Yule shabiki wenu aliyemkumbatia Kaka - yataka moyo!.

Tanzania kila kitu uchunguzi ebo!!! Hao wanaomshikilia mpaka leo hawajui kuwa hivi vitu vya kawaida tuu heheh bahati nzuri hakuvua ngua na kukatiza uwanjani uchi, wamuachie tu wampe onyo labda na masaa 2-3 ya community service.
 
HII KALI!
ILA PAMOJA NA KUFANYA TUKIO LA KUHATARISHA AMANI KWA WACHEZAJI...BADO HUYU KIJANA HASTAHILI ADHABU KUBWA... wenye makosa ni walinda usalama....
Hivi kazi ya polisi uwanjani ni nini?
 
Ah ah ah Bongo tambarale, full kujiachia...!
 


Kijana ameachiwa na kesha kuwa celb, kuhojiwa clouds fm muda si mrefu ujao ndani ya powerbreakfast
 
Last edited by a moderator:
...Niliwasifu jinsi walivyompokea bwana mdogo baada ya kukatisha kiwanja... bila kumpiga Virungu!!
 
wamsamehe tu maana ndio hivyo tena ,utoto na mambo ya emotions, ingawa alifanya makosa.
 
Green Acres, miaka 21? Kibabu hicho!

Kwa mpangilio wa elimu ya Tz mbona yupo sahihi? Ameanza darasa la kwanza 7 years + 7 = 14..+ 4 = 18+ 2...20 Tukumbuke kuna wale ambao wanashndwa kwa sababu mbali mbali kuanza wakiwa na hiyo miaka 7 na pengine kusubiri miaka kadhaa baada ya kumaliza darasa la saba kuendelea na elimu ya sekondari. Hii ndio Tanzania jamani mbona tunakuwa wageni na system zetu?

Issue ni system hizi za kuanza shule kwa umri wa miaka saba na hili la kusoma kwa miaka 15 kati ya shule za awali mpaka sekondari linahitajika?

<input id="gwProxy" type="hidden"><!--Session data--><input onclick="jsCall();" id="jsProxy" type="hidden">
 
Kijana alisukumwa na dhana ya" it happens once in a life time". Wamwachie tu maana ametusaidia kutuonyesha jinsi polisi wetu walivyo wazembe wanapokuwa kazini.
 
Hivi wazee mnafahamu unazi na munkari wa soka?????
Huyu kijana kufanya hivyo ki-usalama haikuwa sahihi lakini munkari wa soka ukipanda [wapenzi wa soka wanaelewa]kuna mambo unaweza kuyafanya ambapo ukiulizwa baada ya munkari kushuka usiwe na maelezo.
 
Jana nimesikia kwenye taarifa dogo ameachiwa na polisi, issue yake wameipeleka kwenye vyombo vinavyohusiana na maswala ya mpira; updates please.
 
... kijana huyo licha ya kufanya kosa lkn ni wazi ni jambo amablo kama mtanzania anaependa michezo sio geni kutokea..
Hata mtu akibaka leo, aachiwe kwa kuwa jambo hilo sio geni kutokea !!? Sababu za kuachiwa zinaweza kuwa nyingine, lakini si hiyo ya kusema kosa fulani ni kawaida kutokea.
 
Teh, teh, teeeh!!!!
Nayo ilikuwa sehemu ya mechi (burudani). Mimi binafsi na wengine wengi tu tuliburudishwa na kitendo kile ''pindi ile kilipotokea'', maana hakuna mtu aliye tegemea kumuona yule bwana mdogo akiingia uwanjani na kumkumbatia kaka.

Ila cha msingi tu ni kwa vyombo vinavyohusika kuzuia kitendo kama hicho kisitokee tena.
 
Polisi jamii ni neno zuri ila utekelezaji wake hauna maana.Mtu anaingiliwa kwake na majambazi wanamjeruhi na kuiba kila kitu lakini bado unaongelea polisi jamii.Shame on you!
 
Hili suala linatakiwa limalizwe haraka saana tena kiutawala kuliko kisheria, anaweza kupewa onyo la kipolisi, tu, lakini wakushughulikiwa na walinzi wa usala kwa uzembe na pili kuchukua sheria mkononi.
Mwema onyesha kwa mba upo fasta fasta kwenye utendaji, urasimu wa nini.
 
Kijana ameachiwa na kesha kuwa celb, kuhojiwa clouds fm muda si mrefu ujao ndani ya powerbreakfast

najaribu kuimagine kama mashabiki kama kumi wangekuwa na wazo na furaha kama ya dogo kwa wakati mmoja!sijui wenyewe ndo wangeoneana aibu au sisi watazamaji?kudiscourage watu wapendao umaarufu wa design hii vyombo vya habari vya uingereza vimeamua kutorusha matukio kama hayo na pindi yatokeapo huonyeshwa wachezaji tu na mtangazaji ndo atazungumzia.....
 
Yule jamaa kwanza anaakili mno hadi kufanikiwa kufanya jambo kama lile!! atafutiwe kazi hata ya usalama maana anaweza kilisaidia sana taifa kwenye kazi za kishushushu....duh kweli saoka lina uchizi wake! afagie ofisi za TFF siku mbili tu then aachiwe ndiyo soka hilo..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…