Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 4,016
- 6,759
Takriban Miaka 3 iliyopita Rais aliyekuwa madarakani (hayati JPM) alitembelea gereza la Butimba, Mwanza kwa ajili ya kukagua maendeleo katika gereza hilo. Naam alijitokeza kijana mmoja ambaye alikuwa na mfungwa na kutoa tuhuma kadhaa dhidi ya askari fulani gerezani hapo.
Tuhuma zile zilimletea askari yule tafrani na kumfanya akabiliane na maswali kadhaa toka kwa hayati JPM, ilipelekea chupuchupu bwana huyo apoteze kazi yake. Baada ya hapo mfungwa yule aliomba Rais aondoke na askari huyo kwani akibaki, atamfanya
Naam siku zimekwenda. Je, yupo wapi mfungwa huyo, hali yake inaendeleaje huko alipo? Mwenye taarifa za Afande yule pia anisaidie kunijuza.
Tuhuma zile zilimletea askari yule tafrani na kumfanya akabiliane na maswali kadhaa toka kwa hayati JPM, ilipelekea chupuchupu bwana huyo apoteze kazi yake. Baada ya hapo mfungwa yule aliomba Rais aondoke na askari huyo kwani akibaki, atamfanya
kitu mbaya. JPM alimwambia abaki hapo na atamuhakikishia usalama wake (HATAMFANYA MBAYA).Naam siku zimekwenda. Je, yupo wapi mfungwa huyo, hali yake inaendeleaje huko alipo? Mwenye taarifa za Afande yule pia anisaidie kunijuza.