NguoYaSikuKuu
JF-Expert Member
- Jul 3, 2013
- 681
- 1,020
Hodi Jamvini,
Nawasilisha mada hapo juu kuhusu dhana ya MaCEO's ambayo huku ipo lakini naona bado ipo duni sana.
Kwenye suala la utendaji hatupimani kabisa kuhusu performances. Unakuta mtu ni mtendaji mkuu wa kuajiriwa iwe ni sekta binafsi au serikali yupo miaka mingi lakini bado Shirika au kampuni inadumaa au haikui na mtendaji mkuu yupo pale pale hana presha. Ni kwamba watu wengi wanafanya kazi ili wapate mishahara.
Upande wa serikali wanavyoteua mtendaji mkuu sijui kuna vigezo gani huwa wanazingatia au mtu anapewa tasks gani kabla ya uteuzi. Wapo wengi wanateuliwa miezi sita tu wanatumbuliwa na unakuta mtendaji mkuu huyo anatoka TANESCO anaenda labda EWURA etc
Kuna hili la DART unakuta wameweka kamba za kufungia ng'ombe za Manilla kwenye stand kama kutenganisha Abiria yaani ubunifu ni zero kabisa. Hapo unakuta kuna viongozi wapo na mtendaji mkuu ana zaidi ya miezi hajaoia vituoni. Ilimradi mishahara unaingia hana shida.
Sekta binafsi pia kuna baadhi ya watendaji wakuu pia huoni perforamances zao ni kwamba bora liende tu. Mfano mkubwa kuna TV imeanzishwa miaka ya 90's hapa mtendaji wao ni yuleyule na ukiangalia ile TV ni kama imepitwa na wakati kuanzia kwenye ubora wa picha mpaka utendaji mzima. Unajiuliza hapa mtendaji mkuu anawaza nini?!!
Ukiangalia Clouds Fm kuna utofauti mkubwa sana toka Ruge afariki unaona kabisa imepwaya. Alikuwa mbunifu sana aliyependa kazi yake kwa dhati. Unaona mi mtu ambaye hakuwa pale kwa Ajili ya mshahahara ni passion zaidi.
Wenzetu watu walioendelea mtu anakuwa mtendaji mkuu , kwanza ni kitu anakijua na Kukipenda na hasa Taasisi au kampuni nyingi zinaajiri CEO kwa kuleta matokeo chanya na uboreshaji.
Hapa nikianza kuorozesha mashirika mfu na watendaji wakuu bado wapo kazini nitajaza pages mbili. Ni kwamba watu hawajali iwe Serikali au Sekta binafsi tupo nyuma sana.
Kwa nchi zetu hizi masikini tukianza kupimana kwa ubora tutafika mbali na kama tukiendelea kubebana kwa kuogopana tutaishia kuwa dampo la Wazungu.Waasia na Waarabu.