DodomaTZ
Senior Member
- May 20, 2022
- 197
- 233
Wakati zoezi la uchukuaji na urudishaji fomu Chama cha Mapinduzi (CCM) likiendelea kada wa Chama hicho Yussuf Kaiza Makame nae amejitosa kuwania kiti cha Uwakilishi Jimbo la Mtambile Mkoa wa kusini Pemba.
Kabla ya hapo Kaiza amewahi kuwa Mkurugenzi wa Baraza la Mji Mkoani na kuitumikia vyema nafasi yake hiyo, ikiwemo kuimarisha maendeleo na kuongeza kodi ya Serikali kama ilivyo dhamira ya Rais wa Zanzibar Dkt.Hussein Ali Mwinyi.
Kaiza ameiambia Jamii Forume ameamua kuchukua fomu kuomba ridhaa ya Chama Chake ili aendelee kuwatumikia Wananchi wa Mtambile, kuhakikisha dhamira njema ya Dkt.Husein Ali Mwinyi inaendelea kuonekana kila mahala katika Jimbo hilo kama ilivyo sasa.
Amesema iwapo Chama Chake kitampa ridhaa ya kupeperusha bendera anaamini atafanya vyema zaidi kwa sababu yeye ni sehemu ya uzawa wa Jimbo hilo,anafahamu namna watu wanavyopongeza na kuhitaji maendeleo.
"Dkt.Mwinyi amefanya maendeleo makubwa kila mahala sasa anatajwa yeye ni lazima apate watu madhubuti zaidi kumsaidia, kumaliza kazi ili kufuta kabisa upinzani baada ya uchaguzi wa mwezi Oktoba" alisema.
Kaiza katika uzoefu wa kisiasa amepata pia kuwa Mbunge wa Chake Chake Pemba na kubeba uzoefu mkubwa katika shughuli za uwongozi na kuwatumikia watu.