tamaa..kushindwa kuliona hili ni wivu mbaya kabisa.. Lakini kinachomsumbua ni vitu viwili vitatu
Hulka
Elimu/ uzoefu
Wapambe/makundi
Hulka ya kulalamika na kutaka kuona kaonewa sana, hili linatokana na kukosa uzoefu wa maisha unaotaka na elimu haba toka kuhitimu mpaka ajira

Wapambe na makundi.. Hawa ndio wanaweza kuwa kaburi lake kisanaa.
Ni kati ya hawa bila kumpamba pamba kwa maneno mazuri na matamu wanaona kula yao iko hatarini.Hawa ndio chawa wenye kutunga kila aina ya uzushi
Kuna makundi ya washindwa.. Hawa ni haters wa Diamond , wamo wasanii na wasio wasanii, hawa wanamtumia Harmo kutolea hasira zao kwa Mond..Yaani wanaona kushindwa kwao kumesababishwa na Mond

Hawa si kwamba wanampenda na kumjali sana Harmo la hasha wako naye hapo kutaka kupata kula yao lakini pia kutaka kumdidima Mond.. Ni kundi lenye wivu na roho mbaya sana na ni kati yao hao watakaokuja kumgeuka Harmo atakapofanya vizuri zaidi.. Ni kundi hili ndio lilikuwa mstari wa mbele kumsema marehemu Ruge leo limemgeukia Mond

Udhaifu wa mikataba upo popote pale duniani.. Labda pengine Harmo halifahamu hili..kupigwa kwenye mikataba ni jambo la kawaida sana, kama nchi na wasomi wake wote inabamizwa itakuwa yeye? Akumbuke hata lebo yake ya Konde boy kama ikisimama vema na kukua itakuja kukumbana na changamoto hizihizi anazozishikia bango kwa Mond

Ishu ya kusema kuwa alituhumiwa kutaka kumzidi boss wake hayo ni mambo ya kawaida sana mbona? Awaulize walio kwenye ajira hasa sekta binafsi ataambiwa.. Nguo nzuri kumzidi boss zinaweza kukuondoa kazini...
Je ya JK na Lowassa anayajua? Shetani mwenyewe alipoleta ujuaji na kutaka nafasi sawa na Mungu alipatiwa haki yake! Mond kafanya ni bjnadamu, Harmo naye atakuja kufanya.. Boss huwa anabaki kuwa boss kataa kubali!

Katuonesha mfanano wake na Musiba...Kumbe kule kujikomba kote kwa mwendazake ni kwa vile alisaidiwa madai yake! Akasahau kila kitu akajitia upofu mkubwa na kumbwagia kila aina ya sifa hata kama mamilioni walikuwa wanaumia..huu ni ubinafsi na choyo kikubwa

Ameshatapika ya kutosha sana, pengine ana nafuu sasa.. Lakini huu ndio muda wa kujitafakari zaidi.. Aliyemshambulia sana hajamjibu kabisa.. Hili linaumiza pia. Dunia tunayoishi ni ya survival of the fittest .. Ile ya upendo na huruma aliondoka nayo Kristo...Ishu ya kupata connection serikalini kupitia JP inamjengea maadui bila kujijua na wengine kati yao ni hao alionao sasa

Viatu vya Ruge bado vinatafuta mrithi
Huwezi kuwa partisan kwa msanii ubaki salama.Huwezi ku-side na mtesi halafu Wateswa wakushabikie.Neutrality or if necessary siding with justice matters a lot.
 
Neutrality or if necessary siding with justice matters a lot.[emoji1534][emoji1545]
 
Team mondi kazini

Umerukaruka weeeee ila lengo lako lilikua ni huyo mmakonde tu
 
Umezunguka zunguka kujifanya unamsifia Ruge lakini nia yako ulitaka kuzungumzia Harmonize na Diamond ungeenda tu direct. Mbona Diamond alishalalamika sana kuhusu Ruge na watu wakamshambulia Ruge, leo akisema Harmonize mnaleta mabandiko yenu...

Kitu kingine Harmonize hajakataa kusaidiwa anacholalamika yeye ni kuendelea kuandamwa wakati alifanya kila kitu kulingana na matakwa ya mwajiri na mikataba ilivyotaka
Huyo harmonize kaandamwa kivipi?
 
89% ya andiko ni Harmo na Nasib wakati kichwa ni Ruge na tasnia ya habari/Sanaa

Ok! Kila mtu afanye kile anaona kinafaa
Ukiniokota jalalani ukanifanyisha kazi na kujilipa, bas huo sio msaada, hiyo n kazi na tahesabu km ulinipa kazi na sio msaada
 
Uandishi ni sanaa na sanaa haina mipaka
 
Moja ya fikra pevu
1638110420086.jpg
 
Ushindi ni lazima uwepo uwe unataka au hautaki lakini uwe ni ushindani ambao ni Fair Competition. Hii tasnia ya muziki bado ina makando kando mengi sana achilia mbali wasanii wenyewe bado wana changamoto zao kibao, bila shaka Diamond pia anamtambua Ruge ni nani ? Hayo mambo amefanyiwa Tupac na Suge Knight kwenye mikataba iwe kwa Harmonize ?

Lazima tujifunze kitu kimoja kwenye hii Dunia kitu chochote usichokijua ni lazima ukilipie gharama kwa namna yoyote. Leo hii ukitaka kuanzisha biashara ya aina yoyote ile cha kwanza ni Gharama. Lakini sisi hizi gharama tunazozilipia tunaziona ni mateso na tunasahau kuwa mioyoni mwetu zinatusogeza kwenye ndoto zetu. Wabongo bado ni watu wanaogopa ushindani sana.

"Watu wanaokushauri ufanikiwe ukianza kuonesha juhudi na mafanikio kuwapita wao wanaanza kuona unashindana nao". Tunafanikiwa zaidi kwa kuwanyanyua watu.
 
Back
Top Bottom