Nakubaliana na wewe kabisa maana kuna Wataalamu wengi sana toka SUA na UDSM ambao wanakwenda huko kufanya kazi, hata hivyo wabongo wanao baki hapa ni kwa ajili ya uzalendo tuRwanda kuna opportunities nyingi tu za kazi, tena kazi za kule zinalipa vizuri tu ukilinganisha na bongo. Kama mtu umefanikiwa kupata kazi Rwanda au nchi yoyote ile ya east africa ni bora uende na ufanye. Nilikuwepo Huko Kigali, wabongo wengi tu wapo wanafanyakazi na life inaenda vizuri tu.
Karudi kwao Rwanda....
Hahaha unanichesha hapa kidogo, maana unaweza kujua kwa kiasi gani Taifa la Tanzania halithamini mchango wa Watanzania wakiwa ndani....SIAMINI KAMA NI MTANZANIA,UKIANGALIA POST ALIZOSHIKA RWANDA UNAWEZA KUHISI KITU.
Kama ni Mtanzania basi ana asili ya huko Rwanda na ameamua kurudi kwenye asili yake aweze kuwasaidia wanao muhitaji.
ni kweli kabisa,acha watu wafanye kazi mahali ambapo umuhimu wao unaonekana kuliko kujali uzalendo ambao hauna manufaa yoyote,warwanda ni watu wazuri tu kufanya nao kazi,Hahaha unanichesha hapa kidogo, maana unaweza kujua kwa kiasi gani Taifa la Tanzania halithamini mchango wa Watanzania wakiwa ndani
Huyu jamaa ali'cut' na ku'paste' curricula ya uhandisi ya UDSM huko KIST. Kelele za bure.. hakuna cha chuo cha mfano wala nini ... pia tembelea KIST -utakuwa dissapointed.
Halafu huyu jamaa arudi hali ilishafika saa 11? Kama alipata PhD miaka 35 iliyopita atakuwa amefikia umri wa kustaafu. tuagalie mbele
Kuna mama mmoja Professor Masanja alikuwa idara ya Math UDSM aikwenda Sabattical leave KIST,mpaka leo hajarudi bado yuko huko anakula bata!!!!!
Kuna Wanataaluma Kibao wanaondoka kwenda Nje kwa ajili ya kufanya kazi huko, Na Taifa linabaki likiwa halina uwezo wa kufanya mamboNamjua huyu mama...kasomea Ujerumani na ana binti yake anaitwa sijui Angela na kijana aitwaye Moses
Kwa mtazamo wa haraka tunaweza sema hiyo ndio sababu. Lakini hii trend ya watu wengine wengi kwenda huko huko inatoa picha nyingine tofauti kwamba kuna kitu watu wanakikimbilia kule. Kama tungekuwa watu wa kutafuta majawabu ya kuondoa tatizo tungelisema kuwa ok kuna issues nyingine zaidi ya kukimbilia kwenye asili.Ila tulivyo tuna majibu rahisi kwenye maswali magumu kama kawaida.....SIAMINI KAMA NI MTANZANIA,UKIANGALIA POST ALIZOSHIKA RWANDA UNAWEZA KUHISI KITU.
Kama ni Mtanzania basi ana asili ya huko Rwanda na ameamua kurudi kwenye asili yake aweze kuwasaidia wanao muhitaji.
Mkuu wangu kuna haja hata serikali yetu kuona na kuwajengea mazoea ya kuona watu kama hawa wanarudi Tanzania na kufanya kazi hapa Tanzania, Sasa Jk anaweza kufanya na kutoa motisha ya kutosha na kuwafanya watu hawa warudi Tanzania na Kujenga Taifa letu Tanzania
Kuna Wanataaluma Kibao wanaondoka kwenda Nje kwa ajili ya kufanya kazi huko, Na Taifa linabaki likiwa halina uwezo wa kufanya mambo
Kama Kingunge bado anadunda mzigo mpaka leo ina shida gani kwa huyu prof? Halafu kama kichwani hajazeeka, nani anayekura hasara? Badala ya kumtumia kwa consultancy kwenye maeneo mengi ya kitaalamu eti tunasema imefika saa kumi na moja.
Kwenye hii ni TZ zaidi ya uijuavyo.Prof Luhanga alipotoka tu UDSM akaenda kufundisha Uingereza...sasa na yeye sio mzee?
Nchi yetu bwana...wataalamu ndio wanazeeka, wanasiasa wanazidi kuwa vijana kadri muda unavyokwenda.
Nafurahi kama nimekuchekesha maana kucheka katika fikra hizi ni kitu adimu sana. Luhanga alikwenda sabatical leave uk baada tu ya kuondoka madarakani.Wacha kuchekesha watu mkuu,Kingunge anadunda mzigo gani? kazi kulala fofofo pale bungeni huku akijua noti zinaingia kila kona pale Ubungo!
Kwa taarifa yako Prof Luhanga sasa hivi anakula tu laga yake karibu na maskani yake, hana mradi wowote wa kitaalam.
Tatizo kubwa la wataalam wetu ni kutegemea ajira ya serikali kukidhi maisha.
Kuna miradi mingi ambayo wangeweza kufanya(siyo kufuga ng'ombe na kuku) na kushirikiana na wataalam wengine duniani, hapa Tanzania.
Hata hivyo wale wataalam waliojitolea kufanya hivyo wanapigwa vita sana na waaalam hao hao walioajiriwa serikalini, Mfano ni wa Dr Masau wa Heart Institute.