Yule Msanii Wa Bongo Anayesifika Kuwa Ndiyo Msanii Mfupi Kuliko Wote Amefunga Ndoa

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304

Cherekochereko! Msanii wa filamu za Kibongo, Meya Shaban ‘Aki wa Bongo Muvi’ ameachana na ukapera baada ya kufunga ndoa na msanii mwenzake, Amina Shaban, Ijumaa Wikienda lilikuwepo ndani ya nyumba.
Staa huyo wa Sinema ya Devil Kingdom ya mwigizaji Emmanuel Myamba ‘Pastor Myamba’ alifunga ndoa hiyo Ijumaa iliyopita kwenye Msikiti wa Mbezi, Tanki-Bovu, Dar na kufuatiwa na bonge la sherehe katika Ukumbi wa Mbezi Beach Park.
Aki akiwa na mke wake. Katika shughuli hiyo iliyohudhuriwa na wanahabari wetu, ilipambwa na watu mbalimbali wakiwemo mastaa wa filamu za Kibongo.

Shughuli hiyo ya kukata na shoka iliwashangaza watu kutokana na maharusi hao majina ya baba zao kufanana huku wageni waalikwa wakisema kwamba ikitokea hivyo ndoa huwa inadumu kwa muda mrefu.

Baadhi ya wageni waliohudhuria sherehe hiyo ya harusi.
Akizungumza mbele ya wageni waalikwa, Aki wa Bongo Muvi alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kuwa ametimiza ahadi ya ndoa kwani mara ya kwanza walikutana na mkewe kwenye Chuo cha TFTC cha Pastor Muyamba na kuanzisha urafiki hadi wakafikia hatua hiyo ya ndoa.
Ukumbi ukiwa umelipuka kwa burudani.
 
Huyo mkewe anafanana na Jack wa Macao
 
Ile muvi ni Devil kingdom au God's kingdom
 
Huyu Aki wa Bongo inabidi atafute sana pesa maana mabazazi wako kazini baada ya hili tukio..,ila wadada wa bongo muvi lazima watajiuliza mwenzao kafata nini hapo ndipo watakapoumia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…