Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yule jamaa alikuwa akipita mafinga pale akitokea tunduma kuanzia changarawe ni full bati watu wakiiona utasikia kisu hicho pisheni! na amewahi endesha basi la songea-mbeya likiitwa Turbo express hatari sana huyu mwamba,where are you my legend?Mara ya mwisho nilipanda basi la Tawaqal nikitokea mkoani Ruvuma lakini kwa sasa ni muda mrefu Tawaqal zimeachana na route hiyo.
Nauliza Wahenga wale wa " Watu wa safari" huyu nguli wa barabarani dereva Giriki yuko wapi siku hizi?
Kazi Iendelee
cc: Bujibuji
Dah,jamaa ana moyo wa chuma.Giriki ni kweli alikua anakimbiza sana bus na sifa yake kuu hajawahi pata ajali alikua makini mno mimi nimepanda bus zote alizoendesha maana kila mwenye bus mpya anapanda dau ili kutengeneza soko ila zingine ni chai tuu sio katili wala hana roho mbaya ya kuwasababishia watu ajali na alikua na roho ngumu mno kwa kutowaogopa trafiki na polisi yeye dakika chache kupelekwa central bus na abiria ilikua kitu cha kawaida ilifikia mpaka RTO wa Iringa akatoa angalizo kwake akipita na bus yeyote akiiendesha ataenda jela ikabidi abadili njia ya Mwanza aliipoona wanamfatilia akaingia kwenye maroli ya songea yanayobeba makaa ya mawe sasa hivi alikua kwenye roli za Tanzania zinazopeleka mizigo DRC mimi mwenyewe alikua rafiki wa ndugu yangu ila nikiona dereva ni yeye hilo bus narudisha tiketi nisharudisha mara mbili ukikata unaambiwa dereva sio giriki baadae ukimuona unaleta uzushi na tiketi wanarudisha fedha kwa sababu ishu ikiwa mbaya wanajua jamaa ana misala vituo vyote vya barabarani bora mmalizane mnazi mmoja hapo...
Dah ndugu umekumbuka hadi leyland victory wengi walisema ni mbadala wa scania KAMATA walikuwa wa kwanza kuzimiliki kwa kweli zilikuwa zinajitahidi sana milimani.Kuna ile iliitwa Navalonge Swela Dar - Iringa
Tulitoka Iringa saa 1:30 usiku tukaingia Dar kule Shimoni sokoni Kariakoo saa 9:17 alfajili.
Enzi zile ngoma zilikuwa zinateleza bwashee.... Hii Navalonge Swela ilikuwa ni Leyland Victory inapanda Kitonga kama Scania!
Kuna basi kali enzi hizi liliitwa the big mayaiSharuks : Abbas Gulamali Mhindi wa Ifakara .
Dar Oyee : Gulam Somji Mhindi wa Mahenge.
Halafu kulikuwa na Ulanga Express , mali ya Ushirika wa vijiji vya Tarafa ya Malinyi.
Makete alikuwa nayo nissan diesel mkiikosa sehemu za milimani hamuipati hadi inafika dar.Alishaendesha pia kampuni ya mabasi ya safina syo ...dar - mby
Ila enzi zile Nissan diesel zilikuwa znatembea sana,alafu ile stop engen zake ahh ni balaa
Ova
Kuna moja iliandikwa ez come ez go posta-mwenge ilikuwa bomba sana.Ah mm dar nishakuwa konda kwenye coaster
Za Italy trans na kuna coaster ya baharia mmoja ilikuwa ina chata time will tell
Wamilik wote hao walikuwa wajanjajanja wa zamani,na ili kuwa kufanya kazi na watu kama hao na wakukubali lazima uwe mjanja
Ova
Ilangamoto ilikuwa ni isuzuNissan Diesel UD nazo zilitikisa sana bwashee.
Makete Bus walitoa mbili Dsm - Njombe zilikuwa moto chini na mzee Kiwanga wa Makambako alitoa mbili zikiitwa Ilanga Moto!
We jamaa uko sahihi kajima na konoike zilikuwa tipper zao na hino nazo walikuwa nazo.Konoike/kajima walikuwa na Nissan UD
Tipper zilikuwa balaa
Ova
Matema na kiswele walikuwa na scania injini nyuma kuna isuzu mv 118 ya matema maarufu mv utelezi ikifika tambalale scania zilisanda!Matema beach naye alikuja vzr ila mwishowe akafeli
Ova
Zainab,scandinavia,nyota walianza na bus za carrier hawa enzi hizoZainabu bus mkongwe naye
Ova
Usiwe mbishi wewe,shabiby iliua wate akapona mtoto mdogo kwa ujinga huuAtamzuga nani wakati watu wapo hiyo kila siku road wanajua hadi wapi kuna shimo na wapi hakuna shimo na leo yupo dar kesho mbeya kipi ambacho kitakua kigeni kwake Mkuu hao wanayajua hadi magari ya kampuni za coca au bia ambayo wanapishana kila siku kona za hiyovi anakwambia Kona mbili zijazo tutakutana na roli la coca kwa sababu wapo humo kila siku na muda wa magari ya kampuni zingine wanajua pia ila wewe ukiambiwa utashangaa kweli...
Jamaa anaonekana ni wa jamii za Greece kabisa nilizani ni jina tu. ila hawa madereva wa miaka hiyo wengi sana walisha-RIP. mungu ampe maisha huyu jamaa
Kama iliua wote wewe umejuaje kama sio habari za kupika hizo kwanye ajali yaani yeye awe anasababisha tuu ajali kwa wengine harafu yeye awe anapona miaka nenda miaka rudi akili za wapi hizo ushawahi kuendesha bus wewe likiwa mwendo wa kasi ni kama karatasi na mtu anaogopa gari ya kutoka nyuma sio mbele inapotokea ajali ya nyuma ni rahisi gari kuchochora zaidi...gari ya nani uguse taa ya breki akuangalie wakati hiyo kesi ya mwendokasi tuu alikua anafukuzwa kazi...Usiwe mbishi wewe,shabiby iliua wate akapona mtoto mdogo kwa ujinga huu
Dreva alifanyiwa ujinga huu
Jamaa Taa za break alitoa
we kweli kitamboMatema na kiswele walikuwa na scania injini nyuma kuna isuzu mv 118 ya matema maarufu mv utelezi ikifika tambalale scania zilisanda!