Yupo wapi Professor Silas Lwakabamba Mtanzania Mwanzilishi wa Kigali Institute-KIST

Samahani san Mkuu Koba, Ainea Kimaro SiYO Proffessor wa KIST, ila a talented technical person.
Miradi uliyyoitaja kaifanya huko Rwanda na sasa yupo Ukonga na anafanya vitu vyake.
Alikuwa Ofisini kwangu last week, hivyo nafahamu ninachikiongelea
Kweli sasa mbona mambo haya Watanzania wanashindwa kufanya ndani ya Nchi yao Tanzania
 
Kweli sasa mbona mambo haya Watanzania wanashindwa kufanya ndani ya Nchi yao Tanzania
Mkuu Josh,watu wa aina ya Ainea Kimaro wapo, tena wengi sana ,nchini kwetu.
Mimi nimeshuhudia vijana wadogo walioanza na mtaji wa elimu yao tu, na sasa wamefika mbali sana.
Matatizo ni mengi lakini lazima tuondokane na mentality ya kuajiriwa na kupewa maofisi makubwa makubwa yenye viyoyozi.Kama mtu ni kijana na akapewa ofisi za aina hiyo huo ndio mwisho wa taaluma yake-and I am serious.
Nimeshuhudia wahandisi wengi tena wenye taaluma nzuri tu, wakiishia kuwa technical cabbages baada ya miaka kumi ya kuvaa suti na kupandishwa mashangingi ya serikali.
Baada ya miaka kadhaa wakijilinganisha na wenzao walioingia kwenye technical field kwa kujitegemea wanakuwa nyuma sana kimaisha.
Si kwamba watu tecnical wasiingie utumishi wa serikali la hasha , lakini inabidi waingie zile field zinazoelekea kuwa relevant na masomo yao ya taaluma.
 
Mi nataka kujiajiri kama contractor ila njia ya kupita imejaa mbigiri na miba. Nimebobea katika fani za mitambo na umeme
 
Mi nataka kujiajiri kama contractor ila njia ya kupita imejaa mbigiri na miba. Nimebobea katika fani za mitambo na umeme
Nakuunga mkono mkuu kwa azma hiyo.
Kuna kijana pale Mbezi ambaye ameanzisha kampuni yake ya miundombinu ya mawasiliano,yuko katika jengo la SHAMo na sasa anaendelea vizuri sana.
I am proud of this guy.
Mbigiri na miiba usiogope mkuu, hizo zipo tena nyingi sana.Cha msingi ni jinsi ya kuziona hizop mbigiri na kuzitanzua.Huwezi kuziona ukiwa nje ya mchezo-sharti uingie ngoma na uicheze.
Kijana mwingine contractor wa umeme namfahamu ameshiriki katika miundombinu ya umeme wa Uwanja wa Taifa mpya,spidi ya maendeleo yake inatia moyo.
Nchi hii itaendelezwa na sisi wazalendo na si taifa jingine , hasa wataalam wachache tulio nao.
 
Wakuu wote nawatakia kila la kheri la kuanzisha mambo haya Tanzania maana utakuta kuwa vijana wengi sana wana metality kama hiyo ya kuajiliwa Tanzania hivyo kufanya fani hiyo isiwe na nguvu katika mambo mengi sana
 

Wiki hii huyu jamaa Amechaguliwa Waziri..wa Miundombinu.......

Mnafikiri huyu alikuwa Mtanzania au mrwanda ?
 
Hivyo kasomeshwa na kodi zetu alafu anatumika nchini kwake? Jamani Tanzania kuna shida sana hapa
 

Nafikiri unamuongelea Bisanda aliyekuwa Wizara ya kilimo ambaye amefariki mwaka juzi, au ni yule mdogo mtu maana wte ni maprof hawa. Ila hii nchi inatakiwa ifanyiwe review
 
Nafikiri unamuongelea Bisanda aliyekuwa Wizara ya kilimo ambaye amefariki mwaka juzi, au ni yule mdogo mtu maana wte ni maprof hawa. Ila hii nchi inatakiwa ifanyiwe review
Wafanye review alafu? endeleeni kulala kupiga majungu kuutukuza udini na makorokocho ya kila aina.
 
Na wew uko nyuma na wakati Prof. Bisanda aliisharudi yuko Chuo kikuu huria.
 
kwa heshima anayopewa huyu profesa rwanda,kurudi Tanzania ni ndoto
NI Mnyaru na amekuwa Waziri wa Elimu huko Rwanda. Jana kwenye habari ITV waliogopa kulitamka jina lake lote wakaishia kusema Rais Paul Kagame amefanya mabadiliko ya mawaziri katika hao wapwa yuko Prof. Silas. sasa sijui waliogopa kumalizia jina lake lote la Rwakabamba kwa kuwa ana pasi ya Bongo na alikuwa anaishi kama mbongo. au ............

Sasa ukishakuwa Waziri kuna cha kujificha tena. Ila bado Serikali yetu wanaweza kuwa hawajui kuwa amekuwa Waziri.

Prof. Rwaka siyo mbaya kiukweli na huko kwao wanaruhusiwa kuwa na raia zaidi ya moja na familia yake iko Bukoba kwa nshomile na watoto wake wengine wanafanya kazi Ikulu ya Rwanda na wengine wako Bongo, Tatizo katiba yetu hairuhusu kuwa na raia zaidi ya moja. Na hawa watu hata wakiwa na raia mbili wanapenda sana kwao kuliko sisi Wabongo tunavyopenda kwetu. angalia akina Prof. Rwakabamba, engineer Butare na wengineo wengi Wanatumia UTZ lakini wote wako Rwanda wanajenga kwao. Kiukweli hawana makosa makosa ni yetu sisi tuliolala Usingizi.
 

Kagame appoints don of Tanzanian
origin minister Wednesday, 27 February 2013 22:01 By The Citizen Correspondent
Kigali. President Paul Kagame of
Rwanda has appointed a professor of
Tanzanian origin, Silas Lwakabamba, as
his minister for Infrastructure in a
cabinet reshuffle announced on Tuesday. President Kagame reshuffled his cabinet
bringing in new faces as well as
creating new portfolios.
Among the new faces in the cabinet
include Prof Lwakabamba, who
originates from Tanzania. According to information obtained from
The Citizen sources in Rwanda, Kagame
has been satisfied and impressed by
Prof Lwakabamba’s performance in
various posts he has been holding. He
has also granted him Rwandese nationality. The source said Rwandese have also
commended the head of state for
putting interests of Rwanda first when
appointing Prof Lwakabamba. “The people here in Kigali have
commended the appointment and they
praise President Kagame...I have not
heard anyone complain on the origin or
nationality of the appointed minister,”
said the source. Born and educated in Tanzania, Prof
Silas Lwakabamba went to the
University of Leeds in the UK for his
training in Engineering. After
graduating with a BSc (1971) and a PhD
(1975) in Mechanical Engineering, he returned to Tanzania to join the staff of
the Faculty of Engineering, which had
just started at the University of Dar es
Salaam.
He progressed rapidly through the
ranks and attained his professorship in 1981. He gained managerial experience
along the way. He became Head of Department,
Associate Dean, and eventually Dean of
the Faculty of Engineering. In 1985, Prof
Lwakabamba joined the UN- sponsored
African Regional Centre for Engineering
Design and Manufacturing (ARCEDEM) based in Nigeria, as a founding Director
of Training and Extension Services. He became the founding Rector of
Rwanda’s Kigali Institute of Science and
Technology (KIST) in 1997, and, in 2006,
he was appointed the Rector of the
National University of Rwanda, the
largest public institution of higher learning in that country, a position he
occupied until Tuesday’s appointment.
 
Hivi orign maana yake nini. Yule alikuwa MTZ wa kujisajili sio wa kuzaliwa. that's why karudia orign yake unyaru.
 
Huyu Jamaa kweli gwiji kubwa sana katika fani ya hiyo ambayo kama kweli Watanzania wangeona anafaa basi angeweza kuwa msaada mkubwa sana katika Tanzania
 
Kweli Kama Taifa hili tungeliona haya yote basi Kagame anawaza mbali sana kuliko sisi. KIST ya kule Rwanda wanakwenda mpaka vijijini na kwenda kuwafungia watu madish haya ambayo leo Tanzania tunasema satellite hivyo kuna umuhimu mkubwa sana kwa serikali yetu kuwapenda na kuwathamini watu kama hawa
 
Ki -ukweli nampa sifa moja tu ni mchapakazi hodari hana longolongo alipokuwa KIST walikuwa wanaiita ya WTZ alivyohamishwa tu WTZ wote wakafukuzwa siku hizi KIST jina, sio ileeeeeeeeeeee.

Naona hatimaye ameamua abaki na uzalendo wake. ila pasi yetu vipi? maana hakuna awezaye kuwatumikia mabwana wawili.

Halafu Rwanda wana asili moja kuwatumia wageni kwa muda wakisha pata wanachohitaji wanakutosa. halafu wao wanaendelea. ndio maana kwao huwezi kukuta eti sekta muhimu zimebinafsishwa only in TZ tulibinafsisha mpaka management ya Tanesco kwa makaburu, Tumebinafsisha shirika la ndege leo liko wapi, angalia Reli wale wahindi walivyo tufanya? kweli chezea shamba ya bibi weye. hayo madini aku. mpaka miaka mia. tuachiwe mashimo yetu. na mikataba feki. yaani tumeuzwa. kwa mfano hayo madini yangekuwa ndio wao wanayo nafikiri hivi sasa management wangekuwa ni wao tu na hata viwanda vya kusafisha na kuchakata vito vingekuwa vimejengwa. sura nyeupe wangekuwa washauri tu. si unaona wanavyoshirikiana kuwapelekesha Wakongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…