Yule dogo aliyekojolea quran aachiwa huru

adakiss23

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2011
Posts
4,732
Reaction score
4,901
Taarifa nilizozipata punde yule dogo wa mbagala aliyekojolea quran na kuzua tafrani ya kufa mtu pande za mbagala ameachiwa huru. Imeonekana hana hatia.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kama katoka bas ni vema kwani hata baraba naye alitoka baada ya pilato kuwauliza wayahudi kuwa nani amfungulie kati ya yesu na baraba.
 
Taarifa nilizozipata punde yule dogo wa mbagala aliyekojolea quran na kuzua tafrani ya kufa mtu pande za mbagala ameachiwa huru. Imeonekana hana hatia.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Binafsi nachukulia zile vurugu zilikuwa na source tofauti na kukojolewa kwa Q'uran, mtoto hakuwa na kosa lolote.
 
Tena alipwe pesa kwa kunyanyaswa utoto wake na watu wazima na akili zao za kuomba.
 
Ni minor kisheria huna legal stand ya kumfunga other than let him free..
 
Hatimae watanzania wawili owaliokua matatani kwa tuhuma za kukujolea kuran,wameachiwa na Mahakama kuu ya Tanzania na ile ya Kisutu. Januari 9, 2013 mahakama kuu ya Tanzania,chini ya Jaji Dk.Feruz ilitoa uamuzi wa kumpa ushindi Bi.Eva Abdalah,ambaye alikua Mrufani akipinga hukumu iliyotolewa mwaka jana na mahakama ya wilaya ya Bagamoyo iliyomtia hatiani kwa kosa la kukojolea kuran. Eva ambae ni mtoto wa IMAM mmoja wa Bagamoyo aliekutana na Injili ya YESU na kuokolewa.Hata hivyo alijikuta ktk matatizo baada ya kutokea ubishi na wasichana wenzake ambao walimuambia kua akikojolea kuran atageuka mbuzi. Ni ktk mabishano hayo, Binti huyo ambae alikua Mwokovu mpya; alitekeleza ubishi huo kwa kuikojolea kuran na hakugeuka mbuzi kama ambavyo wenzake walidai. Hata hivyo inaaminika kuwa huo ulikua ni mtego ili wapate kumshitaki.Na baada tu ya tendo hilo alishitakiwa na kesi ikaendeshwa hadi alipotiwa hatiani na Mahakama ya wilaya iliyomuhukumu kifungo cha miaka miwili jela. Uchunguzi unaonyesha kua baada ya hukumu hiyo,taasisi moja ya kutetea ukristo Tanzania iitwayo BIBLIA ni Jibu,iliandaa Mawakili kwa ajili ya kumtetea na hapo rufaa ya kupinga hukumu hiyo iliwasilishwa mahakamani.Ktk hatua nyingine, Mtoto Emmanuel Josephat aliekua akishikiliwa ktk Gereza la watoto lililopo Kisutu jijini Dsm, kwa tuhuma za kukojolea kuran ktk tukio la Mabishano ya kitoto ilitokea huko kongowe na kusababisha kulipuka kwa ghasia zilizosababisha uchomwaji wa baadhi ya Makanisa,ameachiwa huru na Mahakama ya Kisutu.; Chanzo ni Gazeti la Jibu la Maisha Jan 13-19,2013
 
hahahahahhahhhahah aisee nashindwa kuelewa tunaishi miaka mingapi kwenye hii dunia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…