Sababu za kutovutiwa na wa kwanza:
.....kwanza hajui kukiss nimejaribu kumfundisha ila naona hataaaa haelekei. Sijui midomo (lips) yake migumu na midogo..hata sielewi.
Sipendi harufu ya kinywa chake, mwili wake hata akitoka kupiga mswaki au kuoga.
Pumzi yake ndo sitaki kabisaaaaaa akinihemea nashindwa kuhema. Kuna muda hata anishike vipi nahisi kama naumia na hata kama nilikua na nyege zinapotea.
Nikuulize maswali na nijibu yote.
Mwenyewe anayajua haya?
Kama hayajui yote, umeshawahi kumwambia kwa uwazi kabisa (face face) kuwa hupendezwi na haya?
Kama ulishawahi kumwambia, alisemaje?
Whatever the case, kama yuko tayari kujibadilisha, uko tayari kumsadia?
Kama alikuwa hana haya mambo ungempenda kwa dhati?
Nimeuliza hayo maswali kwa sababu hayo yote uliyoyataja hapo juu yanatatulika.
Kwa mfano, suala la kissing, kimsingi anayetakiwa ku-lead kwenye kissing ni mwanamke, na sio mwanaume.
Tatizo labda hajui jinsi ya kukufanya wewe u-lead in the kissing bila hata kujishtukia. There is a way he can learn this.
Hata tatizo la pumzi mbaya linatatulika.
Kuhusu kulingana umri wala sioni tatizo hapo.
La muhimu ni kama hayo uliyoeleza hapo yakitatuliwa utavutiwa nae?
Kuhusu huyo wa pili unadai:
He is a perfect kisser!!!
Sio siri kama kuna kitu wanakiita soul mate huyu ndie
pale linapokuja suala la mapenzi romance, sex, cuddling…etc he is very good.
Tatizo la huyu kaka wa kazini sasa, mawasiliano kwake ni F.
Anapenda sana Pombe na marafiki kwa hiyo anaweza kukaa wiki mbili bila kukutana nami
Hajawahi kunipa chochote kama zawadi au hela hata vocha ya 500
Pia umedai huyu ana girlfriend.
Tatizo kubwa la huyu ni kwamba tayari ana girlfriend lakini he is cheating on her with you.
Kwa haraka haraka, kama angeamua kuachana na girlfriend wake na kuwa na wewe, kuna uwezekano mkubwa he will cheat on you too.
Remember a cheater is always a cheater.
Kuhusu communication kuwa F, mawasiliano ni muhimu sana kwenye mahusiano.
Kinachonishangaza hasemi kuwa sababu za kuwa na mawasiliano hafifu na wewe ni kwa sababu ya girlfriend wake.
Anakupa sababu ambazo possibly hata mkiamua kuwa pamoja atakuwa anakupa wewe pia.
Umesema he is a perfect kissers, lakini ninavyojua it is actually the woman who lead the man during the kissing.
Mambo ya mapenzi sijui romance, sex, cuddling, etc, yanafundishika kwa mwanaume yoyote unless hataki.
Pombe ni mbaya hasa kama anakunywa sana. Ni wanaume wachache sana wanaokubali kuacha pombe.
Hilo la kutokukupa chochote nalo ni indication kubwa kuwa moyo wake upo wapi.
Kuhusu kuwa soul mate, hata sijui kama kuna kitu kama hicho hapo. Soul make wakati unasema communication yale ni F?
Nafikiri wewe unaona kama ni soul mate, lakini sidhani kama yeye anaona hivyo.
Otherwise, angekuwa ameshamwacha huyo girlfriend wake kitambo.
Ulishawahi kumpa ultimatum is either you or his girlfriend? Alisemaje? If not, try that and will make your job easier.
But to me hakuna soul mate hapo. Soul mate ya kazini ibakie huko huko kazini.
Personally, nilishakuwa na marafiki wa kike so closely to the extent watu wakadhani tunabanjuana, but we never even kissed.
We have moved on na hata sijui wengine walipo sasa lakini watu bado wanadhani 100% kuwa tulikuwa tunabanjuana.
Ndio soul mate wa shuleni na makazini hao. Nothing more.
Ni hivi:
It is important to know that any relationship can be a soul mate relationship, so please don't take it for granted. However, many times, when we meet someone, we feel so close, so bonded to them that we believe they are our soul mates. Then over time, problems arise, but since we were left to believe that it would be a "perfect union", we are often puzzled and confused when conflict does rear its ugly head.
Huyu wa pili naona tayari kuna matatizo kama lack of communication na yeye kusema uongo but you still believe he will be a "perfect union". Sidhani.
Nashindwa nichague Yupi???
Definitely huyo wa pili hakufai. Yes, nasema kama mwanaume hakufai. Utakujajuta baade. Majuto mjukuu.
Hata kama akiamua kuachana na girlfriend wake, na kuwa na wewe atakuja kukuumiza huko baadae. Trust me on this.
Kuhusu huyo wa kwanza, siwezijua mpaka unijibu maswali niliyokuuliza hapo juu kwanza.
Lakini na wewe sio msafi pia to the extent ya hata ya kuolewa na huyo wa kwanza.
Umem-cheat huyo wa kwanza. Kwa hiyo huna tofauti na huyo wa pili
Naambiwa there is no perfect man ila kipi bora katika ndoa???
Exactly. There is no perfect man on earth. Neither there is a perfect woman.
Kwa vile no one is perfect, kilicho bora katika ndoa ni compromise.
Ndoa nyingi zina-survive kwa sababu ya compromise. Win a little loose a little.
nahitaji kuwa na familia baada ya mwaka mmoja na nusu tangu sasa.
Hili nalo tatizo tena linaweza kuwa kubwa sana.
Usipokuwa makini utachagua mtu ambaye humtaki simply because you want to have a family as soon as possible.
Suala hapa sio kuwa na familia ndani ya mwaka na nusu, bali kuwa na the right person wa kuanzisha familia.
Na hili ndilo linalokufanya ku-stick na hao wanaume wawili badala ya kuwa open in your searching
Waliosema haraka haraka haina baraka sidhani akama walikosea.
Don't limit your choice to two men simply because you want to have a family within one and half year.
Kumbuka familia inapangwa na maamuzi ya watu wawili, na sio wewe tuu.