Nchaby
JF-Expert Member
- Aug 12, 2013
- 797
- 259
Wakuu, hapa pameniwea pagumu kuelewa. Lakini naamini katika jukwaa hili, wapo watu waliobobea na waelewa historia ya biblia kwa kiwango cha juu mno kisicho na shaka.
Biblia ninayoisoma inataja Yusufu mwana wa Yakobo aliyeuzwa na ndugu zake utumwani Misri (Mwanzo 37:2-36)
Vilevile, inataja Yusufu mwana wa Yakobo; fundi seremala aliyemchukua Mariamu kuishi naye na hatimaye kuzaliwa kwa mtoto Yesu Jerusalem katika banda la ng'ombe (Mathayo 1:16)
Hapa nashindwa kuelewa!
Yusufu aliyeuzwa na ndugu zake utumwani Misri, ndiye baadae alikuwa fundi seremala na kumlea mtoto Yesu alipozaliwa?
Au hawa Yusufu ni watu wawili tofauti?
Historia ya maisha wana wa Israel ni ndefu sana na wakati mwingine haiko wazi sana kiasi kwamba sisi wengine ambao siyo wabobezi wa maandiko tunapata shida sana kuelewa na kupambanua kwa kina maandiko.
Maisha ya wana wa Israel yamejawa na kuanguka na kusima mara kwa mara. Vile vile historia inasema mara zote wana wa Israel walipotii sheria za Mungu na kukubali kufanya kazi yake; maisha yao yalikuwa yenye furaha, amani na mafanikio makubwa kinyume chake ilikuwa ni kuanguka na kukumbwa na mateso.
Baada ya hawa wateule wa kufanya kazi ya Mungu, kutoka utumwani Misri, inasemekana, walianguka tena, wakawa watumwa kwa mara nyingine tena!
Wajuzi na wabobezi wa maandiko, nisaidieni; hili taifa teule la Mungu, nini kiliwakumba kwa mara yapili na hatimaye kwenda kuwa watumwa?
Ni taifa gani liliwatumikisha kwa mara nyingine Waisraeli na walishikiliwa utumwani kwa kipindi gani?