Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Ukiondoa mambo yote ambayo yalitokea kwenye mechi ya Brazil Vs Tanzania kilichosisimua ni kisa cha shabiki mmoja kukatiza uwanjani na kwenda moja kwa moja kwa Kaka na kumkumbatia. Ni wazi jamaa alikuwa amedhamiria kufanya hivyo, alipiga mahesabu na kutekeleza kwa kiasi kikubwa.
Ni wazi kulikuwa na kuvunjika kwa usalama kiasi ambacho kinatia aibu.. lakini wakati mwingine ndio burudani ya soka..
Angalia mwenyewe..
PICHA: Saleh Ally
Ni wazi kulikuwa na kuvunjika kwa usalama kiasi ambacho kinatia aibu.. lakini wakati mwingine ndio burudani ya soka..
Angalia mwenyewe..
Vitu vingine kuvifanya inahitaji ujasiri wa kipekee. Kitendo alichokifanya shabiki huyu cha kuingia uwanjani kwa lengo la kwenda kumkumbatia mchezaji maarufu wa Brazili Kaka, kilikuwa ni cha kipekee, japo hakuwa na nia mbaya, lakini alihitaji ujasiri. Kamera yetu ilinasa tukio zima hatua kwa hatua...jamaa aliingia uwanjani huku akiita KAKA, KAKA, akiwa mikono juu kuashiria kuwa hana silaha yoyote, ...na hii ni hatua kwa hatua ya tukio zima....
..kafanikiwa kumfikia kaka na kumkumbatia
..bila hiyana kaka naye akampokea na kisha kum pet mgongoni...
...na kisha kuondoka naye hatua chache huku amemkumbatia kishkaji
...kisha anamuaga,,,jamaa anaondoka kwa furaha
...haya kwaheri mshikajii
....kaka kakaa kakaaa!!!!!!!