Yupo wapi Askofu Zacharia Kakobe?

Yupo wapi Askofu Zacharia Kakobe?

Sema nini..
Yule Askofu injili zake za miaka ya nyuma (nyingi nilikua naziskia kwenye radio cassette ya Mshua) zilikua ni balaa,,
Yaani anakemea hadi unasema naacha dhambi😬😬
🤣🤣🤣🤣 Aiseee!
 
Habari zenu nyote!

Kama kichwa cha habari kilivyouliza, Naendelea kuuliza yuko Baba yetu, Jasiri aliyekemea dhambi bila kificho na kujitengenezea maadui wengi kwa kuupigania Ukristo na utakatifu???

Mara ya mwisho alionekana akiwa na mpendwa wetu aliyetutoka late rais magufuri. Baada ya hapo hajaonekana tena.

Injili ya kanisa imepoa sana, despite kuwa na wingi wa matukio lakini ukimya wake ni pigo kubwa kwa injili Tanzania na duniani kote.

Mimi si muumini wake, lakini injili yake nimekuwa naiishi na imenileta karibu zaidi na Mungu kwa miaka mingi sana...


Tafadhari KWA WEMA kabisa, Tujuzane alipo Askofu wetu huyu.


Ahsante.
Yupo Ulaya anatumia zile pesa zenu mlizomjazia miaka nenda rudi.
 
Watu na bahati zao, unakusanya Watu unawachangisha ili uishi maisha ya utajiri na ufahari kwa kumsingizia Mungu.

Hivi ni kwa nini Wasichangishe wakawasaidia Wenye uhitaji wa kweli na wao wakabaki wakiishia maisha ya kawaida?....hiyo si ndio haswa kazi ya Mungu?.
 
Back
Top Bottom