Elections 2010 Yule Asha Mtwangi aliyemhoji Rais ni mtumishi wa Ikulu?

Elections 2010 Yule Asha Mtwangi aliyemhoji Rais ni mtumishi wa Ikulu?

....Hivi mbona jana JK hakuhojiwa na Rose MWAKITWANGE kama ilivyokuwa imepangwa ....maana yule dada ASHA MTWANGI aliyemuhoji ni moja ya waajiriwa wa IKULU chini ya kurugenzi ya habari ........inayoongozwa na SALVA RWEYEMAMU...na kuna wengine pale wakiwamo waandishi wasaidizi waandamizi ie Primi Kabanga...na wengine waandishi ambapo mmoja wao ni Huyu ASHA MTWANGI....

SO tuseme mahojiano ya jana yaliandaliwa na kuendeshwa na kurugenzi ya mawasiliano ya Rais.....


Mimi niliposoma hapa jamvini kwamba Rose Mwakitwange asingefanya mahojiano kama ilivyokuwa kwa Dr Slaa na Lipumba basi nikajua kwamba utakuwa ni usanii mwingine. Hivi hawa jamaa wanadhani wanamdanganya nani na usanii wao? Hivi wanatuona Watanzania ni mbumbumbu sana mpaka wafanya usanii kiasi kikubwa namna ile? 2010 imekula kwao. 😛eace:
 
Kwani we hukuona hta maswali aliyokua anaulizwa? we utauliza je et "mgombea kama ukipata ridhaa unatuahidi nin kwenye elim?" au "kwa kipindi cha miaka mitano ulifanya nin katika elim?"

Hivi hapa unategemea mtu akose jibu kweli?

Angalia swali kama la kibonde la 2025 millenium goal lilivyo mtoa nishai. kwanza sidhani kama anazijua hizo goals za 2025!! ah,anaboatu.

Huyu jamaa mlimsakama sana kipindi fulani leo nimeamin JF ni sawa na ze komedi.
 
Mi niboeka nilipoanza kuona niwaandishi ndo walikuwa wameandaliwa kuuliza maswali. Eti swali hili litaulizwa na Masako aah nikaona kumbe mambo yaliandaliwa na majibu pia alikuwa nayo. Kwa nini hawa waandishi hawakujitoa kujiandikisha na kupeleka maswali yao kwa akina Slaa na Lipumba? Ama walitaka wajulikane kwa Kikwete? Huu ni udhaifu mkubwa nionavyo mimi. Ilinilazimu niende kulala mapema kwa sababu hakukuwa na jipya.
 
so funny,Watz kazi wanayo sana manake wamefanywa wajinga completely
 
Sikuamini masikio na macho yangu pale JK alipokuwa anajibu swali kuhusu ajira ambapo alitaja kuwa mtu akiwekeza kwenye biashara ya Grosari, kwa maneno yake'' mtu akiweka kontena lake atauza bia, soda, sigareti, pale kuna atakayepata ajira ya kufungua vizibo, na kuna watakao sukuma mkokoteni kubeba kreti za bia n.k'' kupoteza muda na kujidhihirisha ni mtu asiye na uelewa mkubwa kujua kuwa kila dakika katika kipindi ilikuwa muhimu kujinadi kwa wananchi, akaunganisha stori ya baa moja maarufu pale kinondoni ambayo watu walikuwa wanasema kuwa usiku maiti zilifufuka kuja kuomba bia baa......
 
Mtangazaji wa tv tumaini/radio tumaini aliyekuwapo ktk panel ile amekiri asubuhi ya leo ktk kipindi cha kahawa au chai kuwa ni kweli waliamriwa kupeleka maswali yao kabla ya jana ili yaidhinishwe yale ya kumuuliza rais. Akaendelea mbele kuwa hali ya jana haikuwa mdahalo bali ni mazungumzo na rais aliyeko madarakani.

Hata kibonde uwepo pale ulithibisha kuwa seriouness ktk media industry haipo na hii ni wazi inatokana na wamiliki wenyewe kuwa compromised na ccm.

Ninashangaa makanisa yanatupiwa maji taka na yenyewe yananyamaza kimya na kuwatuma makatibu wakanushe, nilitegemea kuona kauli kali zaidi toka kwa wakuu wa makanisa kukemea mchezo huu wa timu ya it ya ccm ku chakachua mail akaunti na simu za watu na kupeperusha jumbe za chuki za kidini, wlipaswa waitake serikali kuundan tume ya kitaalamu kuchunguza chanzo za mail hizi na wahusika wawekwe hadharani, huku ni kulichafua kanisa tu just because dr slaa ameitisha ccm na jeikei!!!!!

Sijaridh9ishwa na viongozi wa makanisa kwa namna walivyo react ktk huu mchezo wa hackers wa ccm
 
kibonde ana karama ila anaitemea makohozi kwa bei nafuu, anapaswa akitumie kipaji chake kwa uhakika ili jamii irithi mema na siyo ujanjaujanja wa undumila kuwili.

swali la milenia liliulizwa na geralad hando jana asubuhi ktk power breakfast, majibu ni yaleyale ya usiku runingani.

mkapa aliwapuuza waandishi wetu kwa kutokuwa critical kwenye issue nyeti baadala yake wanaendekeza jungu, outcome ni haya ya jana na ninasikitika kumuona hata kibonde akicheza gwaride haramu in the name of democrasia.

swali la msingi ni kweli chadema wamefanikiwa kuwafumbua macho umma wa tz? Ikiwa mh. Jk atashinda urais kwa urahisi au la si kwa urahisi, basi tutaona mustakabali wa nchi yetu kisiasa.

mungu ibariki tanzania
 
Watz wa sasa wanajua kila...........kiongozi dhaifu anaulizwa maswali dhaifu anatoa majibu dhaifu huyu ndiye kikwete ambaye watz wote wanamjua kuwa ni ndumila kuwili...........chakachueni sana lkn dr.slaa is our presdent
 
Hivi kwanini hawakumuuliza kama akishindwa atakubali matokeo? that is the only question I wanted to hear his response to.
MM heshima kwako mkuu. Naomba nikuulize,katika list ya wauliza maswali ni nani mwenye Moral Authority ya kuuliza swali gumu kama hilo?
 
Maswali mepesi na majibu mepesi.
Mdhalo gani huo mtu ameanza kwa maswali badala ya ata kutupa into toka kwake juu ya mambo mbalimbali.
Nilichoka alipoulizwa hali ya nchi akaanza kusema kuna maeneo mvua zaimechelewa.
I though angeanza kutupa analysis economically,socially,politically etc
JK naona ata shule alikuwa tatizo
 
I know Asha Mtwangi personally
ila sikutegemea kama atakuwa ktk panel ya wahojaji.
enewei siwezi kumkosha hapa ingawa alishaacha pale kwa slava lakini bosi alikuwa mwingine.
Kuna mambo pale hakuyapenda na alishawahi kunipa warning call nilipokuwa nataka kumtokea rafiki yake mmoja wa kike.

Siwezi kumjudge kwani mie sikupoteza muda wangu kumsikiliza kikwete jana wakati najua nitanunua gazeti za leo
 
swali la msingi ni kweli chadema wamefanikiwa kuwafumbua macho umma wa tz? Ikiwa mh. Jk atashinda urais kwa urahisi au la si kwa urahisi, basi tutaona mustakabali wa nchi yetu kisiasa.

mungu ibariki tanzania

JK akishinda ndio atashika adabu kabisaa na siasa za nchi hii kwani amejua iliyo kweli kuwa 70% ya vijana wa Kitanzania hawapendi siasa na sera za CCM na mwalimu Nyerere aliwaambia zamani 1995 vyama vya siasa wakati huo vilikuwa ni vichanga na havina nguvu ila mjifunze jinsi ya kuongoza nchi katika mfumo wa vyama vingi hawakulitilia maanani hiswala na matokeo yake ndio haya sasa CHADEMA inaewafumbua macho kweli kwa mwanasiasa aliyesoma unasubilia upinzani ikufumbue macho kweli serikali aina future plan au haisomi alama za nyakati.

Pamoja na kupeleka maswali siku mmoja kabla bado lile swali la Kibonde hakulijibu hata 1%

 
[
QUOTE=Tausi Mzalendo;1190934]Asha Mtwangi siyo mtumishi wa Ikulu tena.. alikuwa enzi za kipindi cha awamu ya tatu.

Sasa hivi anafanya kazi kwenye International NGO moja ya kimarekani
Huhitaji kuwa na Elimu ya Digrii kujua kuwa bado kuna harufu ya upendeleo katika hali halisi iliyojionyesha katika mahojiano hayo.
Kulikuwa na maswali muhimu ambayo watanzania wana stahili kupata majibu ya kueleweka kama.
Hatima ya EPA,BOT,Meremeta,suala la yeye kupigia Kampeni majukwaani watuhumiwa,..............
haya yote yalikuwa maswahili muhimu na yalihitaji majibu fasaha toka kwa Rais anayemaliza muda wake!!!!!!!!!!!! 31/10/2010 ili asije pata wakati mgumu kujitetea pale waheshimiwa wabunge wetu wapya na serikali mpya na wananchi kwa ujumla watakapo taka kuwachukulia hatua za kisheria ambayo wao wameshindwa kuzichukua.
 
Hivi mlimwona meneja wa kampeni alivyokuwa akiuma meno mheshimiwa alipokuwa anasema yale ambayo hawakupanga?
 
Hata swali la Kibonde tayari alikuwa ameshaandaliwa majibu ila inaonyesha jamaa hakuwa makini kudesa...

Nilichojionea na kujifunza jana ni kuwa Congressional Corruption Movement (CCM) ni chama cha wazee ambao mbaka wafe ndipo Tanzania itakuwa na mafuriko ya maendeleo tunayoyatamania...

Wanachakachua kila kitu wakisaidiwa na mataifa makubwa ya dunia hii...

Sijui kwa nini wale wazee, wengi wakisinzia, walipelekwa pale. Licha ya Ikulu kuandaa hiyo press conference, na labda kumshauri J.K. ajibu namna gani, he was not impressive. E.g. sikuona relevance ya kuwaeleza WaTz. eti bintie anajifunza udaktari wa meno Muhimbili.
 
Nikweli mwanakijiji,asha mtwangi ni mfanyakazi wa ikuru toka kipindi cha mkapa yuko kwenye hiyo departiment.wakati huo Kikwete akiwa foregn affairs walikuwa wako pamoja nilishawahi kuongea nao wakiwa pamoja wakati wa mkutano mmoja wa SADC hapa Dar.
 
....Hivi mbona jana JK hakuhojiwa na Rose MWAKITWANGE kama ilivyokuwa imepangwa ....maana yule dada ASHA MTWANGI aliyemuhoji ni moja ya waajiriwa wa IKULU chini ya kurugenzi ya habari ........inayoongozwa na SALVA RWEYEMAMU...na kuna wengine pale wakiwamo waandishi wasaidizi waandamizi ie Primi Kabanga...na wengine waandishi ambapo mmoja wao ni Huyu ASHA MTWANGI....

SO tuseme mahojiano ya jana yaliandaliwa na kuendeshwa na kurugenzi ya mawasiliano ya Rais.....

wakuu ile ilikuwa ni sehemu ya kampeni ya ccm alikuwa anaongozwa kama mshtaki na wakili katika kueleza sera za ccm.

 
Back
Top Bottom