Yule binti aliyekuwa anataka aje kwetu kuolewa Sasa ninae Kama mke wangu

Holoholo

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2023
Posts
8,723
Reaction score
19,715
Wakuu
Kama mnakumbuka niliwahi kuleta Uzi unaohusu kuwa nilienda kuchumbia, binti akanikubali ila wazazi hawakukubaliana mahali so zoezi halikufanikiwa

Baada ya muda kidogo binti akawa ananipigia simu anadai kuwa licha ya wazazi kua hawakuelewana anataka aje kwetu kuolewa no matter what

Nilimkwepa sana mwisho wa siku nikaingia kwenye mfumo,ikatokea kumpenda Sana tumewasiliana nae kwa takribani 4months

Ndo mwezi huu akaniambia anakuja na kweli kesho yake akaja na kumfanya awe mke wangu

Wazazi wake tumewapa taarifa na hawakuwa na kauli ya kusema badala yake wakapongeza na kubariki ndoa yetu

Namshukuru Sana Mungu kwa hatua hii🙏🙏🙏🙏

Cc Shimba ya Buyenze
 
Fanya hivi:

Mkishajipanga vizuri na kutulia na hizo hekaheka zenu za sogea tukae bila mibaraka ya wazazi; na baada ya kujiridhisha kuwa kweli mko compatible anza mchakato wa kutoa mahari. Waombe msamaha hao wakwe zako. Kimila bila rukhsa na mibaraka yao hamtakuwa na ndoa na maisha yenye amani na furaha kwenu nyinyi na hata watoto wenu huko mbele ya safari. Itakuja kukuleteeni matatizo.

Usione eti wamekubali na kupongeza ukavimba kichwa. Hao wazazi wameumia; na sijui walikuwa na sababu gani kukukatalia usimuoe binti yao. Utajua kuwa wana hasira kama ikitokea ukapatwa na matatizo mf. Huyo binti yao kufariki akiwa kwako na hujamtolea mahari.

Na zingatia sana hili: Mpende sana huyo binti yao. Mtunze sana na kumheshimu. Mtendee kila lililo jema. Mpe furaha. Apendezeee. Anawiriiii. Hata wakija kumuona wafurahi na kuona kuwa walifanya makosa kukukatalia kumuoa in the first place; na kwamba kumbe wewe ndiyo ulikuwa mtu sahihi kwa binti yao.

Usikae zaidi ya miezi mitatu bila ya kupeleka ujumbe kuwa unataka kuanza mchakato wa kutoa mahari na kufunga ndoa na binti yao. Na kutumie kukataliwa kwako kama chachu ya kujiboresha wewe binafsi. Chapa kazi. Tafuta hela. Fokasi na huyo mkeo na punguza/acha michepuko. Hii ndiyo zawadi kubwa ambayo utajipa wewe mwenyewe, huyo mkeo, hao wakwe zako waliokukataa na vimalaika vyenu mtakavyokuja kujaliwa na Mungu huko mbele ya safari.

Ndiyo. Umepita njia ya mkato; na njia nyingi za mkato mara nyingi huwa zina vikwazo. Vikwepe vikwazo hivyo ili mfike muendako kwenye ndoa halali na familia iliyobarikiwa. Ni hayo tu kwa sasa dogo 🙏🏿

20250329_181156.jpg
 
Fanya hivi:

Mkishajipanga vizuri na kutulia na hizo hekaheka zenu za sogea tukae bila mibaraka ya wazazi; na baada ya kujiridhisha kuwa kweli mko compatible anza mchakato wa kutoa mahari. Waombe msamaha hao wakwe zako. Kimila bila rukhsa na mibaraka yao hamtakuwa na ndoa na maisha yenye amani na furaha kwenu nyinyi na hata watoto wenu huko mbele ya safari. Itakuja kukuleteeni matatizo.

Usione eti wamekubali na kupongeza ukavimba kichwa. Hao wazazi wameumia; na sijui walikuwa na sababu gani kukukatalia usimuoe binti yao. Utajua kuwa wana hasira kama ikitokea ukapatwa na matatizo mf. Huyo binti yao kufariki akiwa kwako na hujamtolea mahari.

Na zingatia sana hili: Mpende sana huyo binti yao. Mtunze sana na kumheshimu. Mtendee kila lililo jema. Apendezeee. Anawiriiii. Hata wakija kumuona wafurahi na kuona kuwa walifanya makosa kukukatalia kumuoa in the first place; na kwamba kumbe wewe ndiyo ulikuwa mtu sahihi kwa binti yao.

Usikae zaidi ya miezi mitatu bila ya kupeleka ujumbe kuwa unataka kuanza mchakato wa kutoa mahari na kufunga ndoa na binti yao. Na kutumie kukataliwa kwako kama chachu ya kujiboresha wewe binafsi. Chapa kazi. Tafuta hela. Fokasi na huyo mkeo na punguza/acha michepuko. Hii ndiyo zawadi kubwa ambayo utajipa wewe mwenyewe, huyo mkeo, hao wakwe zako waliokukataa na vimalaika vyenu mtakavyokuja kujaliwa na Mungu huko mbele ya safari.

Ndiyo. Umepita njia ya mkato; na njia nyingi za mkato mara nyingi huwa zina vikwazo. Vikwepe vikwazo hivyo ili mfike muendako kwenye ndoa halali na familia iliyobarikiwa 🙏🏿

View attachment 3287073
Nilitaka niandike haya,umemaliza
 
Wakuu
Kama mnakumbuka niliwahi kuleta Uzi unaohusu kuwa nilienda kuchumbia, binti akanikubali ila wazazi hawakukubaliana mahali so zoezi halikufanikiwa

Baada ya muda kidogo binti akawa ananipigia simu anadai kuwa licha ya wazazi kua hawakuelewana anataka aje kwetu kuolewa no matter what

Nilimkwepa sana mwisho wa siku nikaingia kwenye mfumo,ikatokea kumpenda Sana tumewasiliana nae kwa takribani 4months

Ndo mwezi huu akaniambia anakuja na kweli kesho yake akaja na kumfanya awe mke wangu

Wazazi wake tumewapa taarifa na hawakuwa na kauli ya kusema badala yake wakapongeza na kubariki ndoa yetu

Namshukuru Sana Mungu kwa hatua hii🙏🙏🙏🙏

Cc Shimba ya Buyenze
Mzinifu mzoefu unajisifia umepata mke
 
Kuna jamaa hapo kaongea kwa busara sana .............mleta uzi naomba umzingatie braza hapo juu.............bila shaka braza ni kam hii scenario iliwai kupita kwenye harakati zake za maisha..............
 
Bro peleka mahari hata hyo uliyo kuwa nayo peleka kwanza hakuna mzazi anayependa hayo kuona mnakojoleana tu bila ruhusa anapata wakat mgumu sana akiona wengine wapo formal.
 
Back
Top Bottom