Yupi alikuwa bora kati ya Costantine Kimanda Vs George Magere Masatu

Wahenga wa kabumbu la bongo, ulimkubali beki yupi kwa ubora enzi hizo kati ya Costantine Kimanda (Yanga) na George Magere Masatu (Pamba, Simba)?
Kimanda alikua ni beki aliyekamilika kuanzia skills mpaka physic yake. Japo Masatu alikua beki mahiri lakini in comparison between the two, George Masatu umbo lake dogo na ufupi vinamuangusha
 
Kimanda alikua ni beki aliyekamilika kuanzia skills mpaka physic yake. Japo Masatu alikua beki mahiri lakini in comparison between the two, George Masatu umbo lake dogo na ufupi vinamuangusha
Lakini mkuu Fabio Cannavaro licha umbo.lake dogo na ufupi akicheza kama beki wa kati ni mshindi wa kombe la dunia mwaka 2006 akiwa kama nahodha wa Italy na baadae mwaka huo alitwaa Ballon D'or.
 
Lakini mkuu Fabio Cannavaro licha umbo.lake dogo na ufupi akicheza kama beki wa kati ni mshindi wa kombe la dunia mwaka 2006 akiwa kama nahodha wa Italy na baadae mwaka huo alitwaa Ballon D'or.
Ni kweli kabisa mkuu umbo la Cannavaro halikua kikwazo kwake kua miongoni mwa mabeki bora kabisa kuwahi kutokea Italy

Ninachosema hapa ni kwamba Kimanda na Masatu wote walikua na control ya hali ya juu, utulivu na umakini unaotakiwa hasa kwa mabeki wa kati, ila Constantine Kimanda alikua na umbo lililotisha zaidi amabalo ni muhimu sana kwa mabeki

Actually kwangu mimi Kimanda alitakiwa awe wa kwanza kucheza soka Ulaya kwa mafanikio hata kumzidi Nonda Shaaban Papii
Sijui alikumbwa na masaibu gani hadi akapotea kwenye ulimwengu wa soccer
 
George Masatu ndo alinifanya niipende simba. Kwake mpira ulikuwa haupiti na haupotei kizembe hata kidogo.
Hiyo pekee inamfanya awe mchezaji bora kabisa wa ukabaji(beki) kuwahi tokea pale simba na hata Tanzania kwa ujumla.
 
George Masatu ndo alinifanya niipende simba. Kwake mpira ulikuwa haupiti na haupotei kizembe hata kidogo.
Hiyo pekee inamfanya awe mchezaji bora kabisa wa ukabaji(beki) kuwahi tokea pale simba na hata Tanzania kwa ujumla.
Yondani anamfunika Magere
 
George Magere Masatu, moja ya mabeki bora kabisa waliowahi kupitia simba ninaowakubali mpaka kesho, wengine ni Boniface Pawasa na Victor Costa Nampoka Nyumba.
 
Sio haki kumlinganisha George Masatu na Constantine Kimanda. Nitakupa sababu mbili. George Masatu amecheza muda mrefu sana Simba na Tanzania kuanzia 1992-1997 then ile ya 2000-2002. Kimanda amecheza msimu mmoja tuu Yanga wa mwaka 1994. Masatu ametwaa kila Kombe na Simba . Ubingwa wa Bara 94, 95 na 2001, Muungano, 1993 na 95 na Africa Mashariki na Kati 1992, 1995, 1996 na 2002 achilia mbali makombe kama Hedex na Tusker Challenge Cup na kufika fainali ya Kombe laCAF 1993. So amekuwapo nyakati zote za mafanikio ya Simba akiunganishwa na timu imara na golikipa imara Mohammed Mwameja nyakati hizo.

Kimanda yeye kacheza Yanga mwaka 1994 pekee msimu ambao Yanga hawakuwa na mafanikio na wakifungwa 4-1 na Simba huku goli pekee la Yanga likifungwa na Kimanda kwa njia ya faulo. So huwezi mlinganisha mchezaji mwenye mechi nyingina mafanikio mengi na mchezaji wa msimu mmoja tuu tena asiye na mafanikio katika huo msimu.
 
Good analysis Chamakh, lakini beki bora kabisa kwa Simba japo alicheza muda mfupi kwa mafanikio locally 1990, lakini akaharibiwa na pesa za Gulamali ni Deo Njohole. Alikuwa na uwezo mkubwa wa kuusoma mchezo, na kunyang'anya mpira kwa washambuliaji mguuni, kutoa Pasi za uhakika, hanyang'anyiki mpira mguuni. Japo umbile dogo ana uwezo kukaba aina yoyote ya forward, waulize Makumbi Juma na Sanifu Lazaro. Aliweza kumsoma vizuri golikipa wake Mackenzie Ramadhani, na kumfanya huyu Mrundi aonekane star, yaani hajapatikana Deo mwingine.
 
Ndio mana amesema huwezi shindanisha mchezaji wa muda mrefu mwenye mafanikio na yule wa muda mfupi asiye na mafanikio.
 
Rekodi zinaonyesha hivyo...Yondani kacheza mechi nyingi zaidi Taifa stars na CAF champions league...ana medali nyingi zaidi za ligi kuu..
Fanya reference post #10 hapo juu alichokiandika chamakh ndio ukweli wenyewe, Weka mahaba kando mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…