Yupi bora kati ya mvuta sigara na mnywa pombe?

Yupi bora kati ya mvuta sigara na mnywa pombe?

MLUGURU

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
2,929
Reaction score
3,710
Nipo kwenye daladala hapa Buguruni Makumbusho. Kuna mabishano kati ya konda na abiria kuhusu yupi bora kati ya mvuta sigara na mnywa pombe.

Konda anasema mvuta sigara ni bora maana akishavuta anapiga mswaki anakuwa fresh ila wanawake wanampinga wanasema mvuta sigara anaboa mana mwili unanuka sigara na ndani kuna nuka sigara.

Konda anaendelea: Mnywa pombe, pombe haishii mdomoni tu, bali mpaka chooni akienda kukojoa pombe inaonekana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sigara ina madhara makubwa sana. Kumbuka sigara inaleta madhara kwa Second Smokers yaaani wale waovuta moshi pindi mvutaji anapokuwa anaburudika, lakini pia kuna THIRD SMOKERS wale wanaokutana na masalia kwenye nguo za Mvutaji, matandiko nk.

Madhara yake siyo ya siku hiyo hiyo bali athari zake ni za muda mrefu kwa Mvutaji, Mkewe, Watoto, Waliokaribu nao nk. Kwa kifupi Mapafu, akili na Mfumo wote wa Hewa huathirika vibaya na Sigara.

Pombe madhara yake mara nyingi ni kwa Mtumiaji pekee na mara chache huwapata Second na Third parties kwa maana ya kupata athari zitokanazo na Walevi kusababisha ajali au maamuzi mabovu. Pombe husababisha Ugonjwa wa Akili, Sonona, Kukosa muda wa kuzalisha mali nk.

Vyote ngoma drooo tu. Lkn pombe wapo wanaoimudu na kuifanya Starehe isiyo na madhara yaani kutumia kadri ya Uwezo wa miiili yao. Imeandikwa Drink Responsibly
 
Mkulima ni bora kuliko kulima tumbaku. Sio sigara tu hata kunywa pombe ukiwa unalima haileti mvua sana sana wakifika jamhuri na wimbo mmoja wa zamani
 
Kimazingira Bora Sigara wazee
Lakini Sigara inaonekana ina madhara Zaidi kiafya
 
Hakuna alie bora kati yao wote ni waathirika tu, labda mwenye afadhali.
Nipo kwenye daladala hapa Buguruni Makumbusho. Kuna mabishano kati ya konda na abiria kuhusu yupi bora kati ya mvuta sigara na mnywa pombe.

Konda anasema mvuta sigara ni bora maana akishavuta anapiga mswaki anakuwa fresh ila wanawake wanampinga wanasema mvuta sigara anaboa mana mwili unanuka sigara na ndani kuna nuka sigara.

Konda anaendelea: Mnywa pombe, pombe haishii mdomoni tu, bali mpaka chooni akienda kukojoa pombe inaonekana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee achana na madhara ya mapafu sijui maini mimi hata siyajui. Mimi nikishaona mtu anavuta sigara huwa najikuta namhusisha na tabia zingine kama ukatili, wizi n.k....samahani wavuta sigara najua wengine nawakosea ila ndio saikolojia yangu imejengeka hivyo nimejitahidi kubadilika sijaweza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usifananishe fegi na vitu vya ajabu. Yani walevi mara watukane, walale mitaroni, wajinyee, wabebe bar maids[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Pombe kitu cha ajabu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom