Fanya hivi:
Mkishajipanga vizuri na kutulia na hizo hekaheka zenu za sogea tukae bila mibaraka ya wazazi; na baada ya kujiridhisha kuwa kweli mko compatible anza mchakato wa kutoa mahari. Waombe msamaha hao wakwe zako. Kimila bila rukhsa na mibaraka yao hamtakuwa na ndoa na maisha yenye amani na furaha kwenu nyinyi na hata watoto wenu huko mbele ya safari. Itakuja kukuleteeni matatizo.
Usione eti wamekubali na kupongeza ukavimba kichwa. Hao wazazi wameumia; na sijui walikuwa na sababu gani kukukatalia usimuoe binti yao. Utajua kuwa wana hasira kama ikitokea ukapatwa na matatizo mf. Huyo binti yao kufariki akiwa kwako na hujamtolea mahari.
Na zingatia sana hili: Mpende sana huyo binti yao. Mtunze sana na kumheshimu. Mtendee kila lililo jema. Apendezeee. Anawiriiii. Hata wakija kumuona wafurahi na kuona kuwa walifanya makosa kukukatalia kumuoa in the first place; na kwamba kumbe wewe ndiyo ulikuwa mtu sahihi kwa binti yao.
Usikae zaidi ya miezi mitatu bila ya kupeleka ujumbe kuwa unataka kuanza mchakato wa kutoa mahari na kufunga ndoa na binti yao. Na kutumie kukataliwa kwako kama chachu ya kujiboresha wewe binafsi. Chapa kazi. Tafuta hela. Fokasi na huyo mkeo na punguza/acha michepuko. Hii ndiyo zawadi kubwa ambayo utajipa wewe mwenyewe, huyo mkeo, hao wakwe zako waliokukataa na vimalaika vyenu mtakavyokuja kujaliwa na Mungu huko mbele ya safari.
Ndiyo. Umepita njia ya mkato; na njia nyingi za mkato mara nyingi huwa zina vikwazo. Vikwepe vikwazo hivyo ili mfike muendako kwenye ndoa halali na familia iliyobarikiwa 🙏🏿
View attachment 3287073