Hatimae watanzania wawili owaliokua matatani kwa tuhuma za kukujolea kuran,wameachiwa na Mahakama kuu ya Tanzania na ile ya Kisutu. Januari 9, 2013 mahakama kuu ya Tanzania,chini ya Jaji Dk.Feruz ilitoa uamuzi wa kumpa ushindi Bi.Eva Abdalah,ambaye alikua Mrufani akipinga hukumu iliyotolewa mwaka jana na mahakama ya wilaya ya Bagamoyo iliyomtia hatiani kwa kosa la kukojolea kuran. Eva ambae ni mtoto wa IMAM mmoja wa Bagamoyo aliekutana na Injili ya YESU na kuokolewa.Hata hivyo alijikuta ktk matatizo baada ya kutokea ubishi na wasichana wenzake ambao walimuambia kua akikojolea kuran atageuka mbuzi. Ni ktk mabishano hayo, Binti huyo ambae alikua Mwokovu mpya; alitekeleza ubishi huo kwa kuikojolea kuran na hakugeuka mbuzi kama ambavyo wenzake walidai. Hata hivyo inaaminika kuwa huo ulikua ni mtego ili wapate kumshitaki.Na baada tu ya tendo hilo alishitakiwa na kesi ikaendeshwa hadi alipotiwa hatiani na Mahakama ya wilaya iliyomuhukumu kifungo cha miaka miwili jela. Uchunguzi unaonyesha kua baada ya hukumu hiyo,taasisi moja ya kutetea ukristo Tanzania iitwayo BIBLIA ni Jibu,iliandaa Mawakili kwa ajili ya kumtetea na hapo rufaa ya kupinga hukumu hiyo iliwasilishwa mahakamani.Ktk hatua nyingine, Mtoto Emmanuel Josephat aliekua akishikiliwa ktk Gereza la watoto lililopo Kisutu jijini Dsm, kwa tuhuma za kukojolea kuran ktk tukio la Mabishano ya kitoto ilitokea huko kongowe na kusababisha kulipuka kwa ghasia zilizosababisha uchomwaji wa baadhi ya Makanisa,ameachiwa huru na Mahakama ya Kisutu.; Chanzo ni Gazeti la Jibu la Maisha Jan 13-19,2013