Money Stunna
JF-Expert Member
- Aug 9, 2011
- 13,053
- 6,304
Cherekochereko! Msanii wa filamu za Kibongo, Meya Shaban Aki wa Bongo Muvi ameachana na ukapera baada ya kufunga ndoa na msanii mwenzake, Amina Shaban, Ijumaa Wikienda lilikuwepo ndani ya nyumba.
Staa huyo wa Sinema ya Devil Kingdom ya mwigizaji Emmanuel Myamba Pastor Myamba alifunga ndoa hiyo Ijumaa iliyopita kwenye Msikiti wa Mbezi, Tanki-Bovu, Dar na kufuatiwa na bonge la sherehe katika Ukumbi wa Mbezi Beach Park.
Shughuli hiyo ya kukata na shoka iliwashangaza watu kutokana na maharusi hao majina ya baba zao kufanana huku wageni waalikwa wakisema kwamba ikitokea hivyo ndoa huwa inadumu kwa muda mrefu.
Baadhi ya wageni waliohudhuria sherehe hiyo ya harusi.
Akizungumza mbele ya wageni waalikwa, Aki wa Bongo Muvi alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kuwa ametimiza ahadi ya ndoa kwani mara ya kwanza walikutana na mkewe kwenye Chuo cha TFTC cha Pastor Muyamba na kuanzisha urafiki hadi wakafikia hatua hiyo ya ndoa.
Ukumbi ukiwa umelipuka kwa burudani.
